Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Utumbo me mwenyewe sili. Wauza butcher wa Arusha wana ustaarabu m'baya sana, ukinunua nyama wanamix na utumbo eti. Me nawaambiaga ni heri uniwekee kilo pungufu kuliko kunichanganyia na hayo mautopolo
Aisee;wanafanya vibaya sana,Utumbo na nyama wapi na wapi!??

Kwahiyo ni karibia mabutcher yote!??

Mpaka leo sijui ni nani aliyeanzisha kula utumbo wakati nyama ipo.!!
 
Jinsia yako tafadhali? Ndizi haina ladha!!! Tambi pia, hii kali
Mwanaume .Sijawahi kwanza kuona kwetu nilipozaliwa wamepika tambi au ndizi Kama chakula.Siyapendi hayo matakataka .
 
Aisee;wanafanya vibaya sana,Utumbo na nyama wapi na wapi!??

Kwahiyo ni karibia mabutcher yote!??

Mpaka leo sijui ni nani aliyeanzisha kula utumbo wakati nyama ipo.!!
Ni asilimia karibu 99.99 za wauza mabutcher sijui huko machinjioni hali ipoje... Huwa nawamind wanabaki kuniuliza kwani dada umetokea mkoa gani? Nawaambia mikoa yote niliyopita nyama inauzwa kivyake, na utumbo kivyake hizi mixing ndiyo nimezikuta Arusha kwenu.
 
Siwezi kula dagaa wa mwanza kama hawana nyanya chungu/ bamia. Na hapo nivipike mwenyewe, mama au mdogo wangu na sio nikute kwa ndugu sijui jirani naonaga kama hawajui kupika ile mixing😛
Siku ukipika mwenyewe fanya kunikaribisha basi,maana umenitamanisha,huku kwa Malkia hivyo vitu ni nadra sana.
 
Chapati za maji (kumimina) mbona hazina shida. We mshamba wa wapi.
We mshamba kweli!
Haha me naona watu wengi hapa kinachowazingua ni upishi. Chakula kitakuwa kizuri kama kimepata mpishi haswaa ukitoa vile vyakula vya kukereka na harufu mfano: utumbo, fenesi nk

Me nilikula machalari kwa mmasai mmoja hivi aisee ile kitu sikuipenda, upishi ulikuwa mbovu nikaichukia. Sasa siku ya siku nikakutana na restaurant moja hivi imepika machalari imetuliaa, tamu kinyama thoe mwanzoni rafiki angu alinilazimisha kuitaste kuwa machalari yao nzuri, after tasting nikanogewa
 
Tikiti maji limenishinda. Hata harufu yake siwezi kuvumilia.
 
Nilikunywa supu ya pweza 2012 ila ghafla kichwa kikaanza kuuma, mwili unaisha nguvu, tumbo linaunguruma, jasho linanitoka na kuanza kutapika,

Mpaka leo nikimuona pweza napita kushoto.
Aiiiii pweza.... Nampendaaa.... Sipendi kumla kwa soup tu
 
Back
Top Bottom