Pre GE2025 CHADEMA yakusanya zaidi ya Milioni 64 kupitia kampeni ya Tone Tone

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 03 Machi 2025, Makao Makuu ya Chama Mikocheni Dar es salaam ametoa taarifa ya kiasi kilichokusanywa tangu kuzinduliwa kwa mkakati maalum wa TONE TONE uliolenga kushirikisha umma kukichangia Chama, ambapo mpaka tarehe 1 Machi, amesema jumla ya TSh. Milioni 64,315, 150 ilikuwa imepatikana kupitia TONE TONE

Soma, Pia
 
Mwanzo Mzuri.. Ila pesa bado ndogo.. Kulinganisha na umma. Kikubwa nina ona ni ile spirit ya kuchanga... Ukiweza shawishi mtu akuchangie pesa ni wazi ume mshawishi akupigie kura. Sasa usikute pesa yote wana changia diaspora hapo ndiyo kuna Chamgamoto.
 
Mshahara wa CEO wa Vodavom wa mwezi mmoja.
Tundu Lissu atakufa kwa presha,kuendesha vyama kunataka hela
Watanzania tuko milioni 64 na imepayikana milioni 64 ina maana kila mtanzania kachangia shilingi moja
 
Halafu wewe ni Mtanzania maskini sana kabla ya Lissu, kweli Kuna watu hamna shukrani
 
Mshahara wa CEO wa Vodavom wa mwezi mmoja.
Tundu Lissu atakufa kwa presha,kuendesha vyama kunataka hela
Watanzania tuko milioni 64 na imepayikana milioni 64 ina maana kila mtanzania kachangia shilingi moja
Kwa muda mfupi walioanza, na changamoto walizokutana nazo tunaweza kusema wameanza vizuri sana. Bado tunaendelea kuchanga kila mwezi. Najua wewe unasubiri kwa hamu Lissu afeli lakini Mungu alivyo mkubwa si ajabu wewe ndiye utakayekufa kwa pressure mwaka huu.
 
Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 03 Machi 2025, Makao Makuu ya Chama Mikocheni Dar es salaam ametoa taarifa ya kiasi kilichokusanywa tangu kuzinduliwa kwa mkakati maalum wa TONE TONE uliolenga kushirikisha umma kukichangia Chama, ambapo mpaka tarehe 1 Machi, amesema jumla ya TSh. Milioni 64,315, 150 ilikuwa imepatikana kupitia TONE TONE

Soma, Pia
Mbona vihela vidogo sana hivyo? Mnajua gharama za kuendesha chama nyie?
 
Hongereni sana CHADEMA.

Na hapo Vodacom walikuwa wanarudisha miamala. Sasa wasingerudisha ingekuwaje?

Mungu azidi kuwatangulia mfanikishe lengo lenu.

Ushauri wangu. Tafuteni pia namna ya ku monitor hiyo michango yenu electronically. Kama wameweza kuzuia michango isifike hawashindwi pia kuwaibia kimtandao account ikawa na pesa kidogo.
 
Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 03 Machi 2025, Makao Makuu ya Chama Mikocheni Dar es salaam ametoa taarifa ya kiasi kilichokusanywa tangu kuzinduliwa kwa mkakati maalum wa TONE TONE uliolenga kushirikisha umma kukichangia Chama, ambapo mpaka tarehe 1 Machi, amesema jumla ya TSh. Milioni 64,315, 150 ilikuwa imepatikana kupitia TONE TONE

Soma, Pia
Japo pesa ni TONE lakini hiyo ndio nguvu ya TONE TONE...
 
Hicho chama hakifadhiliwi na wauza unga, hiyo ni nguvu halisi ya watanzania wa chini.
Mbona mna mabasha zenu wa Ulaya wanawafadhili ndio chanzo Cha mapovu ya kibaraka Lisu baada ya kuulizwa na Balile 😆😆
 
Hela ndogo kivipi ikiwa Tone Tone imezinduliwa usiku tarehe 27 Feb kuamkia Feb 28 na kufikia Machi 1 wamepata hicho kiasi cha fedha?
Hivyo ni vihela vidogo sana na watu soon wanachoka na hapo ni Nchi nzima lakini hamjafikia hela za Mbowe 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom