Elections 2010 CHADEMA yatoa tamko: Hatumtambui Kikwete kama rais

Nakubaliana kuwa kutokana na katiba kuwa mbovu rais (japo feki) hashtakiwi. je, hakuna hatua nyingine za kisheria zitakazoletea kupata tume huru na kuondokana na hii ya akina ki-love (kunta kunte au ledy gaga)?
 
hatua zaidi zichukuliwe na chadema,mfano operesheni PAPA/NYANGUMI.
 
MImi pia naungana na Chadema, Sitamtambua mshindi alietangazwa na NEC katika mazingira tatanishi
 
kama nilimsikia vizuri . Mbowe alisema muda si mrefu watatoa matokeo halisi ya uchaguzi kama yalivyo bandikwa na kusainiwa na mawakala kutoka vituo vya uchaguzi.
I hope kuwa baada ya hapo ataeleza next move. Lets be patience.
Nashauri chadema wasikawie sana kutujuza mengineyo yanayojiri.
 
Naam tumesubiri kwa hamu sana hili tamko
nalo ni msimamo wa wapiga kura tulioibiwa kura zetu na NEC ya kikwete.

Maadam sasa tumepata msimamo, kinachojengeka kwenye saikolojia yangu ni kwamba huyu Kikwete ni kiongozi dhalimu na hafai kwa maongozi kwani amejiweka madarakani kiuhalifu
 


Penye red: hayo ni majibu ya kirahisi. Yaani umesha ku-conclude beyond reasonable doubt kwamba majority wale ambao hawakujitokeza kupiga kura ni wapinzani tu(eg Chadema)? Kwa kigezo kipi?

Kama ni hivyo basi kuna something very sisnister about the historical low turn-out this year. Kimakusudi ilifanyika kulenga wapinzani. Tume huru kuchunguza hili ndiyo pekee inaweza kupata ukweli ya kilichojiri katika zoezi zima la kujiandikisha na upigaji kura.
 
Watanzania tunajua Kikwete si rais halali maana kasimikwa na tume ya uchaguzi kwa ushawishi wake mwenyewe. Anaweza kupongezwa au kutopongezwa. Huo ni uamuzi wa nchi husika kuamua wanavyoona.
Bado binafsi simtambui Kikwete kama rais wangu. Mungu nisaidie!
 

Kuna wakati nilitaka kukata tamaa kusikia kauli za wakubwa wetu hawa (hasa mheshimiwa Presida Dr. Slaa). Hebu kamilisheni hilo sosi mtuwekee mezani waungwana maana mtutasababishia vidonda vya tumbo kwa uchu wa kungoja chakula. NAWAAMINIA WAKUU WETU
 
Hata kama CHADEMA wangemtambua,mimi sikumtambua na sitamtambua kwa miaka mitano.I said it and I repeait it again.."As for me and my family,We shall follow Dr. Slaa as our President"
 
hatua zaidi zichukuliwe na chadema,mfano operesheni PAPA/NYANGUMI.

Mukubwa Mmaroroi hapa umenena.....ila ukiachilia mbaliCHADEMA kama viongozi, na sisi kama pro-mabadiliko tunapaswa kuanza kuchukua hatua. Hapa njia ya mabadiliko itakuwa wazi kabisa kama kumsukuma.............
 
Mimi namtumbua jk. Sijapata data za kutosha kunishawishi kuwa alliba kura. Mwenye nazo alete. Tujue idadi ya watu waliopigia kura wabunge na madiwani kisha tujue idado ya waliopiga kura ya urais. Tofauiti ya kura moja hadi laki moja inakubalika. Zaidi ya laki nitatia shaka.
Namkubali jk. Lakini pia nchi hawezi pewa muhuni!!!
 
Mimi nakubaliana na tamko la chadema kwa sababu sisi sote tumeona Dr Slaa pamoja na Chadema wakiandamwa muda wote wa kampeni na hadi wakati wa uchaguzi.

Na kwa ushahidi majimbo yote ambayo Chadema imeshinda kura zilirudiwa mara mbili au tatu kabla ya kutangazwa.

Vilevile kuna baadhi ya sehemu mshindi wa pili ndio anatangazwa mbunge mfano Mvomero, Sh/Mjini, Kahama etc.

Katika hali kama hii huwezi kusema uchaguzi ulikuwa huru na haki hatakidogo.

Peoples Power
 
 
Kikwete ni rais wangu na wenu ninyi wote ndani ya jf, mpende msipende.
Nguvu ya umma ndio iliyomuweka madarakani
nguvu ya umma ndiyo iliyowapa ubunge wabunge 22 wa chadema

Poor thinking I think, 5 million votes out of 19 million? nguvu ya umma haikumchagua, wameshachoka na wizi hawaoni sababu tena, kitakachotokea ndio hatujui maana kama watu hawaamini kura zinaleta viongozi bora wanalo wanaloliamini, hata wewe walijua nafikiri
 

Ukitaka kujua watu walivyo na hasira ni Dr. Slaa atakapokosea akaitisha maandamano ya amani, watu watashangaa mamilioni ya watu watakaohudhuria. Kumkataa to me is a soft approach kwa kweli
 
Chadema kutangaza kutomtambua Rais ilhal imeshaunda KUB na itaunda serikali kivuli itakayokuwa chini ya Rais wanaemkataa na hapo hapo kwa kujua Rais ni sehemu ya Bunge hamuoni usanii hapo? Au Chadema imekuwa CCM C?
 
kweli hatumtambui Kikwete kesha anza ngebe zake anahamisha Ma RPC,na RC kwenye mikoa yote walioshinda CHADEMA hii inadhihirisha kuwa walikataa kuingia mkenge wa kunyang'anya haki za wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…