Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Mlonge nikinywa aisee naugua hapo hapo, kizunguzungu na mwili kukosa nguvu, nimejaribu mara kwa mara lakini hali ni hiyo hiyo nikunywa mlonge ni balaa, pia makongoro yalinishinda
Yaani ulivyoyataja makaongoro leo lazima nikayapige jioni. Yale makitu matamu sana
 
Chapati za maji (kumimina) mbona hazina shida. We mshamba wa wapi.
ivi we unaakili kweli? Acha kukurupuka mie nazungumzia injera za Ethiopian,Somalian, zina upishi wake bob, sio chapati za maji za kawaida
8E069D10-F9F0-4499-9501-AB0EECFEB2B6.jpeg
 
Mimi kwakweli kuna mboga inaitwa choroko .halafu nilikua ugenini walipika na wali..nilikula kwa mateso sana hiyo siku.
 
Ni kweli Kuna vyakula hatuvipendi au hatuwezi kula.

Ila ukikutana na kitu kinaitwa NJAA, Namaanisha ile njaa ya kweli kweli ya kama mtu aliyefukiwa na kifusi ardhini kwa siku Tatu, na uhakika utakula tu tena hata wadudu watambaao utawaona kama lulu, na hata hivi vyakula tunavyovitaja ambavyo vingine tumevitaja tu kwasababu tuna choice au mmbadala wake. Tutakula tu bila hata ya kushikiwa mtutu wa bunduki.
 
Back
Top Bottom