Waliompiga ndo hao wanaohaha sasa kumpeleka matibabu sijui Dodoma sijui India?! Mchawi amejiweka wazi mepamaaa.Yaan wamempiga na kumuumiza mdada wa watu, badala wafuatilie anaendeleaje na hali ya majeraha na mtihani wa maumivu anayopitia baada ya kipigo cha nguvu,
Chadema wanafuatilia mienendo ya siasa za mgonjwa alielazwa, dah!
Masuala ya utu kwa viongozi wao hasa wanaopata matatizo ni mtihani sana ndani ya chadema kwakweli,
ndio maana kauli mbiu ya CCM inasema,
Kazi na utu, tusonge mbele pamoja 🐒
Ok Chadema hiyo ya utu kama mnayo mlienda hospitali kumuona huyo kiongozi wenu mwenezi? Huyo sio kiongozi wa CCM ni wa kwenu wenyewe tena wa kitaifa kwa nini hamukuenda hospitali? Hata kuhakiki tu kwa kweli amepigwa au anafeki bila kujali kama alipigwa na mtu wa Chadema au laHii roho ya utu, upendo na ya kuguswa mmeianza lini nyinyi viumbe mnaofahamika duniani kote kwa kuwateka watu mchana kweupe na kwenda kuwatesa/kuwaua!
Nyinyi ambao mnawakata mapanga wanachama wa Chadema kupitia kile kikundi chenu cha Green Guard, na hamfanywi chochote!!
Kuna watu walilamba asali iliyojaa simtank la lita 10,000 lkn cdm bado inadunda sana tu, sasa huyu ambaye tumemjua baada ya kudundwa hata akitumiwa na Wasira hakuna hata madharaIpo wazi anatumiwa na CCM kuleta mtafaruku
Hakika, Na apuuzwe tuKuna watu walilamba asali iliyojaa simtank la lita 10,000 lkn cdm bado inadunda sana tu, sasa huyu ambaye tumemjua baada ya kudundwa hata akitumiwa na Wasira hakuna hata madhara
Mbona kina Soka huwapiganii kama huyu?Yaan wamempiga na kumuumiza mdada wa watu, badala wafuatilie anaendeleaje na hali ya majeraha na mtihani wa maumivu anayopitia baada ya kipigo cha nguvu,
Chadema wanafuatilia mienendo ya siasa za mgonjwa alielazwa, dah!
Masuala ya utu kwa viongozi wao hasa wanaopata matatizo ni mtihani sana ndani ya chadema kwakweli,
ndio maana kauli mbiu ya CCM inasema,
Kazi na utu, tusonge mbele pamoja 🐒
Huijui CCM vizurAnatumiwa vipi na CCM? Au alikuwa anashirikiana na Noel? Badala ya kumlaumu aliyempiga nyinyi mnamlaumu aliyepigwa.
Mngemuacha arudi na kuongea mngepata hasara gani?
Amandla
Msichoelewa ni kuwa tunategemea CDM wata behave tofauti na CCM. Ndio maana tunasikitika tunapoona wanafanya yale yale ambayo wanawashutumu CCM. Na kibaya zaidi ni pale ambapo badala ya kusikitikia tukio, wao wanasema mbona CCM wanafanya haya haya!
Amandla...
Mtu aende bar kulewa, apigwe afu asingizie Chadema?Angekuwa dada yako ungeongea ujinga wako huo?Inaonekana ninyi CHADEMA wote ni wakatili wa kijinsia
gentleman,Mbona kina Soka huwapiganii kama huyu?
Hapa ndipo ELIMU yenu ya Propaganda inapokwamia.
CCM watakupinga tu hata kama hawakuwepo eneo la tukio kama ulivyotoa huu ushuhuda wako.Kwa nini mnakuwa watu mnaopenda uwongo? Ni wapi CHADEMA imesema kuwa ni halali kupigwa kwa sababu na CCM wanafanya hivyo hivyo?
Mimi nilihudhuria kikao cha ndani cha Njombe. Ukisikia yanayosemwa mitandaoni kuhusiana na kilichotokea kwenye kikao, zaidi ya 50% ni uwongo.
