CHADEMA waonywe kwa tabia ya kuwatukana na kuwadhalilisha Askari wetu katika mikutano yao ya hadhara

Askari hawawadhalilishi bali wanaambiwa UKWELI ,chadema wanaposema wao Askari wanatekeleza Amri za wanasiasa za kuua raia huku hawapati faida yeyote hadi Viatu walivyovaa havijulikani kama ni vya kushoto au kulia maana vipo uelekeo mmoja ,shati hadi limepauka wakati wanasiasa wanaowatuma wakula asali na maziwa huku wao wakipigwa JUA na kuishi kwenye nyumba za FULL SUTI huku Abdul akinunua vifaa vya ndani vya Bilioni 2.
 
Walioua watu kama majani hawakuonywa na wala hawajaonywa ila wanaowalinda na kuwatetea Watanzania waonywe hakika wahi Mirembe kwani jinsi dishi linavyoyumba mwishowe dish na wewe mtaanguka na ukichelewa hutanyanyuka tena kamwe abadani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…