The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,092
Tume ya uchaguzi pia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee Mwanakijiji, asante kwa hili, mimi ni mmoja sio wawashabiki wako bali waumini wako sio kwa sababu ya unachoandika, but kwa underlying reasons behind inayokupelekea kuandika unachoandika lakini kwenye hili, naomba kutofautiana na wewe kwenye logic zaidi tukiachana na kufuata tuu imani ya unachoamini japo nakuunga mkono kwenye mengine yote isipokuwa hili, sikuliunga mkono since day one, na sitaliunga mkono mpaka siku ya mwisho, unless otherwise.Hivyo, tume inaendelea kutangaza matokeo bila ya kujali malalamiko au matatio yaliyotokea kwa sababu wanajua hicho kipengele cha Katiba kuwa wakifika mwisho na kumtangaza mshindi then ITS OVER. Na hicho ndicho kinatokea.
Sasa CHADEMA tunaambiwa wanatakiwa wakubali sasa kuwa kwa vile "mshindi" keshatangazwa waende kukumbatiana naye na kupiga picha za pongezi. Tunaambiwa kuwa kwa vile sasa keshaapishwa na Katiba inasema huwezi kuhoji mahali popote basi Chadema wakubali kutuma pongezi za "ushindi" wakati dhamira zao zinawakatalia.
Sasa CHADEMA wafanye nini? Tunaambiwa lazima wakubali tu yaishe. Wakubali kwa sababu wameridhika na matokeo au kwa sababu kutangazwa kumekidhi the minimum requirement ya katiba?
CHADEMA SASA NDIO wamesema kuwa wanatambua ushindi wa wabunge wao kwa sababu ni rahisi kuutubitisha lakini wanashindwa kukubali ushindi wa Rais kwa sababu well.. u guessed it..
Hatuna ubavu wa kubeza wazo yakinifu kwa sababu ukuu wa hekima zetu hauruhusu hata kidogo.[/QUOTE]Mtikila alishinda Kesi kutaka serikali ifuate katiba ya nchi na kuruhusu Mgombea binafsi. Serikali ya CCM imekula jiwe na kujikausha kama vile haipo. Kifupi imeingiza ubabe na kuvalia miwani ya mbao katiba ya nchi.
Huu si kwamba ni uchuro tu ,hapana . Ni hatari kwa CCM yenyewe na nchi kwa ujumla.
Serikali ikikiuka Hukumu ya Mahakama maana yake inahalalisha Uhalifu kila mahali nchini Tanzania.
Tunahitaji kusema zaidi?
Fahamu kwamba wana mageuzi tunapambana na Jidude lisilofuata taratibu wala sheria. Jidude hili linajiendeshea mambo yake kwa taratibu ambazo hata lenyewe halijaziridhia.
Kimsingi Chadema kwenda mahakamani ni upuuzi, ni kupoteza muda na ni kurudi nyuma hatua zaidi ya elfu.
Kesi hii imefunguliwa mbele ya Wananchi.
Wao wananchi ndiyo Majudge watasikiliza malalamiko ya upinzania,watapitia vielelezo na ushahidi wote, wataenda chemba na kunong'ona kisha watatoa Hukumu ya HAKI.
Sidhani ushauri wa kwenda Mahakamani una nafasi hapa.
Nchi zote Duniani zenye misukosuko isababishwayo na Vyama Dola kama CCM malalamiko na kesi zote huwekwa mbele ya wananchi ili watoa uamuzi wao. Ni wananchi pekee ndiyo wenye uwezo wa kutoa hukumu ya Haki.
CCM ni chama cha Siasa chenye wafuasi waliosehemu ya watu wa tanzania,CCM siyo wananchi wote wa Tanzania na CCM siyo serikali ya Tanzania.
Wananchi watatoa Hukumu baada ya kupitia Ushahidi wote.
Pengine wengi hapa Jamvini wanaweza dhani maneno matupu hayavunji mfupa, mkono mtupu haulambwi nk Lakini pia wanasahau kwamba kuna msemo usemao Shughuli yeyote ile ni watu.