Kikao kile cha ndani, hakikuwa cha siri, na Heche alisema wazi kuwa hata wanachama wa kawaida wanaruhusiwa kuhudhuria ili washuhudie viongozi wao wanayoyajadili. Kwa sababu kikao kilikuwa open, sioni shida hata kutamka yale yaliyotamkwa na kutokea mle ndani:
Baada ya Heche na Dr. Slaa na Mwakajoka kuelezea dhima ya NO REFORM NO ELECTION, Heche alisema kuwa anataka kusikia maoni na hata maswali kutoka kwa wote waliohudhuria. Akawaomba wanaotaka kuongea wanyoshe mikono, alipooona ni wengi, aliomba waorodheshwe majina, na akasema wazi kuwa kila anayetaka kuongea apewe nafasi. Yeye yupo tayari kuwasikiliza hata kama itakuwa ni mpaka asubuhi. Waliojiorodhesha walikuwa 37.
Heche akawaambia wajumbe kuwa kwa idadi hiyo, kila mmoja akiongea kwa dakika 3, itachukua daki 111. Kama kila mmoja ataongea kwa dakika 2, itachukua daki 74. Akawauliza wajumbe wanataka kila mmoja aongee kwa dakika ngapi, akawataka wanaotaka dakika 3, wanyoshe mikono, wakanyosha watatu tu. Wengine wote wakasema dakika 2.
Utaratibu wa kuongea ulifuata mpangilio wa uandikishaji majina. Lakini ulibadilika ghafla baada ya Sigrada kuonesha kuwa anataka kuongea. Kwa sababu ya heshima ya nafasi yake akapewa nafasi ya kuongea, tena bila ya kuzingatia zile dakika 2 ambazo wajumbe wengine walikuwa wanapewa.
Sigrada, kwa mara ya kwanza alikatisha mpangilio wa kuongea, baada ya kiongozi wa jimbo la Makambako kudai kuwa viongozi wa kitaifa na hususani Sigrada, wanawadharau viongozi wa majimbo, akadai kuwa Sigrada aliandika barua kwa OCD kuwataarifu polisi kuwa anafanya mkutano wa hadhara Makambako, bila ya wao kupewa taarifa. Taarifa waliyopewa ni kuambiwa tu waende kwenye mkutano. Malalamiko hayo ndiyo yaliyomwinua Sigrada na kukatisha mpangilio wa kuongea. Heche aliivumilia hali hiyo, akamwachia Sigrada aongee. Aliongea mengi sana, lakini kikubwa alidai kuwa viongozi hao wa Makambako na mkoa wanamhujumu. Baada ya pale, viongozi wa mkoa, BAWACHA mkoa, viongozi wa Makambako na viongozi wa kanda, walihojiwa na Heche. Jambo ambalo halikuwa la kawaida ni kwamba, Sigrada alipokuwa anaongea, wote walikaa kimya, lakini hao viongozi wengine wakihojiwa, wanapotoa maelezo Sigrada alikuwa hawezi kutulia, aliinuka na kuwakatiza wenzake. Tena anasimama na kuongea kwa kunesanesa.
Heche mara kadhaa alimsihi atulie, Sigrada alisema hawezi kutulia kwa sababu wanasema uwongo. Alipoambiwa akae chini, aligoma. Heche akamwambia kuwa kama hawezi kutulia ni aheri atoke nje, Sigrada akasema kuwa itakuwa afadhali. Heche akamwambia, haya toka nje, Sigrada akatoka nje, huku anaenda anaongea. Alitoka mwenyewe, hakuguswa na yeyote.
Huku nyuma, Heche alisikitika sana, na akasema mbele ya wajumbe kuwa Sigrada amemvunja sana moyo kwa sababu alimheshimu sana. Akasema kuwa hata kabla ya kugombea nafasi aliyo nayo yeye Heche, Sigrada ndiye aliyempigia simu na kumwomba agombee. Baada ya maneno hayo ya Heche, Dr. Slaa alisimama na kusema kuwa watu wote wamehuzunishwa na alichofanya Sigrada, lakini baada ya kutolewa nje, anaomba arudishwe, apewe nafasi nyingine, pengine kwa kutoka nje atakuwa ametafakari. Akatumwa mtu kwenda kumwita. Lakini muda wote alipokuwa nje tulikuwa tunasikia anaongea kwa kelele. Alikuwa anaongea na nani? Alikuwa anaongea nini?, labda waliokuwa nje ndio wanaojua.
Tulichoshangaa, hata baada ya kutumwa mtu kwenda kumwita, Sigrada hakurudi tena ukumbini. Muda aliotolewa ilikuwa majira ya karibia saa saa 4 usiku. Kikao kikaisha majira ya saa 6 usiku. Tunatoka nje, hatukumwona Sigrada, polisi walikuwa bado wapo, mlinzi wa Heche alikuwa bado yupo.
