Sikubaliani na uamuzi wa kutokwenda mahakamani. Katika mabandiko yangu ya nyuma nilieleza suala hili kwa urefu sana na kuonyesha kuwa Mahakama ya Rufaa ilikwisha tamka kuwa kitendo chochote kile cha Tume ambacho kimefanywa kinyume cha sheria kinapingwa. Nilijitahidi kuwasilisha maoni yangu kwa mwanasheria wao lakini inaelekea wamekataa. Inasikitisha.
Bado ninasisitiza kuwa Mahakama Kuu inabanwa na uamuzi ule wa Mahakama ya Rufaa na hapo ndio ungekuwa uwanja mzuri wa Chadema kuanika ushahidi hadharani. Lakini Wanasheria hutofautiana mbinu za kupambana.
Mtikila alishinda Kesi kutaka serikali ifuate katiba ya nchi na kuruhusu Mgombea binafsi. Serikali ya CCM imekula jiwe na kujikausha kama vile haipo. Kifupi imeingiza ubabe na kuvalia miwani ya mbao katiba ya nchi.
Huu si kwamba ni uchuro tu ,hapana . Ni hatari kwa CCM yenyewe na nchi kwa ujumla.
Serikali ikikiuka Hukumu ya Mahakama maana yake inahalalisha Uhalifu kila mahali nchini Tanzania.
Tunahitaji kusema zaidi?
Fahamu kwamba wana mageuzi tunapambana na Jidude lisilofuata taratibu wala sheria. Jidude hili linajiendeshea mambo yake kwa taratibu ambazo hata lenyewe halijaziridhia.
Kimsingi Chadema kwenda mahakamani ni upuuzi, ni kupoteza muda na ni kurudi nyuma hatua zaidi ya elfu.
Kesi hii imefunguliwa mbele ya Wananchi.
Wao wananchi ndiyo Majudge watasikiliza malalamiko ya upinzania,watapitia vielelezo na ushahidi wote, wataenda chemba na kunong'ona kisha watatoa Hukumu ya HAKI.
Sidhani ushauri wa kwenda Mahakamani una nafasi hapa.
Nchi zote Duniani zenye misukosuko isababishwayo na Vyama Dola kama CCM malalamiko na kesi zote huwekwa mbele ya wananchi ili watoa uamuzi wao. Ni wananchi pekee ndiyo wenye uwezo wa kutoa hukumu ya Haki.
CCM ni chama cha Siasa chenye wafuasi waliosehemu ya watu wa tanzania,CCM siyo wananchi wote wa Tanzania na CCM siyo serikali ya Tanzania.
Wananchi watatoa Hukumu baada ya kupitia Ushahidi wote.
Pengine wengi hapa Jamvini wanaweza dhani maneno matupu hayavunji mfupa, mkono mtupu haulambwi nk Lakini pia wanasahau kwamba kuna msemo usemao Shughuli yeyote ile ni watu.
Ukiacha methali nyingi na misemo ya kiswahili ambayo mingine huleta maswali mengi kuliko majibu, kuna misemo mingi ya kisayansi itokanayo na uchunguzi wa muda mrefu inayothibisha kwamba Maneno na kitendo cha kuvunja mfupa ni kitu kimoja.
Kuna ukweli ulifanyiwa uchunguzi wa Kisayansi kwamba kuna Uhusiano Wa Moja kwa Moja kati ya Wazo na Kitu Halisi.
Vitu vyote ikiwa ni pamoja na vile tudhanivyo ni vitu asilia kama hewa maji na ardhi viliwahi kuwa wazo.
Hakuna kitu kianzacho tu bila kutungwa mimba ya wazo.
Wazo ndiyo asili,
wazo ndiyo chanzo,
wazo ndiyo mbegu na msingi wa kila kitu.
Hakuna kilichoko leo hapa ulimwenguni ambacho kwanza hakikuwa wazo.
Kwa hiyo ni ukweli usiopingika kwamba vingi visivyo kuwepo sasa,vitakavyokuwako baadaye sasa hivi ni mawazo tu.
Mtu yeyote mwenye hekima iliyopevuka kamwe hadharau wazo hata liwe la kiendawazimu kiasi gani kwa sababu anajua ukuu wa nguvu ya wazo.
Ndiyo maana Serikali zote Duniani hutumia mabilioni mengi sana sana na wakati wake mwingi kujaza mawazo ya aina fulani ndani ya vichwa vya watu wake ili hatimaye vitu fulani vipatikane kutoka kwa wananchi wake.Serikali zote zinafanya hivyo kwa sababu zinajua wazi kabisa kwamba hakuna tofauti kati ya wazo na kitu.
