CHADEMA yashauri Katiba ifuatwe kuunda Serikali, Waziri Mkuu na Mawaziri waliopo hawakuapa mbele ya Rais wa sasa

Mwanasheria wa serikali anazungumziaje hili mbona anashindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo au naye ni jipu linalosubiri kutumbuliwa?
 
Kwa nini wajinyenyekeze? Kwani kuna mtu mwenye hati miliki ya nchi hii? Kila mtu apewe uhuru wa kuchangia mustakabali wa nchi na siyo ajinyenyekeze kwa wananchi wenzake!

Uzalendo siyo kutii serikali iliyopo madarakani bali ni kuipenda nchi yako na kulinda kwa nguvu zote rasilimali zake. Rasilimali za nchi ni pamoja na wananchi wake!
 
Huyu ni miongoni mwa cabinet hataki baraza livunjwe maana ana hofu na kibarua chake
 
Duh, mbona huu waraka ni pacha na ule wa TLS? Kwa hiyo mliwatanguliza TLS ili kutengeneza njia? Lakini walishajibiwa kwa hoja za kisheria wakaufyata, sasa nyie mnataka mjibiwe kisiasa?
Subiri, Mama ataunda lake hawezi kwenda na wale wakina Biteko
 
utii kwa mamlaka Ni AMRI ya MUNGU sio binaadamu, vitabu vya imani zote vina elekeza hivyo.
soma biblia au kuran.
 
Kwa nini baraza tu je wakuu wamikoa makatibu wakuu wakurugenzi na madc nao watoe kwakuwa hawakula kikao kwake
 
Mkuu CHADEMA wapo kikatiba?
katiba ya nchi gani mkuu?
ila vyama vyote viko kikatiba sio chadema tu, ila chadema imejijijengea taswira hasi kwa chama kinacho tawala sasa hapo chadema lazima ikubali maaana kujipima ubavu na ccm utapasuka mapafu bureee
 
utii kwa mamlaka Ni AMRI ya MUNGU sio binaadamu, vitabu vya imani zote vina elekeza hivyo.
soma biblia au kuran.
Tunajadili katiba ya nchi na siyo vitabu vya dini. Kuna maelfu ya Watanzania hawafuati hivyo vitabu.
 
Chadema ni chama cha wachaga.

Siku hizi wameanzisha vita na kanda ya ziwa.

Sisi tunawasubiri 2025 wakati wa kuja kuomba kura. Pengine kura za Kanda ya Ziwa hawazihitaji watajikita kanda zingine
 
Chadema naona wameishiwa pumzi kabisa.hakuna siasa za shortcut.wajiandae 2025yr.uwepo wa rais SSH usiwafanye waanze kujawana wenge,mama Samia hawezi kufanya negotiation na mapendekezo ambayo wanamlengo wa ulafi wa madaraka.kama wanataka madaraka tukutane 2025yr kwenye sanduku la kura,sio kuanza ngonjera zao zaajabu ajabu.Siasa haitaki short cut .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…