Elections 2010 CHADEMA yatoa tamko: Hatumtambui Kikwete kama rais

Mzee Mwanakijiji, asante kwa hili, mimi ni mmoja sio wawashabiki wako bali waumini wako sio kwa sababu ya unachoandika, but kwa underlying reasons behind inayokupelekea kuandika unachoandika lakini kwenye hili, naomba kutofautiana na wewe kwenye logic zaidi tukiachana na kufuata tuu imani ya unachoamini japo nakuunga mkono kwenye mengine yote isipokuwa hili, sikuliunga mkono since day one, na sitaliunga mkono mpaka siku ya mwisho, unless otherwise.

Kwa kuanzia, nimeshiriki mchakato wa uchaguzi wetu huu, mwanzo mwisho, nakiri wazi Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imefanya madudu makubwa. Pia nakiri wazi malalamiko ya Dr.Slaa ni genuine, barua ameiandika kwa Tume wameipata na wameionyesha hadharani, kitendo tuu cha kutoijibu barua ile kwa barua rasmi, na badala yake wakaishia kutoa majibu ya kitoto kwa waandishi wa habari, hii tuu ni tosha na justified reasons ya kutoyatambua matokeo na kwa vile haikujibiwa ni genuine reasons ya kufungua kesi ya kikatiba kuhusu uchaguzi wa rais.

Tume imeonyesha udhaifu mkubwa, Jaji Makame amejichokea siku nyingi, Kiravu ndio huyo na majibu yake ya mkato mkato yasiyo na kichwa wala miguu kwa kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu.

Nilichosema mimi Pasco, na ninachoendelea kusema, sio Dr.aende akakumbatiane na mshindi, wala kumpongeza, wala kusaini kuyakubali matokeo, bali haya wanayoyasema sasa, ndio alitakiwa ayasema pale since day one. Sikusema aende ikulu kumpongeza, wala hakuwa hata na haja ya kumshika mkono, lakini alitakiwa awepo pale inside the ring aseme, thats is all!.

Dr. Slaa alishasema msimamo wake tangu mwanzo, kama uchaguzi ni huru na wa haki, atayatambua matokeo na atamtambua mshindi, kama uchaguzi sio huru na wa haki, hatamtambua mshindi na hata yakubali matokeo, hiki ndicho wale waliompa kura zao Dr. Slaa, tulitaka tumsikie akikisema pale pale inside the ring baada tuu ya kuisha kwa pambano, not otherwise, not other time, not other place, it was suppossed to be there and then!.
 
Hatuna ubavu wa kubeza wazo yakinifu kwa sababu ukuu wa hekima zetu hauruhusu hata kidogo.[/QUOTE]
Nakubaliana na wewe, Mahakama ya haki hapa Tanzania ni wananchi na sio mahakama ya CCM.
 
ndicho nilichokuwa nasubiri Dr atamke! ccm ni wezi tena wasiokuwa na huruma na wanachi wanaoteseka kwa sababu yao! wameshijilimbikizia mali ya umma. Dr Slaa mimi nakuunga mkono usikubaliane na wezi wa kura za watanzania
 
Kwa utangulizi huo CHADEMA mmetoa ahueni kwa wapenda haki wengi wanaoitakia mema nchi hii kwa faida ya vizazi vingi vijavyo. Big up Dkt. wa ukweli Wilbrod Slaa na Party nzima. Watanzania wanasubiri mchanganuo wa mchakato mzima ili ijulikane wazi ni kwa kiasi gani " The vote as the voices of the people has been silenced". Watanzania tunasubiri tamko zito la mwisho. Amani na utulivu wa nchi hii utadumishwa kwa wenye dhamana kutenda haki na si mahubiri ya viongozi wa kisiasa majukwaani.
 

Pasco.. kuna kitu kinaitwa hekima.. wakati mwingine hekima inatufanya tusifanye baadhi ya vitu wakati ambao akili zinatuambia ndio muafaka. Lakini uzuri wa demokrasia ndiyo huo. Chadema wanaweza wakaendelea kutomtambua Kikwete na impact bado itakuwa ni ile ile bila ya kusababisha vitu vingine ambavyo vingekuwa ni distraction. Mimi na wewe tunakubaliana kabisa na hata hiyo tofauti ya wapi kingesemwa kwangu ni very minor kwa sababu ukweli hauitaji jukwaa, unaweza kusemwa popote na ukasimama wenyewe.
 
Wamarekani yawapongeza wa TZ kwa kukamilisha uchaguzi na ampongeza Dr Shein. JK je??????????????????????

