CHADEMA yashauri Katiba ifuatwe kuunda Serikali, Waziri Mkuu na Mawaziri waliopo hawakuapa mbele ya Rais wa sasa

CHADEMA yashauri Katiba ifuatwe kuunda Serikali, Waziri Mkuu na Mawaziri waliopo hawakuapa mbele ya Rais wa sasa

Kweli Saccos ya Chadema imeishiwa ajenda kabisa! Kwenye taarifa yao ni utopolo tupu. Tulishajadiri humu na kuonyesha jinsi gani Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri linakoma au kuvunjwa. Rais akifariki na Makamo wake kuchukua usukari Baraza la Mawaziri halivunjiki automatically.

Chadema someni kwenye Katiba jinsi Waziri Mkuu anavyokoma kuwa Waziri Mkuu siyo utopolo mlioandika kwenye taarifa yenu uchwara au mkiona inafaa kimbilieni Mahakamani ili mkafundishwe jinsi ya kutafasiri vifungu vya Katiba.
 
Unacoment kama vile chadema mko madarakani!

Hii ni ccm, Magufuli alikuwa ccm na Samia ni ccm, hiyo mitazamo mnayojaribu kuitengeneza sijui inawafaidishaje, ila ninachojua ccm ni ile ile chini ya mfumo uleule kama unabisha subiri 2025 uone utakavyogongwa
Bahati nzuri magumu siyo kwa CHADEMA pekee, sukari imepanda kwa wote, vifaa vya ujenzi, mafuta ya kula, uneployment kwa wote, kimsingi wewe baki na ujinga wako
 
Mna imaginations za ajabu kweli.

Nahisi nyinyi ndo huwa mnateseka.

Mimi niteseke kwa lipi?

Sijawahi kuwa mtumishi wa Magufuli.

Kibinafsi, simjui na hakunijua.

Sijawahi kuwa mtumishi wa serikali na kamwe sitokuja kuwa.

Najitegemea mwenyewe.

Sijawahi kupata handout yoyote ile toka kwa serikali yoyote ile.

Sijanufaika na chochote kile kutokana na urais wa Magu

Maisha yangu hayajabadilika kwa lolote lile.

Sasa cha kunitesa ni kipi? Waweza kunitajia?

Yaani kabisa umekaa hapo ulipo na kujiaminisha kwamba Ngabu anateseka?

Magufuli nimemkosoa sana humu JF. Unabisha?

Wewe uliteseka wakati Magufuli akiwa Rais?
Wenzako huku akina Heri James wameanza kutubu dhambi zao hadharani. Chupi zimeanza kuwabana...
 
inaonekana chadema wanadhani ktk kipindi hiki chini Mhe. Rais Samia wanaweza kupenyeza ajenda zao na zikafaulu sijui!!!!
ni ngumu sana, labda kwanza waanze kujenga mahusiano mazuri na ushirikiano wa dhati vinginevyo watasubiria sana.
hakuna litakalo wezekana bila utii kwa mamlaka na unyenyekevu, vuruvuruu ndio inawa cost kila siku.
ndio maaana Hayati JPM aliwapotezea maaana aliamini kuwa hawana nia njema na serikali yake.
chadema mkitaka kweli kuijenga nchi yetu basi onyesheni utii na ushirikiano wa kujenga nchi, acheni malumbano yasiyo na tija. sote ni watanzania tuijenge nchi yetu kwa kutanguliza uzalendo mbele.
hakuna mshindi ktk kuijenga nchi bali kuna adui asiye itakia mema nchi yetu.
nchi ni yetu sote tuijenge nchi yetu sote kwa pamoja.
Waonaje hoja za CDM zina uzito kwa mujibu katiba au la? Achana na porojo weka maoni ya kitaalamu.
 
Chadema ni chama cha wachaga.
Siku hizi wameanzisha vita na kanda ya ziwa.
Tuache UONGO jamani huyu Mnyika John John ni Msukuma aliyemuita Jakaya ni dhaifu leo kawa Mchagga?
Mnyika anapokosea anadhani Makamu wa Rais hakuwepo wakati Mawaziri wote na makatibu walipoapishwa,
Rais hakuweza kuwaapisha hao Mawaziri bila ya makamu wa Rais, Katibu Kiongozi, Jaji mkuu walikuwepo.
Tusilazimishe kusema uongo wakati hatuainishi vipengele vya Katiba vinavyosema km Rais hayupo kwa Kifo, basi Makamu au jaji au spika akiingia avunje Baraza kabla ya Uchaguzi mwingine
 
Unacoment kama vile chadema mko madarakani!

Hii ni ccm, Magufuli alikuwa ccm na Samia ni ccm, hiyo mitazamo mnayojaribu kuitengeneza sijui inawafaidishaje, ila ninachojua ccm ni ile ile chini ya mfumo uleule kama unabisha subiri 2025 uone utakavyogongwa
Samia ni CCM lkn serikali hii siyo ya Magufuli tena ni serikali ya Samia.
 
Hayo Ni mawazo ya chama kikuu Cha upinzani nchi hii cyo ya baba yako kuona mawazo ya wengine hayafai.
Chama kikuu cha upinzani cha nchi gani!!!!! Chadema yenye mbunge mmoja. Zitto an azidi kukubalika jana kalamba jimbo jingine kwa njia ya kidemokrasia. Chadema mnatia aibu.Jiwe mtamkumbuka kwa kuwafundisha demokrasia
 
Naomba kufahamu. Naelewa ni kweli mawaziri hawajaapa kwa rais wa awamu ya sita. Ila, mbona raisi hakupigiwa kura? Nikiitazama katiba ndio ilivyoelekeza endapo raisi aliye madarakani amefariki.
 
Waliapa kwa Rais au kwa magufuli?
Kama ni kuapa kwa rais kama taasisi, kulikuwa haja gani kwa mawaziri walioapa wakati wa JMK, kuapa tena wakati wa JPM ambapo waliteuliwa na JPM kuongoza wizara zilizile? Kiapo kwa maoni yangu kinaonesha utii kwa rais aliyepo madarakani pamoja na taasisi yake ya urais anayoiongoza.
 
Back
Top Bottom