Ukiacha methali nyingi na misemo ya kiswahili ambayo mingine huleta maswali mengi kuliko majibu, kuna misemo mingi ya kisayansi itokanayo na uchunguzi wa muda mrefu inayothibisha kwamba Maneno na kitendo cha kuvunja mfupa ni kitu kimoja.
Kuna ukweli ulifanyiwa uchunguzi wa Kisayansi kwamba kuna Uhusiano Wa Moja kwa Moja kati ya Wazo na Kitu Halisi.
Vitu vyote ikiwa ni pamoja na vile tudhanivyo ni vitu asilia kama hewa maji na ardhi viliwahi kuwa wazo.
Hakuna kitu kianzacho tu bila kutungwa mimba ya wazo.
Wazo ndiyo asili,
wazo ndiyo chanzo,
wazo ndiyo mbegu na msingi wa kila kitu.
Hakuna kilichoko leo hapa ulimwenguni ambacho kwanza hakikuwa wazo.
Kwa hiyo ni ukweli usiopingika kwamba vingi visivyo kuwepo sasa,vitakavyokuwako baadaye sasa hivi ni mawazo tu.
Mtu yeyote mwenye hekima iliyopevuka kamwe hadharau wazo hata liwe la kiendawazimu kiasi gani kwa sababu anajua ukuu wa nguvu ya wazo.
Ndiyo maana Serikali zote Duniani hutumia mabilioni mengi sana sana na wakati wake mwingi kujaza mawazo ya aina fulani ndani ya vichwa vya watu wake ili hatimaye vitu fulani vipatikane kutoka kwa wananchi wake.Serikali zote zinafanya hivyo kwa sababu zinajua wazi kabisa kwamba hakuna tofauti kati ya wazo na kitu.
Upandapo mbegu ya wazomavuno ni kitu halisi.
Kwa mfano,Hakuna tofauti kati ya wazo la kumiliki gari na Gari lako lililopaki nje ya nyumba yako.Kuna Time Delay kati ya Wazo la kuwa na Gari na Gari unalolimiliki lililopaki mbele ya nyumba yako.
Wazo la gari---> Time Delay ---> Gari.
Mtu akitaka Usinunue gari pengine hadi kufa kwako anacheza na Time tu, kwa sababu anajua wazi hakuna namna ya kukuzuia kuendelea kuwaza juu ya gari.
Sasa utajiuliza time inazewa vipi?
Time na Space vimeshikamana na kuchangamana. ukitikisa Space time nayo inatikisika, ukiikunja space time nayo inakunjika, ukirefusha space time nayo inarefuka.Ukiondoa Space yote ukabakiwa na utupu pekee Time nayo inatoweka jumla au tuseme inakuwa infinite kwa maana kwamba sekunde moja inakuwa sawa na miaka billion kadhaa.
Hakuna awezaye kufupisha wala kurefusha Muda.Lakini inawezekana kucheza na Space kwa sana hivyo indirect kucheza na time.
Watu tukiwa kwenye raha na furaha relativelyTime inakatika kwa sana na akili zetu zinajaa mawazo Positive kibao.
Watu tukiwa katika majonzi Time inaslow Down na wengi tunakata tamaa na kuuwa mawazo yetu mengi mazuri, tunabakiza mawazo yale tudhaniyo ni ya msingi. Kula kuvaa na mahali pa kurara tu.
Kimsingi Inawezekana kurefusha muda kati ya Wazo la gari na gari unalolimiliki.
Kwa sababu space ni yote tuyafanyayo kila siku,ni yote tuonayo, ni yote tuwezayo kushika , ni yote tutambuayo kwa akili zetu, ni rahisi sana kwa Serikali dharimu kutengeneza aina fulani ya utaratibu na kuujaza vichwani mwa watu kwa namna moja au nyingine ili watu waendelee ku mark time wenyewe bila kuguswa na mtu na kuamini kabisa kwamba uwezo nia na hamu yao imefikia ukomo.
Watu wanakuwa matajiri wakubwa kwa kutumia mbinu hii.
Serikali zinaweza kuwcontrol watu wake kwa kutumia mbinu hii hii.
