Chakula kipi una mzio nacho au haupendi kula kabisa

Chakula kipi una mzio nacho au haupendi kula kabisa

Duuh yoghurt ndo kinywaji changu pendwa!!!! Soda nikinywa hua nasikia kama kulewa fulani.


Ila ndizi mbichi au zilizochomwa zimenishinda kabisaaa..hata upikeje. Sili
Viazi mviringo ile harufu daah
Duuh mkuu vitu vitamu ndo hauli kabisa.
 
Habari za Usiku wakuu..

Aisee mimi chakula ambacho sina allergy nacho ila kiukweli Hata upike Vipi Hauwezi kula kabisa kwa Upande wangu mimi ni BAMIA NA NYANYA CHUNGU..Vyovyote utakapopika mimi sitaweza kula na sijajua sababu ni ipi..


Je ni chakula Gani Hauwezi kula kabisa na wala kuonja kabisa !!?
Jamani hata mimi hizi ishu sijawahi tia mdomoni..sijui mlenda..sijui bamia.sijui biringanya. Sijui nyanya chungu sijui kisamvu yelewiii🤧🤧🤧
 
Bamia, nyanyachungu, kunde,choroko,[SUB]njugumawe,biringanya,mmlenda,big no[/SUB]
 
  • Mshangao
Reactions: BAK
Karibu vyote vilivyotajwa, nakula bila shida, viungwe kwa mchuzi au vichomwe/ kubanika, ninakula tu.
 
Magimbi na kambare,nikila hivi nakua kama nimemeza doxycillin baada ya kama nusu saa toka kula mwili unakua unachemka napatwa na maumivu ya kichwa kwa mbali then mwisho wa yote natapika involuntarily ndio mwili unakaa sawa.
 
daah mimi sijaona ambacho hakipandi!! najaribu kutafuta kwenye diary yangu sijaona mpaka sasa
 
Nakula kila kitu...namaanisha kila kitu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Maziwa ya kuganda ndio yenye kuniletea taabu lakini haya packed hayaniumizi. Soda zinaniumiza na kunipanua mishipa ya kichwa, kulewa na kukosa isingizi.

Irish potatoes ndio chakula changu cha kwanza kisha wali pia ndizi. Ndizi mbivu kwa siku nakula 15.
Hata Mimi soda hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom