Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Kisusio nilionja nikiwa Arusha, sina hamu tena
Mimi pia imenishinda.
First day nilihisi vimaini sijui mapupu.

Nilikuwa na njaa nikavamia.

Halooo nilitema.

Na sijaonja tena mpaka leo.
 
Mambo vipi wanaJF natumai mko poa. Kwenye misosi kuna kuwa na kile chakula una hamu nacho au tu umekuta sehemu kimepikwa kwasababu hujawahi kula unaamua kula huo msosi kwa mara ya kwanza lakini chakula hicho kina kushinda kabisa hata kukupelekea kujisikia vibaya.

Mimi miaka ya nyuma nilikuwa nasikiaga kuhusu supu ya kongoro siku na mimi nikaamua nijue ikovipi hiyo supu nikaenda sehemu nzuri tu nikaulizia nikaambiwa ipo basi nikaletewa pale nikaanza kuipiga lakini kidogo tu nilikula kama vipande viwili tu vya ile nyama nikajisikia kuchefuchefu vibaya sana hata hiyo nyama kumeza haimezeki nikaacha supu karibia yote pale hadi leo hii sitaki tena kusikia kuhusu hiyo supu

Nyingine hii ilikuwa ni juisi ile ya rozela nilikuta imetengenezwa sehemu nikanywa glasi moja ilikuwa na ladha nzuri tu lakini baada ya hapo nilijisikia vibaya sana kama kizunguzungu mara kama mwili unataka ku vibrate mara jasho linatoka japo kulikuwa na feni yaani ilikuwa ni shida mpaka leo nikiiona hiyo juisi naipitia mbali kabisa. Hata juisi ya miwa ilinishinda kabisa ni bora nile muwa kama muwa

Vipi kwa upande wenu wadau ni kitu gani ulikula lakini baada ya hapo hutaki tena kukila.
Mimi mrenda ni kitu nisichopana nacho
Cookie (Chakula flani cha wacameroon) ukiitazama unaweza dhani ni cake ya birthday lakini taste yake siyo
Ugali wa wa magimbi (nacho chakula cha wacameroon) unavutia machoni ila ladha yake sikuipenda
 
Loshorwa..
Tulienda Moshi kwao na wife,nikapewa hyo kitu..nilipiga vijiko viwili tu nkashindwa endelea yaan
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Kabichi ni tamu sana basi tu wengi hawajui kupika.

Nilikua nachukia Kabichi ila sasa natamani kila leo nilile.

Kabichi + wali nazi +maharage nazi + nyama ya kukaanga. Weeeeeee
Kula kabichi na wali tu achana na hivyo vikorombwezo vingne uone cha mtema kuni"
 
Back
Top Bottom