Baada ya pale baadhi wa wajumbe wakasema hawawezi kulala njaa, wakaenda kwenye baa moja ambayo ni kama night club kwa sababu ipo wazi masaa 24. Wakamkuta Sigrada hapo baa. Muda wote, hakukuwa na taarifa yoyote kuwa kuna mtu amepigwa. Nina hakika wengi, ni kama mimi hatukujua kama huko nje kuna mtu yeyote alikuwa amepigwa. Kwa sababu sikuwa huko nje, siwezi kusema kwa uhakika kama Sigrada alipigwa au hakupigwa, na kama alipigwa, siwezi kujua alipigwa na nani. Lakini, logically, kama alipigwa, basi haikuwa kiasi cha kuumizwa sana maana kama angekuwa ameumia sana, sidhani kama angeenda baa badala ya kwenda hospitali.
Lakini pia, polisi walikuwepo pale nje ya ukumbi, muda wote wakati kikao kinaendelea, kama waliona mtu anatendewa jinai, kwa nini hawakuchukua hatua dhidi ya mhalifu? Kama kweli alipigwa na mlinzi wa Heche, mlinzi yule alikuwepo pale mpaka mwisho wa kikao, na aliondoka na Heche saa 6 usiku. Muda huo wote, wa zaidi ya saa 1, kwa nini hao polisi hawakumkamata huyo mlinzi wa Heche wakati polisi na huyo mlinzi, wote walikuwa nje ya ukumbi wa kikao?
Sigrada kama kweli alipigwa, iwe alipigwa sana au kidogo, siyo hoja, swali kubwa ni kwa nini polisi hawakumchukulia hatua huyo mhalifu hapo hapo wakati wa utendaji kosa?
Kumsaidia anayeumwa siyo tatizo, iwe anaumwa kwa sababu ya kipigo au kwa matatizo mengine ya kiafya. Cha kushangaza ni CCM kulifanya tukio hilo kama mileage ya kisiasa dhidi ya CHADEMA. KAMA CCM wangekuwa na dhamira njema wangeweza kutoa mchango wao wakamkabidhi Sigrada au familia yake. Wangeweza kumsaidia kugharamia usafiri kama kuna haja hiyo. Lakini jukumu la kumhudumia mgonjwa lingebakia kuwa la familia na ndugu wa karibu. Lakini CCM wamemgeuza Sigrada kama kitu cha maonesho. Hali hii inatia mashaka makubwa juu ya dhamira ya CCM dhidi ya Sigrada.
Angalizo:
Ukiona mtu alikuwa adui yako, ghafla anabadilika na kujifanya rafiki na mtu wa karibu sana kwako, chukua tahadhari kubwa.
Maombi yangu kwa Mungu: Mungu amwepushe Sigrada na kila dhamira mbaya iliyojificha dhidi yake. Na tunamwomba Mungu awaaibishe waovu wote na mipango yao mibaya, na uovu ule waupangao dhidi ya Sigrada na chama chake. Uovu waupangao dhidi ya Sigrada au chama chake, uwarudie maradufy na kwa namna ya kujutia.
Tunaogopa hata kwenda kumjulia hali Sigrada kwa sababu ya kuhofia kuwa unaweza kwenda, halafu waovu wakaitumia hiyo nafasi kumfanyia uovu kwa kisingizio kuwa uliyeenda kumwona ndiye mhusika.
Mungu wetu ni mkubwa, hata katika hili, waovu wataumbuka.
Umeeleza mengi sana na karibu yote yanathibitisha kuwa palikuwa na mvutano ndani ya kikao. Kwa maelezo yako ni kuwa palikuwa na shutuma dhidi yake na yeye akajitetea kuwa hizo shutuma sio za kweli.Kwa nini mnakuwa watu mnaopenda uwongo? Ni wapi CHADEMA imesema kuwa ni halali kupigwa kwa sababu na CCM wanafanya hivyo hivyo?

CCM watakupinga tu hata kama hawakuwepo eneo la tukio kama ulivyotoa huu ushuhuda wako.
Rafiki, Kuna kusema na kuropoka! Hapa umeropoka kupitiliza! Ushahidi wa hayo uliyoyaandika unao?Hao si ndio waliomwua Chacha Wangwe? Hata mzee Kibao walimwua wenyewe, wanafanya chokochoko vyombo vya ulinzi na usalama visiwachekee. Mh. Rais hakuna maridhiano ktk usalama na amani ya nchi hii. Jifunzeni DRC, ile nchi imeshamegwa tayari.
