Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Beef lasagne hii menyu ikoje Mkuu
images.jpeg
hii hapa boss
 
1.KAHAWA

kuna jamaa zangu wengi hupenda kweli kahawa,namimi ki ukweli napenda sana ile harufu yake tena nikiona na zile kashata huwa natamani kweli,siku 1 namimi nikasema haiwezekan kila siku nile harufu,Akapta muuza kahawa "nikamuita" kwa kujiamini kama vile member kbsa, akaja nkamwambia "weka kahawa hapa bwana mkubwa" Akanimiminia.

akanipa na kashata zake nikachukua 1,nikatia mdomoni mdomoni "bwana weeee" ilikua chungu hiyooooo haimezeki yani bahati yangu ilivyokua mbaya nilikaa sehemu ambayo hamna hata pakutemea.kote kulikua na tyrese tena nyeupee,asee nilijitahd kunywa ile kahawa ila sikuweza pga hata pafu lingine,muda huo nakunywa kashata yangu mkononi "nishaimaliza mudaaa" ila kakikombe ka kahawa kamejaa full,wenzangu washaongeza round mbili mi npo tu.

nikawa natafuta namna ya kutoka pale nisogee pembeni nikaimwage ie kahawa,ikabd nitege Alarm ya dk 3 nikakaa simu ikaita nikajifanya nimepokea nkainuka nikasogea kwenye mchanga nkamwagilia mbali kahawa lao.
 
2.AL KASUSU

kama kawaida mimi n mzee wa kutamani,kapita mjuba na Thermos yake anauza alkasusu,mwanangu mmoja akamuita akamwambia hebu niwekeee,akatoa vikombe amaizing "nikavipenda kweli" akam miminia jamaa alkasusu,jamaa akaonja,akawa anatngisha kichwa kumwambia yule mjuba muuza alkasuusu kuwa ile alkasusu ya siku ile n tamu sana sana sana.

sasa wakati jamaa anakunywa nikawa naskia harufu ya alkasusu,bwana wee n nzuri hiyooo,nikasema namimi aaah naptwaje bana Ngoja namimi niite niwekewe,jamaa akaja akaniwekea alkasusu yangu.Kutia mdomoni tu heeeee kitu mbayaaaaa haina sukari haina utamu ki ukweli nilijitahd sana sana kumaliza ila ilikua kama nakunywa Dawa.Nilijuta sana.
 
3.KONGORO

natamanigi sana nikiona mtu anakula kongoro anahangaika na bomba lile,huku akpga kijiko cha supu,nahisi anakula kitu kitamu sana,siku moja isiyo na jina namimi nikaitsha kongoro,wapendwa hamna siku hela yangu iliniuma kiasi kwamba nikatamani kulia kama ile siku,maana ki ukweli lile kongoro ile nimeweka mdomoni tu nilirudsha chenchi,ikabd nisingizie naumwa,nikatoka eneo lile nikabadlisha kiwanja nikarudi kwenye supu zetu za ng'ombe.
 
Back
Top Bottom