CHADEMA yaingia zama za kuengua, kusimamisha na kufukuza wanachama wake kama vibaka

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni kipindi ambacho chadema itadhiofika zaidi kwenye medani ya siasa huku wanachama wake wenye hekima na busara wakijiengua mapema kuepuka aibu ya ukosefu wa hekima na busara miongoni mwa viongozi wao dhidi ya wanachama wao.

Ni zama ambazo utovu wa nidhamu na kutwezana utu vitaonekana ndio ujasiri miongoni mwa viongozi wake hususani wapya.

Kwa hekima na busara zao viongozi wengi wa chadema katika ngazi mbalimbali za uongozi wa kitaifa, Kanda, mikoa, wilaya na hata kata wataomba kuachia ngazi na kujiudhulu nafasi zao kuwepa uropokaji na ukosefu wa ustaarabu kwenye uongozi wa juu.

Kama mdau wa siasa, ukizingatia 4rs za Dr.Samia Suluhu Hassan, unadhani chadema imepoteza uelekeo kwa kiasi gani, achilia mbali kwenye suala la rushwa?πŸ’

Mungu Ibariki Tanzania
 
 
Bado hujasema mpaka upwite!
 


Mbona kwenye Chama pia kuna watu wamejiengua? Na kuna watu walifukuzwa?

Kwenye siasa hayo ni mambo ya kawaida sana

Kila mwenyekiti anakuja na mpango kazi wake

Hata mwenyekiti wenu ana mpango kazi wake
 
Kama mdau wa siasa, ukizingatia 4rs za Dr.Samia Suluhu Hassan, unadhani chadema imepoteza uelekeo kwa kiasi gani, achilia mbali kwenye suala la rushwa?πŸ’

Mungu Ibariki Tanzania
4rs za Samia yeye kama nani Chadema???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…