CHADEMA wawasha moto Bungeni, Bulaya auliza swali zito kwa Waziri, Mdee naye ajiandaa

CHADEMA wawasha moto Bungeni, Bulaya auliza swali zito kwa Waziri, Mdee naye ajiandaa

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,721
Reaction score
21,959
Kwa sisi wakazi wa Bunda hii barabara ni muhimu sana.

=====

Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA Ester Bulaya, leo ameingia Bungeni pamoja na baadhi ya wabunge wenzake wa chama hicho na kueleza kuwa suala la kutokamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara limekuwa ni tatizo sugu na kuhoji ni lini barabara ya Kisorya, Bunda itakamilika.

Ni katika Kikao cha Kwanza cha mkutano wa pili wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ndipo alipouliza swali hilo kwa Wizara ya Ujenzi, huku akieleza kuwa mchakato wa ujenzi wa barabara umechukua takribani miaka 15 sasa.

"Uchelewashwaji wa ukamilishwaji wa miradi ya barabara limekuwa ni tatizo sugu, hapa ninapozungumza ujenzi wa barabara wa kutoka Kisorya, Bunda, ahadi na uanzaji wake umechukua takribani miaka 15, sasa nataka kujua ni lini hiyo barabara itakamilika kwa sababu ikikamilika inaunganisha na barabara ya Serengeti na imekuwa kilio kikubwa kwa wananchi wa mkoa wa Mara", amesema Mbunge Ester Bulaya.

Ikumbukwe kuwa Ester Bulaya na wenzake 18, walikwishafukuzwa Uanachama na chama chao cha CHADEMA, baada ya wao kwenda kula kiapo cha ubunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama chao, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni wasaliti.

Chanzo: EATV
 
Salary sleep na erythrocyte njooonii muone wabunge wenu wachadema jinsi wanavyokiwakilisha chama chenu vyema hapa bungenii. Kwakweli wanawake ni jeshi kubwaa. Tunakipongeza chama chenu kwa kutuletea majembe bungenii
Pongezi zirudi kwenye chama chenu mliowapeleka hao covid 19 bungeni na sio Kwa chadema
 
Mwisho wa siku temper ikishashuka, uongozi wa CHADEMA utakuja kugundua kwamba faida za kuwaacha hao kina mama Bungeni ni nyingi kuliko hasara zake na hili saga litaisha kimyakimya (kama bado halijafa)

Normally “you go to war with the army you have....not the army you might wish to have at a later time”
 
Alivyokuwa mbunge wa jimbo hilo alikuwa hatetei wala kulisemea alikuwa kazi kupinga tu ohh maendeleo sio vitu ni watu

Naona sasa akili zimewarudia porojo za Lisu na Chadema za kusema maendeleo sio vitu wameziitupilia mbali na kumrushia Lisu na Amsterdam wake
 
Back
Top Bottom