Chalamila: Huwezi kukwepa kelele Dar es Salaam

Chalamila: Huwezi kukwepa kelele Dar es Salaam

Huyu jamaa commedian sanaa .... kuna clip anasema kwa wenza ukisikia mwenzio anaimba "....mtarimbo huo mtarimbo huoo ...mtarimbo umelala doro.." ujue una la kesi
 
Watanzania sisi ni wajinga sana. Hawa wanaoteuliwa kuwa viongozi ni mbwiga kabisa.

Hakuna alienyimwa kunywa beer kwa kelele. Kinachotakiwa ni kuwa hizo kelele zisisumbue walio nje ya hapo unapokunywa beer zako.

Yaani kama uko club mziki haukatazwi ila mziki usitoke ukawasumbua walio nje ya club.

What part of that don't you understand niggas?
 
Nyie walokole kama hampendi bia waacheni wanaozinywa wazinywe, kama ni kelele mbona mjini kila kitu kinapiga kelele, hata watoto wenu nyumbani wakilia nao wanapiga kelele pia.
Kuna viwango vya kelele vilivyowekwa na Nemc kisheria, ni vyema mzingatie hili.
 
Hivi NEMC ina msomi mmoja tu kwamba akiamka na kukurupuka akiwaza kitu fulani ni uchafuzi wa mazingira basi wote wanaona ni sawa? Mfano ni hii approach yao ya kipuuzi ya kufungia mabaa eti yanapiga muziki kwa makelele! Mabaa yanafungiwa bila critical thinking matokeo yake amri zao zinapuuzwa na wasomi wenzao na wameanza kuyafungua. NEMC wakapambane na jukumu lao hasa la uharibifu wa mazingira. Mazingira ya ardhini, majini na anga, ukataji miti hovyo, usafi wa mazingira, madampo ya kiholela, utupaji taka za sumu, uchafuzi wa maji na hewa. Waachane na kelele za buruduni na kelele za shangwe na burudani wataonekana ni wendawazimu. Ni kama wamedandia gari kwa mbele, kupanda mtumbwi wa vimbwengo. Kelele za shangwe na ibada ni mfupa mgumu NEMC haitaweza kuutafuna
 
Kelele hazina ukomo, kunong'ona nako ni kelele tu inayoweza kumkera mwingine. Walitaka kuingilia kelele za ibada wakanyea wakaishia kutoa kibano kwenye mabaa nako wakakanyaga moto wa gesi. Approch yao kuhusu kelele imegonga mwamba warudi wakajipange upya kupambana na uchafuzi wa mazingira
 
Sema viongozi wetu bana Sheria wanapitisha wenyewe zikianza kutekelezwa wanakuja mbio mbio kuzuia. Tukichekea huu uhuni wa viongozi kugomea Sheria/ kanuni ipo siku li mtu litakatalia madarakani na hamtakua na chakulifanya.

Hata akina kagame, museveni, Mugabe n.k msifikiri waliruka tu mpaka kubadili katiba/sheria no!
Excellent point.

Hitler baada ya kushinda uchaguzi wa kidemokrasia kwa kishindo 1933, alichekewa hivi hivi na mamilioni ya Wajerumani akapitisha miswada kibao bungeni kubadili katiba ya kidemokrasia ya Ujerumani kujipa madaraka makubwa akidai ni muhimu ili kuimarisha taifa nyakati hizo za migogoro mingi ya kimataifa.

Hawajakaa sawa akajaza watu wake kwenye taasisi zote muhimu za nchi pamoja na majeshi yote. Kisha akajitangaza mtawala mkuu (führer) wa Ujerumani na kutawala kama absolute dictator hadi kifo chake akiacha Ujerumani hoi zaidi ikigawanywa na kutawaliwa na US/Europe upande wa Magharibi na USSR upande wa Mashariki.

Ndio hasara ya kuchekea watu waovu.
 
Back
Top Bottom