U.S. Embassy Tanzania
Press Release
November 13, 2010

The White House
Office of the Press Secretary
For Immediate Release
November 13, 2010
Statement by the President on Elections in Tanzania
On behalf of the United States, I congratulate the people of the United Republic of Tanzania on your recent national election and your continued commitment to a tradition of multiparty contests begun in 1992. I look forward to working with President Jakaya Kikwete and the members of the Tenth Parliament as we build on the long, fruitful partnership between our nations to advance shared development goals and tackle the many global challenges before us

I also extend my congratulations to Zanzibar’s President Ali Mohamed Shein, First Vice President Seif Sharif Hamad, the new unity government, and most especially the Zanzibari people, who have made history by conducting a peaceful contest after years of strife. As I said to President Kikwete when we met at the White House in 2009, the people of the United States support all Tanzanians in your efforts to institutionalize democratic, transparent governance, to realize the full potential of your Union, and to ensure that the steps you have taken together toward a lasting peace and prosperity cannot be reversed
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, November 15, 2010
 
Mbona hilo liko wazi Kiranga usichanganye watu rais ni sehemu ya bunge means president is a subset of bunge as universal bunge lina uwezo wa kumuondoa rais bungeni.

Labda kuonesha kuwa Rais ni sehemu ya Bunge tutumie maneno haya 'parliament' ni wabunge pamoja na Rais wanapokaa pamoja na ndio maana huwa anamalizia kazi ya kutunga sheria kwa kuweka sahihi; pia kuna 'national assembly' hapa ni pale Rais hayumo kwenye mijadala ya Bunge. Hivyo Rais ni sehemu ya Bunge kwa maana ya parliamnet.
 
Kipenzi chenu lakini wengi hamkujitokeza kupiga kura mrifikiri kura zitajipiga automatic kwa mapenzi yenu au mawazo. Elimisheni Watu kwa ajili ya uchaguzi ujao 2015 ama sivyo matokeo yatakuwa kama haya.Kwa sasa hivi kuleta malumbano hakutasaidia sana kwa sababu uchaguzi wa rais hauwezi kurudiwa tena wala Rais hawezi kutenguliwa kwa sasa kutikana na malalamiko ya Chadema.
Angalieni hizi kauli za kutomkubali Rais na matokeo yanaweza kutupeleka kule nyuma kama ilivyokuwa Zanzibar kabla ya maridhiano kitu ambacho hakuna Mtu anetakia mema taifa hili atapenda.
Mungu ibariki nchi yetu na watu wake tukae kwa amani. Amen
 

Mzee Rugemeleza tuko pamoja. Ingawa siyo msharia, ni mwalimu wa ngumbaru, nina imani kubwa sana hakuna sheria ya mabavu iliyowahi kutungwa duniani hapa ikabana watu wakakosa pa kupitia. Wanasheria watapanua matundu machache yaliyoko kwenye sheria hiyo na kutoa upenyo mkubwa. Sheria hiyo ya uchaguzi wa rais kwa mujibu wa katiba ina matundu kadhaa ya kupanua kama nitavyoonyesha baahdi yake hapa chini. Kwanza ngoja niinukuu hapa chini halafu nionyeshe matundu yanayoweza kutumiwa na wanasheria.

Vifungu vya 41(6) na 41(7) vinatosha kuonyesha matundu kwenye sheria hiyo na hivyo kuiruhusu mahakama kutengua mamlaka ya Kikwete kwa vile uchaguzi wake haukufuata Katiba. Tukumbuke kuwa kesi zote za uvunjwaji wa Katiba zinatolewa maamuzi na mahakama kuu wala siyo bunge kwa hiyo siyo kesi ya impeachment tena.

Nitaanza na kifungu cha 41(7) kinachosema hivi "Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.


Kuna matundu mawili kwenye kifungu hicho kama nilivyonyesha kwa rangi nyeusi:

  • Mahakana zinazuiwa kuchunguza kuchaguliwa kwa rais lakini hazizuiliwi kusikiliza na kutolea maamuzi malalamiko yatolewayo na raia kuhusu kuchaguliwa kwa rais huyo. Siamini kuwa ni wajibu wa mahakama zetu kuchunguza kesi, bali ni kusikiliza kesi kama zinavyoletwa na walalamikaji na kuzitolea maamuzi.

  • Kifungu hiki kinazungumzia mtu aliyeachaguliwa kuwa rais kwa mujibu wa ibara hii (yaani ibara ya 41). Kwa hiyo kama Tume itamtangaza mtu ambaye hakuchaguliwa kwa mujibu wa ibara hii, basi kifungu hakitumiki.

Baada ya hapo ninarudi nyuma kwenye kifungu cha 41(6) kiachosema kuwa "Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote.

