Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 321
- 691
“Electronic Balloting System (EBS)”, ni mfumo wa kupiga kura kidigitali, yaani kwa kutumia vifaa maalum vya tarakilishi. Mfumo wa kutumia tarakilishi katika uchaguzi sii mgeni hapa Tanzania, kwani toka mwaka 2015 Tume ya Uchaguzi nchini ilianza kuutumia kwa kuandikisha na kuhakiki wapiga kura. Mfumo huu unaitwa “Biometric Voter Registration – BVR”. Kumbe hakutakuwa na gharama kubwa ya ziada kuingia kwenye mfumo wa kupiga kura kidigitali, ni kuongeza vifaa vichache tu, na mfumo huu unaweza kuandaliwa na Wahandisi wetu wa Tehama walioajiriwa ndani ya serikali na/au wale wa sekta binafsi. Kama mfumo huu utaridhiwa na kuanza kutumika, kwa ujumla utapunguza sii tu kero za uchaguzi, bali gharama za kifedha kwa kiasi kikubwa.
Kilelezo Na. 1: Zoezi la Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015
Chanzo: “Tanzania Election Monitoring Committee”
Tunapozungunza habari ya Uwajibikaji na Utawala Bora katika ngazi ya Taifa, huwezi kutenganisha na chaguzi zinazowaweka viongozi katika ngazi mbalimbali za maamuzi. Chaguzi zinazofanyika Tanzania kila baada ya miaka 5, huleta Mwenyekiti wa Mtaa/Kijiji na serikali yake; Diwani wa Kata, Mbunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mwakilishi wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Zanzibar, na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tume ya Uchaguzi imekuwa inajitahidi kuboresha mfumo wa uchaguzi mara kwa mara, lakini bado dosari zinaendelea kujitokeza, na hivyo kuwafanya wadau mbalimbali kuendelea kulalamikia mfumo wa Uchaguzi.
Hii ndio sababu iliyonifanya nije na pendekezo hili la kufanya Uchaguzi kwa kutumia mfumo wa kidigitali (Electronic Balloting System – EBS). Sasa haimaanishi mfumo huu wa EBS pekee ndio utakuwa muarobaini wa matatizo ya chaguzi hizi, la hasha; ni lazima uende sambamba na mageuzi ya tume ya uchaguzi, ndipo utazaa matunda yanayotarajiwa!
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC)
Kwa kifupi, ufuatwao ni muundo wa Tume: Mwenyekiti wa Tume na Sekretarieti yake - ngazi ya taifa; Wakurugenzi wa Uchaguzi ngazi ya wilaya (majimbo) – ambao ni Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji/Manispaa/Miji/wilaya; Maafisa Uchaguzi ngazi ya kata, ambao ni Maafisa Watendaji wa kata.
Kimtizamo, muundo huu kwa kiasi kikubwa una mgongano mkubwa wa kimaslahi! Kwanini? Mwenyekiti wa Tume anateuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (au Rais wa Zanzibar kwa upande wa Zanzibar – ZEC) aliyepo madarakani, ambaye aidha yeye au mtu mwingine kutoka chama chake ni mgombea wa uchaguzi husika.
Kwa kuwa mfumo wa uchaguzi unafanana kati ya Tanzania bara na Tanzania visiwani, katika maelezo yangu nitajikita zaidi upande wa Tanzania bara.
Wakurugenzi wa Uchaguzi ngazi ya wilaya ni Wakurugenzi wa Halmashauri husika za jiji/manispaa/mji/wilaya, ambao pia ni wateule wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania; na Maafisa Uchaguzi ngazi ya kata, ni Maafisa Watendaji Kata, ambao ni waajiriwa wa Wakurugenzi wa Halmashari (Jiji/Manispaa/Mji/Wilaya) husika. Vilevile, uzoefu unaonyesha kwamba wasimamizi wakuu katika vituo vya kupigia kura kwa kiasi kikubwa huwa ni wanajeshi wa Jeshi la Wananchi, ambao wapo chini ya Amiri Jeshi Mkuu (ambaye ni Rais wa nchi).
Kimuundo, Mkuu wa Wilaya ni mteule na mwakilishi wa Rais, ndiye msimamizi wa vyombo vyote vya usalama wilayani kwake, pia ni Msimamizi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji/Manispaa/Miji/Wilaya zilizopo wilayani kwake.