Upandapo mbegu ya wazomavuno ni kitu halisi.
Kwa mfano,Hakuna tofauti kati ya wazo la kumiliki gari na Gari lako lililopaki nje ya nyumba yako.Kuna Time Delay kati ya Wazo la kuwa na Gari na Gari unalolimiliki lililopaki mbele ya nyumba yako.
Wazo la gari---> Time Delay ---> Gari.
Mtu akitaka Usinunue gari pengine hadi kufa kwako anacheza na Time tu, kwa sababu anajua wazi hakuna namna ya kukuzuia kuendelea kuwaza juu ya gari.
Sasa utajiuliza time inazewa vipi?
Time na Space vimeshikamana na kuchangamana. ukitikisa Space time nayo inatikisika, ukiikunja space time nayo inakunjika, ukirefusha space time nayo inarefuka.Ukiondoa Space yote ukabakiwa na utupu pekee Time nayo inatoweka jumla au tuseme inakuwa infinite kwa maana kwamba sekunde moja inakuwa sawa na miaka billion kadhaa.
Hakuna awezaye kufupisha wala kurefusha Muda.Lakini inawezekana kucheza na Space kwa sana hivyo indirect kucheza na time.
Watu tukiwa kwenye raha na furaha relativelyTime inakatika kwa sana na akili zetu zinajaa mawazo Positive kibao.
Watu tukiwa katika majonzi Time inaslow Down na wengi tunakata tamaa na kuuwa mawazo yetu mengi mazuri, tunabakiza mawazo yale tudhaniyo ni ya msingi. Kula kuvaa na mahali pa kurara tu.
Kimsingi Inawezekana kurefusha muda kati ya Wazo la gari na gari unalolimiliki.
Kwa sababu space ni yote tuyafanyayo kila siku,ni yote tuonayo, ni yote tuwezayo kushika , ni yote tutambuayo kwa akili zetu, ni rahisi sana kwa Serikali dharimu kutengeneza aina fulani ya utaratibu na kuujaza vichwani mwa watu kwa namna moja au nyingine ili watu waendelee ku mark time wenyewe bila kuguswa na mtu na kuamini kabisa kwamba uwezo nia na hamu yao imefikia ukomo.
Watu wanakuwa matajiri wakubwa kwa kutumia mbinu hii.
Serikali zinaweza kuwcontrol watu wake kwa kutumia mbinu hii hii.
Wazo ni hatua muhimu, hatua nyingine muhimu ni, tamko. Tamko ni hatua ya kuliweka wazo katika maandishi au usemi. Tamko ni sawa kabisa na kuvuna wazo kutoka vichwani mwa watu kadhaa na kulipanda katika vichwa vya watu wengi katika safari ya wazo kuwa kitu.
Watu wengi hudhani tamko ni hatua ya kwanza la hasha,Tamko ni hatu ya pili hatua ya kwanza ni wazo.
watu walioko kwenye majonzi time kwao iko streached kwa maana hiyo wakipewa wao sahihi wanamuda mrefu sana wakutafakari.
Watu wlaio katika majonzi wakiachwa bila wazo la maana wanatumia muda wao mwingi kukata tamaa na kujilaumu bila kisa.
Wakati huohuo watu walioko katika furaha hawana muda wa kutafakari kwani kwao muda ni mfupi unakatika upesi,muda kwao ni mali na mambo ya kufanya mazuri na yenye kufurahisha moyo ni mengi.
Hawana muda wa kulitafakari wazo na kutambua matokeo yake.umuhimu mkubwa kwao ni juu ya vile vilivyopo mbele yao tu.
Kuna kitu Wazungu wanaita Manifestation.
Tangu wakati wazo linapandwa ndani ya vichwa vya watu wengi mpaka kitu halisi kuzaliwa kuna kitu wenzetu wanaita Manifestation. Katika ubinafsi wa kila mtu kuna wakati utambuzi na ufahamu hukaa pamoja na kuzaa msukumo wa kutenda. Hali hiyo ikifikiwa hakuna kurudi nyuma tena, wazo ni lazima liwe kitu kwa sababu time =0.
Hapo ndipo waswahili walikuja na methali isemayo kimya kingi kina mshindo. Kimya halafu Mshindo??
Hatuna ubavu wa kubeza wazo yakinifu kwa sababu ukuu wa hekima zetu hauruhusu hata kidogo.