Chalamila: Nasisitiza nikifa nizikwe kama waislamu siyo kiislamu. Tunafanya misiba ya kifahari baada ya miezi 2 watoto wanafukuzwa ada

Chalamila: Nasisitiza nikifa nizikwe kama waislamu siyo kiislamu. Tunafanya misiba ya kifahari baada ya miezi 2 watoto wanafukuzwa ada

Karibuni kwenye uislamu hii ni dini simple sana, watu mnacimplicate maisha bure tu.
Uislamu sio tu kazika hata harusi zetu ni simple tu.
Ni msikitini pekee unaweza kukuta raisi wa nchi anasali safu moja na walala hoi hakuna special reserved seats kwa mheshimiwa yeyote msikitini.
Umeongea kweli nimekumbuka siku moja nilipita Kariakoo kusali ijumaa ghafla nikasikia honi na magari kumbe raisi mwinyi alikuja kusali.
Alikuta safu za mbele zimejaa walitaka kumpisha akakataa tukawa naye line ya nyuma
Jambo hili lilinigusa sana.
Hapa kazini kwangu bahati tuna msikiti ndani.Siku moja manager mkuu sio mtanzania alichelewa kuja kusali maana kamsikiti ketu kadogo hakika alisalia nje sisi wafanyakazi tuko ndani.
Jambo hili lilinifanya nizidi kuupenda uslam.
Uislam sio dini ya kinafiki kabisa
ila tahadhari sijataja dini nyingine hapa kulinganisha na wala hii sio comment ya kidini mapovu mwiko.
Dini zingine naziheshimu pia
 
Ukifa sisi ndo tutaamua msiba wako uweje, saa hiyo huo ukuu wa mkoa huna, hata kumove kidole huwezi achilia mbali kufumbua macho.

Tutatumia hela zako kushughukikia msiba wako, tena si ni wa nyanda za juu kusini wewe.
Msiba kama sherehe kwa pesa ulizoacha.
 
Wakuu,


"Nikifa nizikwe kama Waislamu siyo nizikwe Kiislam, miaka ya leo tumekuwa na misiba yenye mbwembwe nyingi sana bajeti ya mamilioni zinakwenda kuupa ufahari msiba lakini baada ya wiki mbili au miezi mitatu kama ni baba na mama waliowaacha watoto msiba unakuwa ni mzuri na wakifahari halafu baada ya miezi miwili mitatu watoto walioachwa wakiwa yatima wanaanza kufukuzwa ada.

Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es asalaam kwenye hafla ya kutoa misaada kituo cha watoto yatima UMRA Kinondoni.
Huwa namkubali sana huyu jamaa.
Huwa anausema ukweli bila kumng'unya maneno.
Kufa ni ile hali ya kuwa kama hukuwahi kuwepo.
Kwa maneno mengine, aliyekufa, hajui chochote.
Hivyo mbwembwe zote ambazo huwa zinafanyika, ni kuonesha tu ufahari kwa waliobaki na wala si kwa aliyekufa.
 
Ninaweza kumuunga mkono kwa uwezo wake wa kifikra ana hoja nzuri lakini ningekuwa mimi hili jambo lilikuwa halina haja ya kuja public keti na familia yako wape misingi kama hiyo katika msiba wako siku ukifa hakuna atakayekataa lakini kuja mbele za watu na kuzungumza ushuzi kama ule haileti maana yoyote
Hukumwelewa.
Yeye ni kiongozi wa Mkoa anayemwakilisha Rais na wala si kiongozi wa familia yake pekee.
Hivyo anawajibika kutoa ushauri kwa watu wake.
Suala la kuuchukua ushauri au kuuacha ni juu ya washauriwa.

(Vinginevyo, hata suala la kuhudhuria kwenye hicho kituo cha watoto yatima, asingeenda na hicho kituo chenyewe hakikupaswa kuwepo kwa sababu hata hao watoto wanatoka kwenye familia zao kwa mtizamo wako! Au siyo?)
 