Yaani polisi walikuwepo na walishuhudia mtu akipigwa na hawakuchukua hatua! Uliwahi ona wapi polisi wa aina hiyo? Halafu upigwe Kisha upate nguvu za kwenda bar! Hebu scrutinize maelezo ya mleta hoja na uisome kwa utulivu kabla hujaihoji la sivyo utaiharibu.Umeeleza mengi sana na karibu yote yanathibitisha kuwa palikuwa na mvutano ndani ya kikao. Kwa maelezo yako ni kuwa palikuwa na shutuma dhidi yake na yeye akajitetea kuwa hizo shutuma sio za kweli.
Kitu ambacho hamkielezi vizuri ni huyo aliyetumwa kumfuata Sigrada alitoa sababu gani za kutorudi nae. Mtu haonekani kwa masaa mawili hata hamstuki?
Hiyo hoja ya kwa nini polisi hawakumkamata Noel haina mashiko maana inawezekana walisita kufanya hivyo baada ya Sigrada kuamua kujiondokea bila kudai mtu akamatwe. Bila shaka waliona huo ni ugomvi wa ndani ya CDM na wangeingilia wangeangushiwa jumba bovu.
Naona mnakazania kuwa kwa vile mlimkuta Sigrada Bar basi bila shaka hakuumia. Ninavyojua mimi mara nyingi watu wanaopata trauma hasa ya kichwa huwa wanajisikia hawajambo baada ya tukio. Si ajabu effect ya kipigo ( concussion ) ikaonekana baadae. Na dalili zake ni kama alizosema alikuwa nazo Sigrada. Kupoteza fahamu, kizungu zungu, kutapika n.k. Mtu anaweza hata kupoteza uhai.
Wewe kama mwanasiasa unashangaa nini kuona CCM wanatafuta kick katika suala hili. Hawakuanza na Sigrada.
Unakosea unaposema kuwa kupigwa au kutopigwa kwa Sigrada sio hoja. Kuwa hoja ni kwa nini polisi hawakumchukulia hatua Noeli. Polisi wasingeweza kuchukua hatua yeyote bila ushirikiano wa Sigrada. Kama Sigrada alisema hajaumia sana wasingeshughulika na Noel. Wameanza kumtafuta Noel baada ya hali ya Sigrada kuonekana kama imebadilika. Ukweli ni kuwa kupigwa mtu hata kama ni kidogo sio suala la kulifumbia macho. Ndio maana tunashangaa kwa nini CDM ilichukua muda mrefu ku reaction? Hivi Makalla angewakuta watu wa CDM wako pamoja na Sigrada angeweza ku take advantage?
Ninachoshangaa ni kuwa wote mnaosema kuwa tunapotosha mnakiri kuwa hamkuwa eneo la tukio. Mnajuaje kuwa Sigrada anasema uongo kama hamkuwepo?
Mimi nataka niamini kuwa Heche ana nia ya dhati ya kuponya vidonda vya uchaguzi. Lakini kwenye hili ameteleza. Kwa vile huko Njombe kuna mtu wao wa karibu sana walipaswa kufanya kila jitihada ili Sigrida asijione mpweke katika kikao na baada ya kikao. Ati mnaogopa kwenda kumtakia hali Sigrada kwa kuhofia kusingiziwa! It does not make sense kabisa.
Kwa kweli hatua mlizochukua na mnazochukua mnatufanya sisi wengine tuone kuwa Sigrada hataweza kutendewa haki maana mmeisha muona kama adui yenu. Hilo ni kosa kubwa ingawa inaelekea hamlioni. Kwa ushauri wangu kaeni na wakina Sigrida na muwa hakikishie kuwa wana nafasi katika chama chao. Kaeni pia na wale wanaodai kuwa wanawaonea, muwaambie kuwa uonevu wa aina yeyote haukubaliki.
Sigrada na wenzie ni wapambanaji. Sio watu wa kuwapoteza kirahisi rahisi.
Amandla....
