Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Supu ya pweza! Aisee sitakuja kuijaribu Tena.
 
Sijui hata ilikuaje lakini mimi nikila dagaa au yai la kuchemsha nitatapika balaa
Dagaaa hata Mimi Wana nisumbua, wale wa mwanza, kigoma,
Lakini nimejaribu wa ziwa nyasa hawanipi shida
 
Nilikunywa supu ya pweza 2012 ila ghafla kichwa kikaanza kuuma, mwili unaisha nguvu, tumbo linaunguruma, jasho linanitoka na kuanza kutapika,

Mpaka leo nikimuona pweza napita kushoto.
Alikuwa kaharibika huyo
 
Chakula kinategemea na upikwaji wake.

Hata huo wali maharage kuna mpishi akiupika hauwezi kuula.
Uko sahihi Daby; chakula kinategemea upikwaji wake. Ukila kwa mara ya kwanza chakula kilichopikwa vibaya, hutakaa ule tena chakula hicho ukijua daima ni kibaya.
 
Pizza na Supu ya pweza aisee hapana jaribu tena
 
Siku moja ilikuwa nitie aibu nilikula mlenda ule wa asili sijui unachanganywa na nini
aisee niliona nikichafua seble ya watu bahati Mwili ulijireverse ile hali ikapotea
japo sipendagi kushindwa , hata makongoro siku ya kwanza ilikuwa hovyoo but sipendi kushindwa vyakula nimekomaa mpaka nimevizoea japo mlenda naula kwa spidi gavana na kwa tahadhari ya kutosha
 
Hahahahaha..ww na mimi hatuna utofauti
Siwez kula wadudu aisee, kuanzia senene,kumbikumbi na mdudu anaitwa pweza..


Kweli kabisa mkuu mimi huwa nawaambia watu siwezi kula mdudu aisee😀wapenda kumbikumbi na senene wanabaki kunishangaa!
 
Back
Top Bottom