Akaandike wosia kwa familia yake akifa azikwe kama waislam. Kigogo kama huyo akifa atakuwa ni maiti isiyoweza kusema izikweje, atazikwa kwa heshima zote familia yake itakavyoona ni vema ikishirikiana na serikali na chama chake. Wanaweza wakamjengea kaburi la kifahari na kumuweka kwenye sanduku la bei ghali na kumuhifadhi kwenye kaburi lisilowekwa udongo na kujengewa kisha kuwekwa zege juu na kuwekwa vigae/marumaru ghali lipendeze. Kisha watu watakula na kunywa kana kwamba ni sherehe ya kifahari
 
HAKUNA UCHAWA HAPO, HIYO NI FACT AMBAYO WAISLAM PEKEE WANAIFAHAM....
Amesema hivi, watu wanafanya misiba ya kifahari na baada ya msiba familia iliyobaki hata kama ilikuwa na watoto wadogo wanatelekezwa. Badala ya kutumia mahela meeengi kwenye msiba afahadhali hizo fedha zipewe familia/watoto wake kama wapo (kama Waislam wanavyo wapa familia hela zilizo changwa kwenye msiba).
Watu wana chuki hadi ukweli na point hawaioni. Unasababu gani ya kutumia mamilioni kwemye msiba halafu watoto wako baadae wanakosa hata hela ya ada?
Hata mimi natamani nizikwe simple, sio lazima sanduku la mamilioni,suti ya mamilioni, msafara wa kubeba mwili una magari kibao ya kukodi ili iweje na nishakufa
 
Anajuaje...atazikwa mamilioni ? Ilè michango watu sio za marehemu....sasa kusema eti watoto watafukuzwa ada....havina uhusiano....wekeza sasa ajili watoto wako...period
 
Kwani Ukristu unazuia mtu kuzikwa saa hiyo hiyo aliyokufa, au ni maamuzi tu ya wanafamilia?
Yeye hana haja ya kuwaambia watu wengine hadharani, awaambie tu wanafamilia wake au aandike wosia, naamini watauheshimu. Hata serikali huwa inasikia kwanza ratiba ya familia. Awaambie tu wanafamilia kuwa hata akifa kifo chenye utata asicheleweshwe, azikwe saa hiyo hiyo, naamini watamtii, hawatasubiri uchunguzi wa polisi
Lazima awaambie watuhadharani, Yeye ni kiongozi na ndio maana ya kiongozi, kilicho chema Kwa manufaa ya Raia lazima uwaambie.

We unafikiri yeyey anashida yoyote? Ameyaona haya Kwa watu anaowaongoza na ni matatizo yanayoikumba jamii, kwa hiyo kaamua kufikisha ujumbe Kwa style hiyo, na kasema wazi kabisa..

Lakini izo mbwembwe zipo Mjini tu, Sisi huku vijijini majeneza yenyewe tumeanza kuyajua hivi karibuni.... Mh. Kumbe hakutakiwa kusema kama waisilamu, alitakiwa aseme kama vijijini.
 
Lazima awaambie watuhadharani, Yeye ni kiongozi na ndio maana ya kiongozi, kilicho chema Kwa manufaa ya Raia lazima uwaambie.

We unafikiri yeyey anashida yoyote? Ameyaona haya Kwa watu anaowaongoza na ni matatizo yanayoikumba jamii, kwa hiyo kaamua kufikisha ujumbe Kwa style hiyo, na kasema wazi kabisa..

Lakini izo mbwembwe zipo Mjini tu, Sisi huku vijijini majeneza yenyewe tumeanza kuyajua hivi karibuni.... Mh. Kumbe hakutakiwa kusema kama waisilamu, alitakiwa aseme kama vijijini.
Angekuwa ana mamlaka ya kuwapangia watu, angekuwa sahihi maana yangekuwa ni maelekezo ya kiongozi kwa anaowaongoza.

Sasa hapo hatoi maelekezo maana hayo mamlaka hana. Hapo anajizungumzia msiba wake yeye binafsi akifa. Sasa sisi tunahusikaje na mazishi yake? Akifa huyo, wewe una uwezo wa kwenda kuilazimisha familia yake imzike leo leo kama alivyosema? Kama hauna uwezo wa kuilazimisha familia yake, huo ujumbe wake una faida gani kwa wasio wanafamilua wake?

Haya, ikitokea amekutwa barabarani amekufa, utailazimisha Polisi isifanye uchunguzi wa mwili kisa eti alisema azikwe haraka haraka?
 