Katika ngazi ya mkoa, kuna Mkuu wa Mkoa, ambaye pia ni mteule wa Rais, ni kiongozi wa Wakuu wote wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Jiji/Manispaa/Miji/Wilaya mkoani kwake; na Mkuu wa vyombo vyote vya usalama mkoani kwake.
Kwa muktadha huu, utaona Tume ya Uchaguzi imebebwa na serikali nzima kuanzia ngazi ya kata hadi ngazi ya taifa. Kwa akili ya kawaida, viongozi na watumishi wa serikali ambayo ina wagombea wa uongozi katika ngazi mbalimbali, watapenda kuona ushindi unabaki upande wao.
Tuhuma kwa Viongozi wa Serikali na Vyombo vya Ulinzi na Usalama za Kuvuruga Uchaguzi
Kila kipindi cha Uchaguzi Mkuu, kumekuwa na tuhuma nyingi kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali dhidi ya viongozi wa serikali, pamoja na vyombo vya ulinzi za kuvuruga uchaguzi kwa lengo la kuwawezesha wagombea fulani (hasa wa chama tawala) kushinda, hata kama hawakustahili kupata ushindi.
Habari hizi zinathibitishwa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), Idhaa ya Kiswahili (Oktoba, 30, 2020), ambapo lilinukuu Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, ukisema, unataka kero za uchaguzi zishughulikiwe.
Taarifa inaendelea kusema, Ubalozi huo kupitia tamko lake lililotolewa Oktoba 29, 2020 unasema kufanya hivyo kutarejesha imani na kutekeleza azma ya kuheshimu utawala wa sheria na dhana ya Utawala Bora.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hii, malalamiko haya yalipingwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania kwamba hayana ukweli kupitia kwa Mwenyekiti wake, Jaji Kaijage.
BBC iliendelea kusema, Serikali ya Marekani imeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu ripoti za uhakika kwamba kulikuwa na kusambaa kwa dosari nyingi katika upigaji kura, kuingilia kati kwa huduma ya intaneti, ukamataji, na ghasia ambazo zimefanywa na majeshi ya usalama kote Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Kuhusiana na tuhuma hizi za vurugu katika zoezi la uchaguzi mkuu, Sauti ya Amerika - VoA (Novemba 2, 2020), ilimnukuu Waziri wa Mambo ya Nje (Marekani) Mike Pompeo akisema, “Marekani kwa kushirikiana na washirika wake, wanafikiria hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuweka masharti ya visa, kama inavyoona ni muafaka, kuwawajibisha wale ambao wamegundulika kuhusika na ukiukaji wa haki za binadamu na kuingilia kati utaratibu wa uchaguzi”.
Hitimisho
“Electronic Balloting System (EBS)” na Muundo Mpya wa Tume ya Uchaguzi utapunguza, kama sii kumaliza kabisa dosari za uchaguzi mkuu; kwani matokeo yatakuwa wazi mara tu baada ya zoezi la kupiga kura kumalizika..
Pamoja na matumizi ya vifaa vya kidigitali katika zoezi la upigaji kura, napendekeza muundo mpya wa Tume ya Uchaguzi kama ifuatavyo: Mwenyekiti na Sekretarieti yake waajiriwe kwa njia ushindani na tume maalumu itakayoundwa kisheria na Mhimili wa Mahakama. Watendaji wa Tume ngazi ya wilaya, kata na vijiji/mitaa waajiriwe na Sekretarieti ya Tume ya Uchaguzi ngazi ya Taifa. Hii ndio itakayokuwa Tume ya Uchaguzi huru, ambayo haitaingiliwa na viongozi wa kisiasa katika ngazi yoyote.
Marejeo
Sauti Kubwa (Machi 4, 2021) “Tanzania Election was Rigged”.
Sauti ya Amerika (Novemba 2, 2020), Marekani Yasikitishwa na Dosari za Uchaguzi Mkuu Tanzania.
Shirika la Habari la Uingereza (BBC), Idhaa ya Kiswahili (Oktoba 30, 2020), Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Ubalozi wa Marekani wataka kero za uchaguzi kushughulikiwa.

Upvote
6