Chakula cha Mama Ntilie ni kwaajili ya masikini

Chakula cha Mama Ntilie ni kwaajili ya masikini

Hao mama ntilie ndio waliotukuza mpaka tukakua. Heshimu kazi za watu mkuu.

Halafu naona umekuja na ID mpya baada ya ile ya mwanzo kubumba.

Mr. whyme

By the way, vipi kuhusu ule utajiri wa kutoa kafara, ulifanikiwa?
 
Sina mengi wakuu nawasalimu.
Hii misosi ya mama nitilie ni kwaajili ya maskini.
Mabenchi machafu
Viti vimevunjika
Meza chafu, inzi wakutosha
Msosi sometimes unanuka moshi
Wahudumu wachafu
Customer care iko chini.
Kula kwa mama nitilie ni umaskini au labda ukumbwe na dharuura.
Mchele wanapika ule wa 1100/-(wa bei ya mwisho)
Nyanya wanatumia yale masalo wanayouza mateja.
Chapati au maandazi ya mama nitilie viko chini ya kiwango.
Wewe unaongelea matanda yale machafu machafu au aina ya mama ntilie na uchafu wake.

Mimi ninakwenda kwa mama ntilie siyo kwa sababu ya kukosa elfu 10-15 ya chakula,ninaweza sana kula chakula cha namna hiyo isipokua [emoji116]

1. Mama ntilie kachinja kuku wake asubuhi na kampika vizuri mwenye ladha kichwani na ni kuku wa kienyeji

2. Mahotel makubwa tunako lala tukisafiri au yaliyo jirani na kazini kwetu yanauza kuku wale wenye presha,kuku amekaa kwenye jokofu wiki 92. Analazimishwa kua mwenye ladha kwa viungo vingi vya viwandani pia

3. Mama ntilie msafi ana chakula kizuri chenye bei nafuu, labda tu ungeongelea usafi ningekuelewa maana hata hayo mahotel makubwa yapo ambayo usafi ni sifuri.

4. Peleka balaa mbele
 
Kwa mama ntilie/lishe nakula;
Ugali + mboga za majani + nyama finyango mbili/tatu + maharage + dagaa, nachukua tunda langu au juice yangu na jumla haizidi 3,000/.

Niambie wewe kwenu unapika ugali na mboga ngapi?
 
Sina mengi wakuu nawasalimu.
Hii misosi ya mama nitilie ni kwaajili ya maskini.
Mabenchi machafu
Viti vimevunjika
Meza chafu, inzi wakutosha
Msosi sometimes unanuka moshi
Wahudumu wachafu
Customer care iko chini.
Kula kwa mama nitilie ni umaskini au labda ukumbwe na dharuura.
Mchele wanapika ule wa 1100/-(wa bei ya mwisho)
Nyanya wanatumia yale masalo wanayouza mateja.
Chapati au maandazi ya mama nitilie viko chini ya kiwango.
Hapa Kilombero hiyo ndo bei ya mchele supa
 
Fukua baba

JF bana
 
Alichoongea mshikaj ni sahihii sana hawa madada wanajiendekeza sana ya unakuta wali mtu anapikia mchele wa vitumbua chuya kibao ata mtu kupeta tu hawez kutoa pumba juz yamenikuta aisee nlivokiona tu chakula nilirudisha na maneno nlimpa yule dada sijui uwa wanafanya makusud I...

Lkn kuna dada mmoja nje ya ofisi yetu ana mazingira ya hovyo sana mabench machaf lkn chakula anachopika apo mitaa ya kamata ni balaa buku 2 tu lkn ukikikuta sehem iliyoboreshwa ni 7000 ama 10000
 
Lakini vinatutoa shavu mkuu Tena unapimiwa mzigo wakutosha Mboga Kama zoote yaani tunafaidi Sana

Ila ukienda kwenye hotel zenye hadhi msosi unapewa Kama umeomba Tena ukute hakijaiva vzr na wananyodo Sana wahudumu wahiyo mihotel

Yalinikuta apo shef pride birian ata halielewek kuku anatoa harufu ya kuharibika mwisho wa siku ten ikamtoka tajir mi roho inaniuma tu...
 
Sina mengi wakuu nawasalimu.

Hii misosi ya mama nitilie ni kwa ajili ya maskini.

