SI KWELI CHADEMA yapiga marufuku ambao hawana elimu ya kidato cha sita na kuendelea kugombea serikali za mitaa na uchaguzi mkuu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wewe unaiamini hiyo barua? Kwa akili ya kawaida tu, CHADEMA wanaweza kufanya hivyo?
FAKE! FAKE! FAKE! FAKE!
Na nina imani hiyo barua kaiandika Makala! Maanake akili zake huyooo……..

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Kumbe una imani tu, weka counter evidence kuthibitisha ni feki
 
Elimu inakupa uwezo wa kupambanua mambo ,mwanasiasa mwenye elimu anakuwa bora.
 
Sharti la kujua kusoma na kuandika ni sharti ambalo ni 'minimum'. Kupata elimu zaidi ni bora kuliko kubaki na elimu ndogo, hasa katika mazingira ya ulimwengu wa sasa ambao ni rapidly revolving. Kama chama kikiweka sharti la wagombea wake kuwa na elimu kuanzia kidato cha SITA, sioni inakuwaje ni kuvunja Katiba, wakati Katiba haijaweka ukomo wa kupata elimu kwamba ni marufuku mtu kuwa na elimu zaidi ya kusoma na kuandika. Shida ni kwamba mbona sharti hili limekuja abruptly hivyo kama linatokea kwenye vyanzo sahihi vya chama? Nadhani linaweza kuwa tangazo "fake".
 
Hiyo itakuwa ni CHADEMA ya kuchongwa katika ofisi za Lumumba.
 
Kama wanavyofanya CCM kwenye Urais??
 
Kwa nafasi ya mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa mtaa na vijiji Mara nyingi sio rahisi umpate mwenye Elimu ya Six achilia mbali form four.

Hasa vijijini .

Hii taarifa itakuwa sio rasmi. Ebu tusubiri tuone.
Pamoja na shule zote hizi za kata upatikanaji wa form four kuongoza vijiji na mitaa bado ni changamoto??
 
Mkuu,

Katiba ikisema haki ya kupiga kura ni ya kila Mtanzania aliyefikisha miaka 18 na mwenye akili timamu, halafu Tume ya uchaguzi ikazidisha vigezo na kusema mpiga kura ni lazima awe kamaliza form six, hapo Tume ya Uchaguzi imevunja katiba au haijavunja katiba?
 
CHAWA mnahangaika sana na CHADEMA ambayo mlisema imekufa, sioni mkisema kuhusu ACT na CUF.
 
Yaani utokee ugomvi wa wana ndoa mtaani mtu aupeleke kwa kijana ambaye hata hajaoa, na muda wote kalewa visungura. Mwenyekiti wa mtaa ni mzee wa busara wa eneo hilo
UVCCM ndio wanataka hivyo.
 
Kwani Tume ndiyo iliyoweka hilo sharti? Mimi nimeongelea katika muktadha wa ilani ya chama kwa sababu kusema kiongozi awe na elimu ya kidato cha SITA hakujaondoa sharti la kujua kusoma na kuandika, na wala si kuwanyima Watanzania haki ya kupiga kura. After all, nilitoka maoni haya ni hypothetical sense, kwa sababu hili tangazo kinaonekana tu jamiiforums na sijaliona katika vyanzo vingine vya chama kama mtandao wa X na Facebook au kwenye taarifa ya habari, na pia kwa nini limekuja abruptly hivyo wakati Chadema wameshaanza chaguzi za ndani ya chama bila sharti hili jipya? Hivyo, inawezekana ni tangazo la kupika (fake news).
 
Ni hivi,

Kimantiki, levels za elimu Tanzania ziko hivi.

Kuanzia chini kwenda juu.

1. Kujua kusoma na kuandika. Kigezo hiki hakihitaji usome shule yoyote, ufaulu mtihani wowote, uwe na cheti chochote.

2. Darasa la saba. Kigezo hiki kinataka umalize shule ya msingi na uwe na cheti cha kumaliza darasa la saba.

3. Form Four. Ditto.

4. Form Six. Ditto.

5. Vyuo vya elimu ya juu kwa ngazi zake.Stashahada mpaka shahada zote mpaka shahada ya uzamivu


Kwa hiyo, ukisikia kigwzo cha kazi fulani ni kujua kusoma na kuandika, maana yake hapo hata cheti cha darasa la saba hakihitajiki.

Sasa, ikiwa katiba inamruhusu mtu anayejua kusoma na kuandika tu kugombea uenyekiti wa kijiji, nradi awe anajua kusoma na kuandika tu, CHADEMA ikiweka kigezo cha ziada cha kumaliza form six hapi haitawanyima wananchi haki yao ya kikatiba inayosema hawahitaji kumaliza form six, hawahitaji kumaliza form four, hawahitaji kunakiza darasa la saba, wanahitaji kujua kusoma na kuandika tu?

Sharti likiwa minimum maana yake mtu akitimiza sharti hilo tu anaruhusiwa. Mfano, minimum age of voting is 18 years. Maana yake mtu aliye na umri wa zaidi ya miaka 18 anaruhusiwa kupiga kura, lakini wa chini ya miaka 18 haruhusiwi.

Sasa ukisema sharti la kusoma na kuandika ni minimum, halafu ukaweka sharti lingine minimum la form six, hapo umeondoa minimum kutoka kujua kusoma na kuandika umeipandisha mpaka kuwa form six.

Huoni kwamba watu wanaojua kusoma na kuandika lakini hawajafija form six umewaengua katika kutafuta uongozi hapo? Na kama katiba ya nchi inawaruhusu kugombea uongozi, huoni kiwa hiki kigezo kinavunja katiba ya nchi?
 
Kiongozi, for the sake of mjadala (ingawa nahisi tangazo ni fake) soma Ibara ya 30(2)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, halafu urudi tujadili vizuri zaidi. Hii ibara ina'restrict' haki zote zilizotolewa kwenye Katiba. Si unajua the Bill of Rights kwenye Katiba yetu "is not entrenched?" Anyway, cheki kwanza, halafu uone je Tume ikisema hivyo, itakuwa imekosea/imevunja Katiba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…