SI KWELI CHADEMA yapiga marufuku ambao hawana elimu ya kidato cha sita na kuendelea kugombea serikali za mitaa na uchaguzi mkuu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Ndugu zangu Chadema hapa mmejiandalia sanda wenyewe. Hivi hamkufikiria kwamba mtapoteza wanachama wengi kwa kigezo hiki??
 
Tuanzie huku chini, wapewe vijana wenye elimu tupande tuone labda kutabadilika. Naunga mkono hoja ya Chadema.
Hoja haina mashiko kistratejia. Mnaenda kupoteza mapema sana...
 
Reactions: Tsh
Kwani hakuna wazee waliomaliza form six au wenye degree? Tatizo ukisikia form six unadhani ni Hawa wa sasa
Kama hii taarifa ni ya kweli nadhani ni uamuzi mbaya. Siyo kwamba sijui umuhimu wa elimu au elimu haina umuhimu kwenye uongozi wa sasa, ila uamuzi umekuwa wa ghafla mno na umetoka juu. I mean jambo kama hili inatakiwa ifanywe research kwanza, wapiga kura na wananchi kwa ujumla waulizwe maoni yao baada ya hapo ndiyo uamuzi ufanyike. Vinginevyo, kama huu uamuzi ni matokeo ya utafiti uliofanywa basi hakuna shida. NB: wanasiasa wetu wamezoea sana amri za kutoka juu kwenda chini na nyingi hufanyika bila wananchi kushirikishwa.
 
Shida watawapata kweli? Maana huku mtaani changamoto kwakweli vijana wengi wa Elimu hiyo hawajitoi sana kwenye mambo ya kijamii kwanini hata wasingeweka kidato Cha nne Kwa serikali za mitaa maana CCM bado tunaruhusu darasa la pili
 
Kuliko kuchukua mtu wa darasa la sababu kuwa mwenyekiti WA Kijiji au mtaa Karne ya 21, Bora wasiwe na viongozi uongozi.
Naunga hoja mkono 100%
Je walimu walio ishia form four na kwenda chuo cha ualimu nao hwana sifa. Nafikiri kunahitajika maelezo zaidi.
 
Hoja haina mashiko kistratejia. Mnaenda kupoteza mapema sana...
Tunaenda kupoteza nini? Wakati unajibu ukumbuke Mm ni mpiga kura si mwanasiasa na sio chawa hivyo sifungwi na upande wowote.
 
Fake hawa watu wanao tengeneza barua za chama fake inabidi wakamatwe.
 
Kwa maeneo ya mjini ni sawa ila huko vijijini Kazulamimba au Mahande wanaokubalika utakuta hata kuandika jina shida
Wewe unaiamini hiyo barua? Kwa akili ya kawaida tu, CHADEMA wanaweza kufanya hivyo?
FAKE! FAKE! FAKE! FAKE!
Na nina imani hiyo barua kaiandika Makala! Maanake akili zake huyooo……..

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Kuliko kuchukua mtu wa darasa la sababu kuwa mwenyekiti WA Kijiji au mtaa Karne ya 21, Bora wasiwe na viongozi uongozi.
Naunga hoja mkono 100%
Mimi CCM naungana na wewe

Serikalini sasa hivi hawaajiri darasa la saba hata kuendesha mkokoteni

Hayo mambo yaende hadi kwa wagombea ubunge,udiwani na serikali za mitaa viwango vipande jamani

Hivi karne hii kweli mtu anataka darasa la saba awe kiongozi wa mtaa ,kitongoji au kijiji au mbunge enzi hizi za shule za sekondari kila kata nchi nzima hapana

Darasa la saba waanze kuwa phased out viwango vya elimu vimepanda kwenye hata kata
 
Kwanza ni kinyume na Katiba na Kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…