Nadhani hauelewi tu maana ya "trauma" na "concussion ". Kutokana na simulizi za Sigrida ni kuwa alipigwa ngumi akaangukia kichogo. Alipoanguka alipoteza fahamu kidogo lakini baada ya hapo akaondoka akaenda nyumbani. Na alianza kujisikia vibaya sana alipokuwa nyumbani kwake. Kutokana na hali hiyo akaenda hospitali. Kwa taarifa yako, hata polisi akishuhudia ajali isio na madhara makubwa huwa wanawashauri wahusika wamalizane wenyewe. Kwa sababu hiyo hamna kitu cha ajabu kwa polisi kutochukua hatua kama mhusika amesema kuwa anaweza kwenda mwenyewe nyumbani. Polisi hawapendi kazi ya kuandika maelezo na raia wengi hawapendi kwenda polisi.Yaani polisi walikuwepo na walishuhudia mtu akipigwa na hawakuchukua hatua! Uliwahi ona wapi polisi wa aina hiyo? Halafu upigwe Kisha upate nguvu za kwenda bar! Hebu scrutinize maelezo ya mleta hoja na uisome kwa utulivu kabla hujaihoji la sivyo utaiharibu.
Kama wanauhakika kwamba huyo mgonjwa ni DOUBLE AGENT je?.Na vipi kama ndio njia ya kumuonesha kwa vitendo kwamba wanajua kinachoendelea?Chadema hata hospital hawakukanyaga na ukichukulia kuwa huyo ni kiongozi wao mkubwa sana kitaifa kwenye chama chao
Kwa nini hawakwenda hospitali kumuona kiongozi wao?
Nakwambiaje, hujui maana ya trauma na concussion. Nani alimuinua alipoanguka ili atupe taarifa kamili la tukio Hilo?Nadhani hauelewi tu maana ya "trauma" na "concussion ". Kutokana na simulizi za Sigrida ni kuwa alipigwa ngumi akaangukia kichogo. Alipoanguka alipoteza fahamu kidogo lakini baada ya hapo akaondoka akaenda nyumbani. Na alianza kujisikia vibaya sana alipokuwa nyumbani kwake. Kutokana na hali hiyo akaenda hospitali. Kwa taarifa yako, hata polisi akishuhudia ajali isio na madhara makubwa huwa wanawashauri wahusika wamalizane wenyewe. Kwa sababu hiyo hamna kitu cha ajabu kwa polisi kutochukua hatua kama mhusika amesema kuwa anaweza kwenda mwenyewe nyumbani. Polisi hawapendi kazi ya kuandika maelezo na raia wengi hawapendi kwenda polisi.
Amandla...
Haujui maana ya trauma na concussion. Ungejua usingeuliza swali la nani alimuinua alipoanguka. Sio lazima mtu aliyepigwa kichwani ashindwe kuinuka. Anaweza kuinuka na kujisikia kuwa hajaumia sana. Hasa kama hatoki damu au haoni jeraha lolote.Nakwambiaje, hujui maana ya trauma na concussion. Nani alimuinua alipoanguka ili atupe taarifa kamili la tukio Hilo?
Yaani unaandika as if ulikuwepo. Upigane mbele ya polisi Tena wa bongo Kisha wakuachie tu.
Mbona huongelei ripoti ya daktari aliyemuhudumia? Acha kuzipa umuhimu taarifa za kusikia, utanishukuru baadae.
Kiwewe na mtikisiko wa ubongo aliupataje? Au konyagi zilimsababishia hayo? Usinikimbie kwa kisingizio Cha kupotezeana muda. Tukeshe humu!Haujui maana ya trauma na concussion. Ungejua usingeuliza swali la nani alimuinua alipoanguka. Sio lazima mtu aliyepigwa kichwani ashindwe kuinuka. Anaweza kuinuka na kujisikia kuwa hajaumia sana. Hasa kama hatoki damu au haoni jeraha lolote.
Hata hao mnaosema ni mashuhuda wanakiri walikuwa ndani kwa hiyo hawawezi kusema kama Sigrada alipigwa au hakupigwa. Sigrada hakupigana bali alipigwa na kwa sababu hiyo sio ajabu polisi kuamua kuwa hilo ni suala la kumalizana wenyewe kwa wenyewe.
Mtu yeyote atakayekuambia kuwa ana taarifa za daktari aliyemhudumia atakuwa ni muongo maana taarifa hiyo ni ya siri kati ya mhusika na daktari. Ukiitoa bila ridhaa ya mgonjwa unaweza kushitakiwa.
Nikushukuru kwa kitu gani? In fact, naona unanipotezea muda tu na sitakujibu tena.
Amandla...