Huu uliouandika ndiyo upumbavu wenyewe. Hujui chochote!!
Juzi usiku wanachama wa CHADEMA waliposikia Sigrada yupo hopitali ya Iringa wameenda mpaka hospitali ya Iringa, walimpigia aliyetoa hiyo taarifa, akawathibitishia kuwa mgonjwa yupo hospitali ya Iringa. Walipomwambia kuwa wapo kwenye gate la hospitali, alikata simu, na hakupokea simu yoyote. Watu wamekaa kwenye gate la hospitali mpaka saa 2 usiku, baadaye taarifa inatoka kuwa Sigrada yupo Dodoma. Hiyo ambulance ilipita wapi hata watu wasiione wakati gate la kutokea ni moja? Uchunguzi baadaye ulithibitisha kuwa wakati wanaambiwa Sigrada yupo hospitali ya Iringa, hakuwepo. CCM waliingia hospitali ya iringa na Sigrada na kumwambia daktari wa zamu aandike rufaa ya kwenda hospitali ya Benjamin Mkapa. Daktari alipowaambia kuwa hawezi kuandika rufaa bila ya kumpima mgonjwa, CCM wakaamua kuondoka na mgonjwa.
Kwa mazingira yaliyopo watu wa CHADEMA hawatakiwi kumwona Sigrada. Atakayelazimisha anaweza anaweza kuishia kubambikiziwa kesi.
Kama Sigrada anaumwa kweli au haumwi, kama anaumwa kwa kiwango kinachosemwa au sivyo, kilolicho muhimu ni kuwa yupo hospitali, na bila shaka anapata huduma nzuri. Mengine yatajulikana baadaye. Ila hofu ya wengi, CCM wasije wakamfanyia uovu, maana wameanza kutengeneza mazingira yanayotia shaka sana. Mtu aliyeendesha gari toka ukumbi wa kikao mpaka baa, wanasema alipigwa mpaka kuwa mahttuti.
Kumpiga mtu yeyote, iwe sana au kidogo, ni hatia, lakini exageration na kutumia mkasa wa mtu kwa dhamira chafu ni ushetani wa hali ya juu.
WanaCCM, kama mtu mmoja mmoja, wapo watu wema na wazuri, lakini CCM kama taasisi, ni chama shetani ambacho hakina huruma wala upendo kwa mtu yeyote mkosoaji wa CCM, serikali yake au viongozi wake.
CCM ndiyo inatajwa kuendesha ushetani wa utekaji na mauaji ya wakosoaji, halafu leo ikawe na upendo kwa kiongozi wa CHADEMA!! Ndiyo maana wengi wana hofu juu ya usalama wa Sigrada kwenye mikono hatari ya CCM.