  • Kifungu hiki ndicho kinachoweza kubatilisha hiyo kinga iliyomo kwenye kifungu cha 41(7) hapo juu. Kama CHADEMA watakuwa na ushahid wa kutosha kuwa Tume ilimtangaza Kikwete kama mshindi huku akiwa hakupata kura za kuwashinda wagombea wengine, basi itakuwa ni dhahiri kuwa kutangazwa kwa Kikwete kama mshindi wa urais ni kinyume cha ibara hii ya 41, hivyo kifungu cha 41(7) kinakuwa hakifanyi kazi tena.
SIjapata upenyo wa kusoma sheria ya uchaguzi kwa hiyo siwezi kukoment lolote kuhusu kifungu cha 41(5) kinachosema "Mambo mengine yote yahusuyo utaratibu wa uchaguzi wa Rais yatakuwa kama itakavyofafanuliwa katika sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo. Inawezekana kuna mambo mengine yanayoweza kuonekana kuwa Tume ilikosea.
 
Nafikiri huu ndio mwanzo wa kudahi katiba mpya,Chadema wanaangalia ni kwa jinsi gani wananchi watawaunga mkono katika mchakato mzima wa mabadiliko ya ukweli.
mimi naunga mkono CHADEMA lakini

Je ni hatua gani zinachukuliwa kufichua kilichofanyika?
Je, kuna precaution zozote zinafanyika ili wakuu wa Dr Slaa wasillishwe kasa na kumpatia Dr. SLAA KASA?
Je, What is the way forward?????
 
Nadhani CHADEMA lazima ionyeshe ukomavu wa kisiasa hapa. Matamko shallow na yasio rasmi hayana maana. kutomtambua maana yake ninini kwa sasa. Wanachama wachadema wafanye nini huko waliko. Je wabunge walioko mjengoni watoke au wafanye nini. leo anamteua waziri mkuu atakaye thibitishwa na bunge ambapo Mbowe na wenzake wapo. Je watatoka nje kuonyesha msimamo wao kuwa hawamtambui rais na mteule wake??? Nasubiri kwa hamu. Wakishindwa kufanya hivyo nawaomba waache sanaa za kisiasa tusonge mbele.
 
Aliyekuwa mgombea Urais kwa kupitia Chadema amesema hatamtambua Rais Kikwete kwa kuwa hakupiti kihalali,na msimamo wa chama ndio huo.Mimi binafsi pamoja na kupenda amani ya Tanzania lakini sipendi kabisa kuongozwa na wasanii(washinda uchaguzi kwa hila) kwani ataendelea kutenda hila tu kwani ni sawa na kula nyama ya mtu hutaacha utaendelea tu.Naomba maoni yenu wana JF.
 
Ninachokiona hapa, watu wataanza kushindwa kumtofautisha Slaa na Lyatonga Mrema. Kama kweli hamtambui Rais awaambie wabunge wake wasiingie bungeni kama walivyofanya wenzao wanaume CUF 1995-2000.

Wabunge ni wawakilishi na watetezi wa wananch,kutokuingia bungeni ni kuwanyima wananchi haki yao lakini pia kumkubali Rais aliyeshinda kwa kuchakachua matokeo ni sawa na kuwanyima haki wananchi ambao kwa sehemu kubwa wanamjua rais waliyempigia kura.
 
Nina doubt kama wewe kweli siyo mwanasheria!
YeshuaHaMelech, nakubaliana na wewe sehemu, jamaa amezama deep, ila kuna watu ambnao sio wanasheria, wanazama sana deep kwenye issues za kisheria, wakati kuna wanasheria wa darasani lakini wanaishia kwenye mambo mengine.
 

Mkuu naomba niongezee kitu hapa.
kwa hekima natumai Dr.Slaa hakuweza kulitamka hili la kutomtambua Kikwete(matokeo ya Urais) on the spot, kwa kujua kwamba hali iliyokuwepo haikuwa njema.Hivyo pangezuka vurugu zaidi kwani tayari NEC walisha watibua wanachi.Sasa angeongezea na hili natumai kile kilichowafafika watani zetu Kenya tungekishuhudia hapa.
 
Nimekubali yaishe, kama hakwenda kwa hoja za kutumia busara ili asije alaanzisha mengine, then its fine, mimi tafsiri yangu, nilidhani kwa vile amekosa, amenuna hivyo amesusa.

At this juncture, Chadema watunme barua nyingi NEC na kuwacopy UNDP kuomba access ya NEC data base, huko tutaona scanned copies za matokeo yote kituo kwa kituo, na walinganishe za zile signed copies za mawakala wao, wakithibitisha tofauti, this is a proof before the court of law.

Ubalozi wa Uingereza na wafadhili wengine, wametumia mabilioni ya fedha kuiwezesha NEC kufanya uchaguzi huru na wa haki usiokuwa na madudu madudu yasiyoeleweka, kama Chadema wakiprove uchakachuaji wa NEC, jumuiya yote ya kimataifa ita smphasise na Chadema, na yatafuatia mashikizo ya kuhahakikisha utumbo kama huu hautokeo 2015, jamaa ajichukulie nchi kiulaini na kwa amani.
 
Kuchezea kura zilizopigwa na wananchi ni kosa la jinai. Kwa hiyo wote waliohusika wanatakiwa kukemewa kwa nguvu zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…