CHADEMA Yapinga Uteuzi wa Jakaya Kikwete ndani ya AU, Yataka Mapitio ya Haraka

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Kikwete-profile-pic-small.jpg

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeiandikia Umoja wa Afrika (AU) kikitoa wito wa kufanyika kwa mapitio ya haraka kuhusu uteuzi wa Jakaya Kikwete kama Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja huo kwa Ukanda wa Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu.

Machi 25, 2026, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mahmoud Ali Youssouf, alimteua Rais Mstaafu Kikwete, kuwa Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Mwenyekiti wa AUC katika eneo la Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu.

Katika barua rasmi, CHADEMA imeeleza kuwa ingawa uteuzi huo uliwasilishwa kama hatua ya kuimarisha diplomasia na amani barani Afrika, unaibua maswali makubwa kuhusu uadilifu, kutokuwa na upendeleo na uaminifu wa Umoja wa Afrika katika kutekeleza majukumu yake.

Kupitia barua hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora wa chama hicho, John Kitoka, CHADEMA imeeleza kuwa historia ya kisiasa ya Kikwete inaibua wasiwasi, hasa kuhusu mchango wake katika mchakato wa katiba mpya nchini Tanzania.

Chama hicho kinadai kuwa Kikwete alihusika katika kusuasua kwa mchakato huo, jambo lililodhoofisha matarajio ya kidemokrasia ya wananchi. Aidha, kimemtuhumu kuunga mkono tawala za John Magufuli na Samia Suluhu Hassan ambazo zinadaiwa kubana uhuru wa kisiasa na haki za kiraia.

Hoja ya kutokuwa huru

CHADEMA pia imeeleza kuwa uhusiano wa karibu kati ya Kikwete na Rais Samia Suluhu Hassan unatia shaka uwezo wake wa kuwa mpatanishi huru katika ukanda wenye migogoro mikubwa.

Kwa mujibu wa chama hicho, Kikwete anaendelea kuwa mshauri wa karibu wa Rais Samia, hali ambayo inamfanya kushindwa kuwa na msimamo wa kati katika juhudi za kusuluhisha migogoro ya kikanda.

Barua hiyo inaonya kuwa uteuzi huo unaweza kudhoofisha juhudi za amani katika Ukanda wa Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu, eneo lenye umuhimu mkubwa wa kimkakati kutokana na biashara na changamoto za kisiasa.

CHADEMA inaeleza kuwa kumteua kiongozi mwenye historia yenye utata kunaweza kuongeza kutokuaminiana miongoni mwa wadau wa kikanda na kudhoofisha juhudi za Umoja wa Afrika katika kutatua migogoro.

Hoja ya uaminifu wa taasisi

Chama hicho pia kimehoji iwapo mchakato wa uteuzi ulizingatia uchunguzi wa kina (due diligence), kikisema kuwa maamuzi ya aina hiyo yanaweza kupunguza imani ya umma kwa Umoja wa Afrika kama msimamizi wa demokrasia na haki za binadamu barani.

CHADEMA imeutaka Umoja wa Afrika kufanya mapitio ya kina ya uteuzi huo na kuzingatia kuubatilisha, ikipendekeza kuteuliwa kwa mtu mwenye rekodi inayoakisi maadili ya demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu.

Tamko hilo linaongeza presha kwa Umoja wa Afrika kueleza misimamo yake kuhusu vigezo vinavyotumika katika uteuzi wa wawakilishi wake wa ngazi za juu, hasa katika maeneo yenye migogoro nyeti barani Afrika.
 
Attachments

  • Kikwete-profile-pic-small.jpg
    Kikwete-profile-pic-small.jpg
    20.4 KB · Views: 32
  • jakaya-Kikwete-tanzania.jpg.webp
    jakaya-Kikwete-tanzania.jpg.webp
    26.5 KB · Views: 28
View attachment 3565492

Kinara wa watenda maovu wa chama dola

Samia naye yatamfika, kuwajibika ICC The Hague.