Kumbe Uislamu mnaokubali japo mnaishi kiunafiki
Kwenye kuzika mmenyooka mkuu, ila inapokuja suala la kitimoto, ushungi, jihad na story nyingine za Mudy hapo mnazua tafrani kubwa sana.
 
Karibuni kwenye uislamu hii ni dini simple sana, watu mnacimplicate maisha bure tu.
Uislamu sio tu kazika hata harusi zetu ni simple tu.
Ni msikitini pekee unaweza kukuta raisi wa nchi anasali safu moja na walala hoi hakuna special reserved seats kwa mheshimiwa yeyote msikitini.

Kumbe Uislamu mnaokubali japo mnaishi kiunafiki
Kufanya mazishi au harusi "simple and inexpensive" ni maamuzi ya wahusika, si kanisa wala msikiti. Kuna waislam wanalisha nyomi kwenye harusi na misiba mpaka wanafunga barabara.
Nimeshuhudia classmate wangu kwao wana uwezo mkubwa tu lakini kafunga ndoa ya saa 12 asubuhi.
Ni maamuzi binafsi.
 
Naona sijui anapalilia kibarua, au Nitoke vipi kwenye media. Hii ilikua ni suala lake na Familia yake
 
Huyu anafanya uchawa kwa Samia hana lolote ,

Uzikwe na sanda,uzikwe kwenye sanduku, uzikwe uchi kama hukujiandaa na Mungu wako haisaidii kitu

Huyu anasema hivo ili Samia asimtumbue
Hoja yake ipo kwenye gharama zisizo za lazima ili kuepuka watoto kufukuzwa shule kukosa ada na mifano ya namna hiyo.

Hapa Chalamila yuko sahihi 100%
 
Hoja yake ipo kwenye gharama zisizo za lazima ili kuepuka watoto kufukuzwa shule kukosa ada na mifano ya namna hiyo.

Hapa Chalamila yuko sahihi 100%
Muongo Mzee,chalamila humjui Mzee , kwamba kuzikwa kwenye jeneza kunazuia vipi watoto kufukuzwa shule?

Chalamila anacheza game ya kujipendekeza kwa Samia
 
Huyu kuna kitu ameshtuka.
Kauli yake ya kwanza alisema anataka akifa azikwe kiisilamu. Kama kawaida Roman Catholic wakainote down hiyo kauli maana huwa hawapendi kujihusisha kwenye mazishi ya mtu ambaye imani yake katika Kanisa imeondoka waziwazi (kwa kutamka, kuishi wawili bila ndoa, kujiua, kufia maeneo yanayoashiria uwepo wa matendo mabaya).

Sasa hivi amekuja na kauli mpya kwamba azikwe kama waisilamu na sio kiisilamu.

Ngoja msubiri picha siku atakapokufa kweli, bila kitubio Roman Catholic huwa hawaangalii sura ya mtu. Aulizwe Ngombale Mwiru, Ruge Mutahaba na Bilionea wa Arusha
Naomba kukuuliza, hayo uliyoyasema kuhusu kanisa katoliki, NI mafundisho ya moja kwa moja ya biblia? Au ni matashi ya kanisa?

Hoja yangu hapa NI KWAMBA, tunatakiwa kufuata mafundisho ya biblia au mafundisho ya kanisa?
 
Akifa huyo, wewe una uwezo wa kwenda kuilazimisha familia yake imzike leo leo kama alivyosema? Kama hauna uwezo wa kuilazimisha familia yake, huo ujumbe wake una faida gani kwa wasio wanafamilua wake?

Mi kwangu nimeelewa kama ni ushauri hususani Kwa jamii inayomzunguka... Na hajatoa maelekezo Kwa jamii. Na hajazuia maana Kun Wenye uwezo wa kufanya hayo na maisha yakaendelea vizuri tu..

Nb:
Kikubwa watu waache kujiingiza kwenye gharama zisizo za msingi .. sasa Brother fikiria mtu anaingia mkopo bank tu Kwa ajili Harusi, inaleta afya kweli?

Mfano Mwamba Mmoja Mahakamani Juzi kama umesikia kwenye vyombo vya habari " Bwana Harusi feki"...
 
Back
Top Bottom