CHADEMA yashauri Katiba ifuatwe kuunda Serikali, Waziri Mkuu na Mawaziri waliopo hawakuapa mbele ya Rais wa sasa

CHADEMA yashauri Katiba ifuatwe kuunda Serikali, Waziri Mkuu na Mawaziri waliopo hawakuapa mbele ya Rais wa sasa

Mwanasheria wa serikali anazungumziaje hili mbona anashindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo au naye ni jipu linalosubiri kutumbuliwa?
 
inaonekana chadema wanadhani ktk kipindi hiki chini Mhe. Rais Samia wanaweza kupenyeza ajenda zao na zikafaulu sijui!!!!
ni ngumu sana, labda kwanza waanze kujenga mahusiano mazuri na ushirikiano wa dhati vinginevyo watasubiria sana.
hakuna litakalo wezekana bila utii kwa mamlaka na unyenyekevu, vuruvuruu ndio inawa cost kila siku.
ndio maaana Hayati JPM aliwapotezea maaana aliamini kuwa hawana nia njema na serikali yake.
chadema mkitaka kweli kuijenga nchi yetu basi onyesheni utii na ushirikiano wa kujenga nchi, acheni malumbano yasiyo na tija. sote ni watanzania tuijenge nchi yetu kwa kutanguliza uzalendo mbele.
hakuna mshindi ktk kuijenga nchi bali kuna adui asiye itakia mema nchi yetu.
nchi ni yetu sote tuijenge nchi yetu sote kwa pamoja.
Kwa nini wajinyenyekeze? Kwani kuna mtu mwenye hati miliki ya nchi hii? Kila mtu apewe uhuru wa kuchangia mustakabali wa nchi na siyo ajinyenyekeze kwa wananchi wenzake!

Uzalendo siyo kutii serikali iliyopo madarakani bali ni kuipenda nchi yako na kulinda kwa nguvu zote rasilimali zake. Rasilimali za nchi ni pamoja na wananchi wake!
 
Mbona unaficha hivyo vya juu? Au na ww umekaririshwa? Hayo masharti ni pale Rais kama kaenda nje ya nchi,anaumwa au kuna sababu nyingine ambazo zinapelekea kiti chake kulaliwa na mwingine kama VP kwa muda, hivyo atakayekalia icho kiti ndiye hawezi kufanya hayo, ila Huyu kashaapishwa ni Rais, halafu unasema hawezi badilisha waziri mkuu!, mnachekesha sana.
Huyu ni miongoni mwa cabinet hataki baraza livunjwe maana ana hofu na kibarua chake
 
Duh, mbona huu waraka ni pacha na ule wa TLS? Kwa hiyo mliwatanguliza TLS ili kutengeneza njia? Lakini walishajibiwa kwa hoja za kisheria wakaufyata, sasa nyie mnataka mjibiwe kisiasa?
Subiri, Mama ataunda lake hawezi kwenda na wale wakina Biteko
 
Kwa nini wajinyenyekeze? Kwani kuna mtu mwenye hati miliki ya nchi hii? Kila mtu apewe uhuru wa kuchangia mustakabali wa nchi na siyo ajinyenyekeze kwa wananchi wenzake!

Uzalendo siyo kutii serikali iliyopo madarakani bali ni kuipenda nchi yako na kulinda kwa nguvu zote rasilimali zake. Rasilimali za nchi ni pamoja na wananchi wake!
utii kwa mamlaka Ni AMRI ya MUNGU sio binaadamu, vitabu vya imani zote vina elekeza hivyo.
soma biblia au kuran.
 
Hili tukio la kufiwa na kiongozi mkuu (Rais) wa nchi ni jipya na geni kabisa na ukichanganya na namna au style lilivyotukia ndiyo inakuwa utata mtupu..

Inasemaekana kwa kuwa ni tukio ambalo katiba haijaliwekea utaratibu mahususi wa kulishughulikia, ilipelekea VP Samia Suluhu Hassani kubabaika kwa kiasi kikubwa...

Inasememekana aliogopa hata kutangaza kifo cha Rais. Hata alipopata ujasiri wa kutangaza akakosea kutangaza siku rasmi za maombolezo ya kitaifa kwa mujibu wa sheria. Badala ya 21 yeye akatangaza siku 14. Tunashukuru baada ya kupata utulivu alirekebisha...

Vivyo katika hili. Inawezekana bado ni ile hali ya kuweweseka tu inayowakabili...

Hili liko wazi sana. Ni lazima Rais mpya aunde serikali/baraza la mawaziri jipya litakalowajibika kwake moja kwa moja baada kula kiapo kwake. Hili lililopo limekufa pamoja na Rais wake...

Na kama Rais Samia Suluhu Hassani anataka kufanya kazi na kuwapenda hawahawa, basi atamke hivyo na kisha wafanye jambo moja tu muhimu, KULA KIAPO KIPYA KWA RAIS MPYA..

Na nchi hii inashangaza sana, maana ni kana kwamba haina Mwanasheria mkuu wa serikali ili kumshauri Rais vyema mambo yq kisheria na kikatiba...
Kwa nini baraza tu je wakuu wamikoa makatibu wakuu wakurugenzi na madc nao watoe kwakuwa hawakula kikao kwake
 
Mkuu CHADEMA wapo kikatiba?
katiba ya nchi gani mkuu?
ila vyama vyote viko kikatiba sio chadema tu, ila chadema imejijijengea taswira hasi kwa chama kinacho tawala sasa hapo chadema lazima ikubali maaana kujipima ubavu na ccm utapasuka mapafu bureee
 
utii kwa mamlaka Ni AMRI ya MUNGU sio binaadamu, vitabu vya imani zote vina elekeza hivyo.
soma biblia au kuran.
Tunajadili katiba ya nchi na siyo vitabu vya dini. Kuna maelfu ya Watanzania hawafuati hivyo vitabu.
 
Chadema naona wameishiwa pumzi kabisa.hakuna siasa za shortcut.wajiandae 2025yr.uwepo wa rais SSH usiwafanye waanze kujawana wenge,mama Samia hawezi kufanya negotiation na mapendekezo ambayo wanamlengo wa ulafi wa madaraka.kama wanataka madaraka tukutane 2025yr kwenye sanduku la kura,sio kuanza ngonjera zao zaajabu ajabu.Siasa haitaki short cut .
 
Back
Top Bottom