MACKY SALL AKANWA NA NCHI ZA AFRIKA LICHA YA RAIS WA BURUNDI KUJARIBU KUMBEBA KWA MBELEKO

Ndayishimiye faces backlash as AU member states oppose unilateral nomination of Macky Sall for UN top job

On Mar 28, 2026 at 11:16 AM

A total of 20 African Union (AU) member states have broken silence over the actions of Burundian President Evariste Ndayishimiye, who is leading the AU in 2026. This followed Ndayishimiyes unilateral nomination of Macky Sall for the position of UN Secretary-General, which he attempted to push through with an unreasonably short 24-hour deadline for African leaders to approve it.
On March 27, 2026, media reports indicated that the AU had decided not to support Macky Sall’s candidacy due to procedural violations.

Amb. Nduhungirehe, Rwanda’s Minister of Foreign Affairs, has explained that the 20 AU member states who broke their silence were not rejecting any candidacy but rather opposing the flawed procedure initiated by President Ndayishimiye, which ignored AU rules governing international nominations.

“What happened today at the African Union is a stark reminder that leadership matters. It's unbelievable to note that a whole continental organisation can be tarnished or driven into a crisis by its own Chairperson, who is in office for not even two months,” Nduhungirehe posted on X .

The nomination process for the UN Secretary-General can be initiated by any country or group of countries, but the nominee need not necessarily be from the country that submits the candidacy.

On March 2, 2026, the Permanent Representative of Burundi to the UN notified the General Assembly that the Burundian government serving as current Chair of the African Union nominated Macky Sall, former President of Senegal, for the position.

“This submission of an African candidature to the position of UN Secretary General came as a surprise to all African Heads of State and Government, as none of them was consulted by the AU Chairperson before taking this important decision,” Nduhungirehe emphasized.

After the nomination, President Ndayishimiye attempted to pressure fellow African leaders into endorsing his decision by imposing a 24-hour “silence procedure.”

According to Amb. Nduhungirehe, Ndayishimiye convened the AU Bureau, where only two other members participated, and gave African governments 24 hours to approve or reject the nomination either by silence or by response.

“In other words, President Ndayishimiye, instead of calling an AU meeting for advice on the right procedure, chose to give his fellow AU Heads of State and Government only 24 hours to either endorse, by keeping silent, an AU decision that ‘EXPRESSES ITS FIRM SUPPORT to the President of the Republic of Burundi, H.E. Evariste Ndayishimiye, Chairperson of the AU for 2026, for having presented the candidacy of President Macky Sall […] for the position of Secretary-General of the United Nations,’ or to reject it by breaking the silence,” Amb. Nduhungirehe added.

This authoritarian approach was too much for many AU member states, which responded by breaking their silence and blocking the decision. They reminded Ndayishimiye that the AU must be governed by the rule of law.

Despite the damage to the AU's international reputation, Nduhungirehe hopes this incident will serve as a lesson for future appointments of AU Chairpersons.

The new UN Secretary-General will begin their term in January 2027. Any candidate must be nominated by a country or group of countries, and it is not a requirement for the candidate to come from the country making the nomination. This means that Burundi could have nominated Macky Sall on their own behalf, but the actions of Ndayishimiye caused a stir within the AU.

While it is not always followed strictly, UN leadership positions are generally rotated among different regions of the world, and there is growing support for the idea that it is time for a woman to lead the UN.

Other candidates who have submitted their nominations for the position include Michelle Bachelet, former President of Chile; Rafael Grossi, Director-General of the International Atomic Energy Agency; Rebeca Grynspan, former Vice President of Costa Rica; and Virginia Gamba from Argentina.

Since Ndayishimiye took over the AU chairmanship, analysts have criticized his leadership, questioning his ability to address the pressing challenges facing Africa, such as the ongoing war in the eastern part of the Democratic Republic of Congo, where Burundi is involved in the conflict.

dg.jpg
Since Ndayishimiye took over the AU chairmanship, analysts have criticized his leadership, questioning his ability to address the pressing challenges facing Africa.
 
Sababu za Macky Sall kukanwa

TOKA MAKTABA:
 
Ngoja Michele mie; eti hivi vinabo vinataka kushindana na Kikwete 🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Anyways, kwa yetote atakayebarikiwa kuja kuwa Raisi wa taifa hili, Kuna kubwa la kujifunza kuhusu siasa za nchi hii. Nalo ni KAMWE, narudia, KAAAMWE, usije ukafanya kosa la kuwaamini hawa wangese waitwao chadema.......kama nao mbali kabisa tena kwa uwe na sura ngumu nao ya kikauzu. Jifunzeni kwa Kikwete, hawa wangese aliwapendelea saaana, sana, saaaana lakini angalia malipo yao kwake! Ushenzi tu.

Ewe Raisi ujae, usiwe bwege, wakazie chadema kama JPM, kudadadeki!!!
 
Kipi wamekosea hapo??
Kikwete ana track record ya kusuluhisha, kuanzia hao Chadema wenyewe ambao waliruhusiwa kwenda Hadi ikulu mpaka nje ya Africa migogoro kibao yeye ndio amesuluhisha, Msumbiji, Congo, Burundi, South Sudan etc Kikwete amezuia Vita sababu ya Diplomasia yake.

Kumshuku Kikwete hawezi KAZI hio ya "preventive diplomacy" ni kama kumtuhumu Tanzania one wa hesabu hajui kusolve hesabu ya kujumlisha. He is like the only guy Nchi hii mwenye experience hio.
 
Maputo accord wasuluhishi walikuwa ni Mirko Manzoni, Neha Sanghrajka, Jonathan Powell

Wasuluhishi wakuu wa migogoro wa DRC kwa muda mrefu walikuwa ni Mkapa na Obasanjo lakini hata hivyo hakuna aliyeweza kusuluhisha huo migogoro mpaka Leo, Hawa wasuluhishi wa Africa huwa wanakuwa kama pain killers tu ila sio dawa kamili za kumaliza mizozo.

South Sudan haijawahi kuwa na amani, ni failed state kama Somalia tu, kama JK ndiye alikuwa msuluhishi basi hakuna chochote alichofanya.

Hata hivyo jukumu kubwa zaidi la usuluhishi alilowahi kupewa JK akiwa kama kiongozi wa jopo ni la usuluhishi wa migogoro wa Libya, unaweza kutupa mafanikio yake huko.
 
Kikwete ana track record ya kusuluhisha, kuanzia hao Chadema wenyewe ambao waliruhusiwa kwenda Hadi ikulu mpaka nje ya Africa migogoro kibao yeye ndio amesuluhisha, Msumbiji, Congo, Burundi, South Sudan etc Kikwete amezuia Vita sababu ya Diplomasia yake.

Kumshuku Kikwete hawezi KAZI hio ya "preventive diplomacy" ni kama kumtuhumu Tanzania one wa hesabu hajui kusolve hesabu ya kujumlisha. He is like the only guy Nchi hii mwenye experience hio.
Kikwete amewahi kuzuia vita nchi gani??
 
Maputo accord wasuluhishi walikuwa ni Mirko Manzoni, Neha Sanghrajka, Jonathan Powell

Wasuluhishi wakuu wa migogoro wa DRC kwa muda mrefu walikuwa ni Mkapa na Obasanjo lakini hata hivyo hakuna aliyeweza kusuluhisha huo migogoro mpaka Leo, Hawa wasuluhishi wa Africa huwa wanakuwa kama pain killers tu ila sio dawa kamili za kumaliza mizozo.

South Sudan haijawahi kuwa na amani, ni failed state kama Somalia tu, kama JK ndiye alikuwa msuluhisi basi hakuna chochote alichofanya.

Hata hivyo jukumu kubwa zaidi la usuluhisi alilowahi kupewa JK akiwa kama kiongozi wa jopo ni la usuluhishi wa migogoro wa Libya, unaweza kutupa mafanikio yake huko.
Who said ukiwa msuluhishi ni lazima iwe permanent? Kazi ya usuluhishi ni kutatua Hilo tatizo la mbeleni watu wasiuane, ukitokea ugomvi mwengine anaenda mwengine etc. ingekua measure ya usuluhishi ni kuzuia vita permanent basi wasuluhishi wote Duniani ni zero brain.
 
ujinga mtupu
Nchi zote za Afrika ziridhie halafu kichadema kinaota kutengua teuzi
 
Who said ukiwa msuluhishi ni lazima iwe permanent? Kazi ya usuluhishi ni kutatua Hilo tatizo la mbeleni watu wasiuane, ukitokea ugomvi mwengine anaenda mwengine etc. ingekua measure ya usuluhishi ni kuzuia vita permanent basi wasuluhishi wote Duniani ni zero brain.
Kuna kitu kinaitwa "lasting Peace", jifunze zaidi.
 
Back
Top Bottom