Wazo ni hatua muhimu, hatua nyingine muhimu ni, tamko. Tamko ni hatua ya kuliweka wazo katika maandishi au usemi. Tamko ni sawa kabisa na kuvuna wazo kutoka vichwani mwa watu kadhaa na kulipanda katika vichwa vya watu wengi katika safari ya wazo kuwa kitu.
Watu wengi hudhani tamko ni hatua ya kwanza la hasha,Tamko ni hatu ya pili hatua ya kwanza ni wazo.
watu walioko kwenye majonzi time kwao iko streached kwa maana hiyo wakipewa wao sahihi wanamuda mrefu sana wakutafakari.
Watu wlaio katika majonzi wakiachwa bila wazo la maana wanatumia muda wao mwingi kukata tamaa na kujilaumu bila kisa.
Wakati huohuo watu walioko katika furaha hawana muda wa kutafakari kwani kwao muda ni mfupi unakatika upesi,muda kwao ni mali na mambo ya kufanya mazuri na yenye kufurahisha moyo ni mengi.
Hawana muda wa kulitafakari wazo na kutambua matokeo yake.umuhimu mkubwa kwao ni juu ya vile vilivyopo mbele yao tu.
Kuna kitu Wazungu wanaita Manifestation.
Tangu wakati wazo linapandwa ndani ya vichwa vya watu wengi mpaka kitu halisi kuzaliwa kuna kitu wenzetu wanaita Manifestation. Katika ubinafsi wa kila mtu kuna wakati utambuzi na ufahamu hukaa pamoja na kuzaa msukumo wa kutenda. Hali hiyo ikifikiwa hakuna kurudi nyuma tena, wazo ni lazima liwe kitu kwa sababu time =0.
Hapo ndipo waswahili walikuja na methali isemayo kimya kingi kina mshindo. Kimya halafu Mshindo??
Hatuna ubavu wa kubeza wazo yakinifu kwa sababu ukuu wa hekima zetu hauruhusu hata kidogo.
Dr. Slaa alishasema msimamo wake tangu mwanzo, kama uchaguzi ni huru na wa haki, atayatambua matokeo na atamtambua mshindi, kama uchaguzi sio huru na wa haki, hatamtambua mshindi na hata yakubali matokeo, hiki ndicho wale waliompa kura zao Dr. Slaa, tulitaka tumsikie akikisema pale pale inside the ring baada tuu ya kuisha kwa pambano, not otherwise, not other time, not other place, it was suppossed to be there and then!.
Mbona hilo liko wazi Kiranga usichanganye watu rais ni sehemu ya bunge means president is a subset of bunge as universal bunge lina uwezo wa kumuondoa rais bungeni.
Kwa yule ambaye si Mwanasheria anaweza kubabaika na kuamini kuwa ni kweli kabisa kuwa Katiba inazuia lakini Wanasheria tuna kanuni za kutofautisha maamuzi na kuvuka kile ambacho kinaonekana kuwa ni kipingamizi au kizuizi kwa lugha ya kawaida kabisa. Uwezo na mbinu hizi ndizo zilimfanya Shakespeare aandike kuwa Mfalme Henry alipotaka kutunga sheria ambayo itaondoa kila aina ya upinzani kwa utawala wake alisema kuwa jambo la kwanza la kufanya ni kuua wanasheria wote "The first thing we do, we kill all lawyers". Hii ilitokana na yeye kuelewa kuwa hata kama angetunga sheria ambayo inaonekana kuwa inabana kila kitu bado Wanasheria wangeweza kupata upenyo na kuweza kumpinga. Inaelekea Chadema na Wanasheria wao wanaamini kuwa hakuna upenyo lakini mimi ninauona. Kwa hiyo naomba nitofautiane nao.
