Chalamila: Huwezi kukwepa kelele Dar es Salaam

Chalamila: Huwezi kukwepa kelele Dar es Salaam

NEMC wanapambana kuzuia unnecessary Makelele yeye ndo kwanza anahamasisha. Mgema akisifiwa Tembo hulitia Maji.
RC uwe makini wanaolalamika wakiona unajibu jeuri watajichukulia sheria mkononi..Sijui kuna shida gani kufuata sheria za nchi..Unamwambiaje mtu ahame kwenye nchi yake???
 
Sheria nyingi za mazingira zilizopo ni copy paste ya za ulaya, Sasa sisi na ulaya wap na wap.
Upo Sawa kabisa kwamba sheria zifuatwe, lakini swali ambalo halijibiwi hawa watu walitunga vip sheria zisizotekelezeka?
hivi wewe unaona sawa kupigiwa makelele usiku kucha halafu useme sheria haitekelezeki?

hakuna sheria ya copy paste ya ulaya ni ujinga wetu sisi tusilalamike tuendelee tu na vurugu zetu.

Leo ni makelele lakini kesho itakuwa jirani yako anatiririsha maji machafu mbele ya nyumba yako na utaendelea kunyamaza tu.
 
Je, wanapotunga sheria wanatushirikisha?au wanatunga kutukandamiza m naamini hakuna sheria imewekwa kumnufaisha mwananchi bali kutukandamiza kwasababu hakuna maoni ya wananchi bali ni maoni yao na kwa maslahi yao
 
Walevi ni wengi na wanachangia Pato la Taifa.

Kama serikali inataka kuondoka na utegemezi wa vileo katika mapato yake izibe mianya ya upotevu katika vyanzo vingine.

Sio inashindana na walevi halafu bado inawategemea.
 
Je, wanapotunga sheria wanatushirikisha?au wanatunga kutukandamiza m naamini hakuna sheria imewekwa kumnufaisha mwananchi bali kutukandamiza kwasababu hakuna maoni ya wananchi bali ni maoni yao na kwa maslahi yao
we huna mbunge? Ulitaka wananchi wote tuende bungeni kutunga sheria? Sheria ikipita tumeshirikishwa maana yupo mwakilishi wako kule anategemewa kutoa ushauri na mawazo yake kwa niaba yako
 
Kama kasema hivyo kakosea sana kwa sababu inakuwaje starehe yake na walevi wenzake iwe kero kwa watu wengine wanaoishi maeneo jirani bila kujali kama kuna wagonjwa,watoto,wazee na hata wakati mwingine hutokea dharura ya misiba lakini wote hao wateseke eti tu kwa vile kuna washenzi wachache wanakunywa pombe!
Halafu kama yeye anapenda sana kulewa ndio anatakiwa arudi kwao huko akanywe ulanzi atakavyo sio kuwaambia wenye mji wao eti wahame,halafu nilikuwa namsapoti sana Rais lakini tayari ameanza kunitoka kabisa naona kile kilevi kiitwacho madaraka kimemzidi kwa sababu hata kilichomshawishi kumleta Dar sijui ni kipi au sijui kuja kuhamasisha ulevi na mikelele!
 
RC uwe makini wanaolalamika wakiona unajibu jeuri watajichukulia sheria mkononi..Sijui kuna shida gani kufuata sheria za nchi..Unamwambiaje mtu ahame kwenye nchi yake???
Mimi namshangaa mteuzi sijui katumia kigezo gani hadi kumteua huyu jamaa kuwa RC Dsm,huyu na Makonda hawana tofauti wao wapo kimaslahi zaidi huku wakitumia vitisho kulazimisha watu wafuate wanachokitaka.
 
Sasa watu wa Dar nimepata RC, Nemc mkopo?

========

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaomba Wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo huku akiongezeka kuwa Jiji la Dar es Salaam haliwezi kukwepa kelele wala kukwepa starehe.

Akiongea wakati wa Swahili Comedy Show iliyofanyika Swahili Exprience, Coco Beach Dar es salaam, amesema “Kikubwa Mimi kama RC naahidi kutoa ushirikiano wa kiulinzi lakini zaidi kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo kwasababu maana na tafsiri ya kelele bado ni jambo ambalo ni gumu kidogo, adhana ikipiga asubuhi asiye Muislamu atasema hizo ni kelele"

"Vyombo vya Kanisani vikipiga kwa nguvu asiye Mkristo atasema ni kelele, miziki ya Baa ikipigwa Mtu ambaye sio mnywa pombe atasema ni kelele, kwahiyo kuna mahali panahitaji busara kuhusu tafsiri sahihi ya kelele ili Muislamu, Mkristo wapate haki zao, mnywa pombe apate haki yake na asiye imani apate haki yake, kikubwa Dar es salaam huwezi kukwepa kilele, huwezi kwepa starehe"

 
Back
Top Bottom