  • Mabenchi machafu
  • Viti vimevunjika
  • Meza chafu, inzi wakutosha
  • Msosi sometimes unanuka moshi
  • Wahudumu wachafu
  • Customer care iko chini

Kula kwa mama nitilie ni umaskini au labda ukumbwe na dharuura.

Mchele wanapika ule wa 1100/-(wa bei ya mwisho)

Nyanya wanatumia yale masalo wanayouza mateja.

Chapati au maandazi ya mama nitilie viko chini ya kiwango.
Ndugu tajiri sijakuona kwenye orodha ya Forbes au wamesahau jina lako tuwashtaki
 
Chakula cha mama ntilie kimenisaidia sana hasa kipindi nipo chuo ila kuna baadhi ni wachafu. Kuna kipindi flani niliingia mgahawa flani mbezi mwisho nikaagiza chakula wakaniletea na kijiko kichafu! njaa yote iliniisha nikaghairi kula
 
Sina mengi wakuu nawasalimu.

Hii misosi ya mama nitilie ni kwa ajili ya maskini.

  • Mabenchi machafu
  • Viti vimevunjika
  • Meza chafu, inzi wakutosha
  • Msosi sometimes unanuka moshi
  • Wahudumu wachafu
  • Customer care iko chini

Kula kwa mama nitilie ni umaskini au labda ukumbwe na dharuura.

Mchele wanapika ule wa 1100/-(wa bei ya mwisho)

Nyanya wanatumia yale masalo wanayouza mateja.

Chapati au maandazi ya mama nitilie viko chini ya kiwango.

IMG_7075.jpg

Mimi huwa nakula kwa mama lishe nikiwa kwenye shughuli zangu. Kiukweli huyu mama lishe na timu yake napenda chakula chao ni kitamu kwa ladha, mpaka wali ni wa nazi, mboga nyingi, hapa ningekuwa nimeagiza ugali mboga zingeongezeka kama mlenda , maharage
Sijawahi kukutana na changamoto zikanipelekea kukereka kula kwa mama ntilie
Chakula hicho ni Tsh.2,000/= na bei hiyo ni kutokana na eneo hilo yani hiyo bei ni ya juu
Pengine bei ni Tsh.1,500|=kwa wali ugali mpaka 1,000/=.
Hawa watu nawaheshimu sana.
 
Sina mengi wakuu nawasalimu.

Hii misosi ya mama nitilie ni kwa ajili ya maskini.

  • Mabenchi machafu
  • Viti vimevunjika
  • Meza chafu, inzi wakutosha
  • Msosi sometimes unanuka moshi
  • Wahudumu wachafu
  • Customer care iko chini

Kula kwa mama nitilie ni umaskini au labda ukumbwe na dharuura.

Mchele wanapika ule wa 1100/-(wa bei ya mwisho)

Nyanya wanatumia yale masalo wanayouza mateja.

Chapati au maandazi ya mama nitilie viko chini ya kiwango.
unaweza kuwasaidia vipi sasa, watu wanasomesha watoto na sisi wengine tumekuzwa na vyakula hivyohivyo, acha dharau.
 
Mama Ntilie nao wako na classes zao..mimi kuna baadhi ya mama Ntilie huwezi kunilisha chakula chao asee hasa mama Ntilie wa Dodoma ni wachafu hatari.
Dodoma [emoji1787][emoji1787] Ni kweli unakuta chapati Ina mchanga
 
Hivi wakuu yule aliesemaga usafiri wa daladala ni kwa masikini tu sio huyu kweli?
 
Huuu ni ukweli usiopingika mkuu,, Mama ntilie ni huduma kwa ajili ya makapuku, mwenye hela hawezi kula kwa mama ntilie.. Me nayesema hivi ni miongoni mwa mwa makapuku na ndo maana nasupport hv ni kutoka na ushuhuda was wazi kabisa nilionao..
Sisis makapuku pekee ndo tunakula kwa mama ntilie
Vyakula vya hotelini vingi havina ladha chunguza utajaniambia,
 
Kwenye hiyo migahawa unayoiamini ndiko ambako vyakula visipoisha vinawekwa kwenye mafreezer,kesho yake vinapashwa.
 
Supu yangu ya mapupu ya jelo na mihogo mitatu ya nguvu ya mia sita paleeee stesheni.......asante mama ntilie
 
Back
Top Bottom