CHADEMA yashauri Katiba ifuatwe kuunda Serikali, Waziri Mkuu na Mawaziri waliopo hawakuapa mbele ya Rais wa sasa

Kweli Saccos ya Chadema imeishiwa ajenda kabisa! Kwenye taarifa yao ni utopolo tupu. Tulishajadiri humu na kuonyesha jinsi gani Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri linakoma au kuvunjwa. Rais akifariki na Makamo wake kuchukua usukari Baraza la Mawaziri halivunjiki automatically.

Chadema someni kwenye Katiba jinsi Waziri Mkuu anavyokoma kuwa Waziri Mkuu siyo utopolo mlioandika kwenye taarifa yenu uchwara au mkiona inafaa kimbilieni Mahakamani ili mkafundishwe jinsi ya kutafasiri vifungu vya Katiba.
 
Bahati nzuri magumu siyo kwa CHADEMA pekee, sukari imepanda kwa wote, vifaa vya ujenzi, mafuta ya kula, uneployment kwa wote, kimsingi wewe baki na ujinga wako
 
Wenzako huku akina Heri James wameanza kutubu dhambi zao hadharani. Chupi zimeanza kuwabana...
 
Waonaje hoja za CDM zina uzito kwa mujibu katiba au la? Achana na porojo weka maoni ya kitaalamu.
 
Chadema ni chama cha wachaga.
Siku hizi wameanzisha vita na kanda ya ziwa.
Tuache UONGO jamani huyu Mnyika John John ni Msukuma aliyemuita Jakaya ni dhaifu leo kawa Mchagga?
Mnyika anapokosea anadhani Makamu wa Rais hakuwepo wakati Mawaziri wote na makatibu walipoapishwa,
Rais hakuweza kuwaapisha hao Mawaziri bila ya makamu wa Rais, Katibu Kiongozi, Jaji mkuu walikuwepo.
Tusilazimishe kusema uongo wakati hatuainishi vipengele vya Katiba vinavyosema km Rais hayupo kwa Kifo, basi Makamu au jaji au spika akiingia avunje Baraza kabla ya Uchaguzi mwingine
 
Samia ni CCM lkn serikali hii siyo ya Magufuli tena ni serikali ya Samia.
 
Zanzibar sasa wamepata nafasi... Ngoja ajaze ijumaa tu.. Siunajua walivyo wadini
Upimwe akili wewe, Mambo ya udini ya Nini sasa. Wewe na jamapili unataka usaidiwe Nini. Acha kuropoka tuliza mnyeo wako
 
Hayo Ni mawazo ya chama kikuu Cha upinzani nchi hii cyo ya baba yako kuona mawazo ya wengine hayafai.
Chama kikuu cha upinzani cha nchi gani!!!!! Chadema yenye mbunge mmoja. Zitto an azidi kukubalika jana kalamba jimbo jingine kwa njia ya kidemokrasia. Chadema mnatia aibu.Jiwe mtamkumbuka kwa kuwafundisha demokrasia
 
Naomba kufahamu. Naelewa ni kweli mawaziri hawajaapa kwa rais wa awamu ya sita. Ila, mbona raisi hakupigiwa kura? Nikiitazama katiba ndio ilivyoelekeza endapo raisi aliye madarakani amefariki.
 
Waliapa kwa Rais au kwa magufuli?
Kama ni kuapa kwa rais kama taasisi, kulikuwa haja gani kwa mawaziri walioapa wakati wa JMK, kuapa tena wakati wa JPM ambapo waliteuliwa na JPM kuongoza wizara zilizile? Kiapo kwa maoni yangu kinaonesha utii kwa rais aliyepo madarakani pamoja na taasisi yake ya urais anayoiongoza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…