Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Mtu yuko serious kbsa anakutuma buchani ukamnunulie utumbo wa ng'ombe

halafu anakwambia eti "huu nikiunga na nazi,utajilamba nakwambia" yaniiii

huo utumbo hata ukatie humo noti za elf kumi kumi upike siliii ng'o,hata harufu staki iskia...
 
Loshoroo, ngararimo, anjero, nyama ya kondoo, ghee

Wee ngararimo ile kituu tamu hivyo asee na chai ya rangi naweza kula chungu kizima full kujamba mpaka inzi wanakufa [emoji1] alafu yale ya mahindi kwanza (maturu) nayapiga kwanza wakiweka maharage ndio balaa kabiisa
 
Mtu yuko serious kbsa anakutuma buchani ukamnunulie utumbo wa ng'ombe

halafu anakwambia eti "huu nikiunga na nazi,utajilamba nakwambia" yaniiii

huo utumbo hata ukatie humo noti za elf kumi kumi upike siliii ng'o,hata harufu staki iskia...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]yaan umenichekesha, utumbo umekufanya nn ndugu yangu
 
Mm ni kama nguruwe tu sibagui, sichagui chochote kinacho katiza mbele yangu nakula ilimradi kiwe kimepikwa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]yaan umenichekesha, utumbo umekufanya nn ndugu yangu
Unakulaje kitu kinahifadhi takataka zote za mwili?

yani nyama zote kuna paja,kidari,kifua,Filet,na sehemu kibao

mtu zote hizo hazioni anakwambia pitia buchani niletee UTUMBO😟
 
Unakulaje kitu kinahifadhi takataka zote za mwili?

yani nyama zote kuna paja,kidari,kifua,Filet,na sehemu kibao

mtu zote hizo hazioni anakwambia pitia buchani niletee UTUMBO[emoji45]
Mkuu mbona husemi watu wanakula maini ambapo sumu zote zinachujwa na tena ni bei kuliko nyama zote ktk ng'ombe, kila sehemu ya nyama inaladha yake wapo watu wanapenda ladha ya utumbo wengine wanakula hadi kwato[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu mbona husemi watu wanakula maini ambapo sumu zote zinachujwa na tena ni bei kuliko nyama zote ktk ng'ombe, kila sehemu ya nyama inaladha yake wapo watu wanapenda ladha ya utumbo wengine wanakula hadi kwato[emoji23][emoji23][emoji23]
Maini yanafata ila kwa ng'ombe nyama ghali na sehemu Gharama zaidi ni

nyama ya Fillet,ng'ombe mzima anaweza kutoa fillet kilo 3-5 tu na ni nyama

laini yenye ladha kuliko nyama ya sehemu zingine ktk mwili wa ng'ombe,5 star hotel

hutengeneza mishkaki ya Fillet ni mshkaki unaouzwa gharama kuliko hii mishkaki mingine.

sema kuna watu ni kula kula sana kama pumbu tu za ng'ombe/mbuzi zinaliwa,ije kuwa hizo kwato?

yawezekana kuna wajuba kwato kwao wanaona kama crips vile,kama kakau flani ameiziiiing 😂 😂 😂
 
Mkuu Fillet ndio nyama ya wapi hiyo katika ng'ombe sababu nimecheki Fillet it's just boneless meat au kwa kiswahili tunaweza kusema ni minofu hata kwa samaki inaweza tolewa hiyo Fillet. Sasa sijajua wewe mkuu Fillet umemaanisha ni nyama gani ni nundu au..
 
Fillet ya ng'ombe ni sehemu ambayo ipo ndani ya mbavu ni sehemu ndogo sana yenye nyama ndefu kama kamba nyama ambayo wewe kapuku mwenzangu unaweza usiijue na usiweze iona kwasababu fillet hununuliwa kwenye mahotel makubwa na sehemu wanazopika vitu classic kwa wateja ambao pesa si tatizo kwao.

Fillet kilo.1 buchani jirani ninaponunua nyama kila siku inauzwa 15,000 sasa piga hesabu hiyo nyama ikitengenezwa mshkaki huo mshkaki utauziwa sh ngapi wewe ili yule mnunua ile fillet nae arudishe hela yake na apate faida Juu?

Hii ndio picha ya ng'ombe na sehemu zake ambapo fillet inapatikana



Hiyo picha ya kwanza

Picha ya pili inayokuonyesha fillet inapopatikana kwenye ng'ombe



ni kasehemu kadogo sana kanakotoa nyama kama kilo 3-5 kwa ng'ombe alienona kweli kweli,Fillet ukiikuta imeandaliwa imekaa mkao wakutumika muonekano wake ndio kama huu hapa chini



huo mzigo hapo ni laini kiasi kwamba hata steki ya kwenye paja au kidari haikuti ulaini wa hiyo nyama,ni nyama ambayo wakati wakutengeneza mishkaki yake inahtaji utaalamu mkubwa sana otherwise unaiharibu inapukutika yote.

achana na steki unazoziona kwenye mapaja,Fillet ni zaidi ya steki sema siku hizi wajanja wamekua wengi,hasa sisi watu wa majikoni majikoni watu wananunua steki ya kawaida STEKI KABISA kisha ili kuilainisha bila viungo wanatumia kitchen hammer,nyama inapibwa pigwa mpk inakoma,ikitoka hapo ukiletewa unaweza hisi ni Fillet (kwa wasio na utaalamu wa fillet) ukala ukasema umekula fillet kumbe umelishwa steki ya kawaida tu.

Ni Hotel kubwa tu ndio wanaopika mishkaki ya fillet ambapo stick ya finyango 3 unauziwa 10,000 - 15,000, can you afford my brazaaaaa?!! if YES (go for it) ni tramu sanaaaaaaa...
 
Shukrani mkuu kwa maelezo yaliyo jitosheleza kabisa with aid of diagrams hapo naomba nikupe marks 95%, hiyo Fillet itabidi niicheki kwenye sehemu classic ama kwenye zile Nyama choma festival maana kwenye hizi hotel zetu za vichochoroni tunachojua ni kongoro tu[emoji23][emoji23][emoji23].

Na hizi ng'ombe tunazochinja kinyumbani nyumbani nahisi hiyo Fillet tunachanganya tuu humo humo na steki zingine tunachojua ni kutenga maini, moyo na utumbo. Unavyozungumza huo ulaini wa hiyo Fillet linakuja wazo ni kama mapupu vile[emoji23][emoji23][emoji23]
 
mapupu nayaona na kuyasikia tu ila ki ukweli sijuagi hata yana taste

gani mdomoni,kuna vitu siwezi weka mdomon kwangu ujue mkuu 🤣
 
Sausage.

Ni mbayaaaaa
 
Mrenda kwakweli ulinishinda
Nya ya mamba japoo tamu ila nikivua picha alivyo mbaya inakata stimu
 
Ugali wa udaga wa mwanza nilipata shida Sana kumeza na nilikuwa ugenini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…