Vifungu vya 41(6) na 41(7) vinatosha kuonyesha matundu kwenye sheria hiyo na hivyo kuiruhusu mahakama kutengua mamlaka ya Kikwete kwa vile uchaguzi wake haukufuata Katiba. Tukumbuke kuwa kesi zote za uvunjwaji wa Katiba zinatolewa maamuzi na mahakama kuu wala siyo bunge kwa hiyo siyo kesi ya impeachment tena.41.-(1) Baada ya Bunge kuvunjwa au kukitokea jambo jingine
lolote lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 38 na
inalazimu uchaguzi wa Rais kufanyika, kila chama cha siasa
kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha
kwa Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jina la
mwanachama wake mmoja kinayetaka asimame kama mgombea
katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na jina la
mwananchama wake mwingine kinayempendekeza kwa nafasi
ya Makamu wa Rais.
(2) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi
wa Rais yatawasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi katika siku na
saa itakayotajwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na
mtu hatakuwa amependekezwa kwa halali isipokuwa tu kama
kupendekezwa kwake kunaungwa mkono na wananchi wapiga
kura kwa idadi na kwa namna itakayotajwa na sheria iliyotungwa
na Bunge.
(3) Endapo inapofika saa na siku iliyotajwa kwa ajili ya
kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea
mmoja tu ambaye anapendekezwa kwa halali, Tume itawasilisha
jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au
kumkataa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii na ya sheriailiyotungwa na Bunge.
(4) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano utafanywa
siku itakayoteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria
iliyotungwa na Bunge.
(5) Mambo mengine yote yahusuyo utaratibu wa uchaguzi wa
Rais yatakuwa kama itakavyofafanuliwa katika sheria iliyotungwa
na Bunge kwa ajili hiyo.
(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote.
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza kuchaguliwa kwake.
Nina doubt kama wewe kweli siyo mwanasheria!Mzee Rugemeleza tuko pamoja. Ingawa siyo msharia, ni mwalimu wa ngumbaru
mimi naunga mkono CHADEMA lakini
Je ni hatua gani zinachukuliwa kufichua kilichofanyika?
Je, kuna precaution zozote zinafanyika ili wakuu wa Dr Slaa wasillishwe kasa na kumpatia Dr. SLAA KASA?
Je, What is the way forward?????
Ninachokiona hapa, watu wataanza kushindwa kumtofautisha Slaa na Lyatonga Mrema. Kama kweli hamtambui Rais awaambie wabunge wake wasiingie bungeni kama walivyofanya wenzao wanaume CUF 1995-2000.
YeshuaHaMelech, nakubaliana na wewe sehemu, jamaa amezama deep, ila kuna watu ambnao sio wanasheria, wanazama sana deep kwenye issues za kisheria, wakati kuna wanasheria wa darasani lakini wanaishia kwenye mambo mengine.Nina doubt kama wewe kweli siyo mwanasheria!
Pasco.. kuna kitu kinaitwa hekima.. wakati mwingine hekima inatufanya tusifanye baadhi ya vitu wakati ambao akili zinatuambia ndio muafaka. Lakini uzuri wa demokrasia ndiyo huo. Chadema wanaweza wakaendelea kutomtambua Kikwete na impact bado itakuwa ni ile ile bila ya kusababisha vitu vingine ambavyo vingekuwa ni distraction. Mimi na wewe tunakubaliana kabisa na hata hiyo tofauti ya wapi kingesemwa kwangu ni very minor kwa sababu ukweli hauitaji jukwaa, unaweza kusemwa popote na ukasimama wenyewe.
Nimekubali yaishe, kama hakwenda kwa hoja za kutumia busara ili asije alaanzisha mengine, then its fine, mimi tafsiri yangu, nilidhani kwa vile amekosa, amenuna hivyo amesusa.Pasco.. kuna kitu kinaitwa hekima.. wakati mwingine hekima inatufanya tusifanye baadhi ya vitu wakati ambao akili zinatuambia ndio muafaka. Lakini uzuri wa demokrasia ndiyo huo. Chadema wanaweza wakaendelea kutomtambua Kikwete na impact bado itakuwa ni ile ile bila ya kusababisha vitu vingine ambavyo vingekuwa ni distraction. Mimi na wewe tunakubaliana kabisa na hata hiyo tofauti ya wapi kingesemwa kwangu ni very minor kwa sababu ukweli hauitaji jukwaa, unaweza kusemwa popote na ukasimama wenyewe.