Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeongea kweli nimekumbuka siku moja nilipita Kariakoo kusali ijumaa ghafla nikasikia honi na magari kumbe raisi mwinyi alikuja kusali.Karibuni kwenye uislamu hii ni dini simple sana, watu mnacimplicate maisha bure tu.
Uislamu sio tu kazika hata harusi zetu ni simple tu.
Ni msikitini pekee unaweza kukuta raisi wa nchi anasali safu moja na walala hoi hakuna special reserved seats kwa mheshimiwa yeyote msikitini.
Huwa namkubali sana huyu jamaa.Wakuu,
"Nikifa nizikwe kama Waislamu siyo nizikwe Kiislam, miaka ya leo tumekuwa na misiba yenye mbwembwe nyingi sana bajeti ya mamilioni zinakwenda kuupa ufahari msiba lakini baada ya wiki mbili au miezi mitatu kama ni baba na mama waliowaacha watoto msiba unakuwa ni mzuri na wakifahari halafu baada ya miezi miwili mitatu watoto walioachwa wakiwa yatima wanaanza kufukuzwa ada.
Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es asalaam kwenye hafla ya kutoa misaada kituo cha watoto yatima UMRA Kinondoni.
Hukumwelewa.Ninaweza kumuunga mkono kwa uwezo wake wa kifikra ana hoja nzuri lakini ningekuwa mimi hili jambo lilikuwa halina haja ya kuja public keti na familia yako wape misingi kama hiyo katika msiba wako siku ukifa hakuna atakayekataa lakini kuja mbele za watu na kuzungumza ushuzi kama ule haileti maana yoyote
Watu wana chuki hadi ukweli na point hawaioni. Unasababu gani ya kutumia mamilioni kwemye msiba halafu watoto wako baadae wanakosa hata hela ya ada?HAKUNA UCHAWA HAPO, HIYO NI FACT AMBAYO WAISLAM PEKEE WANAIFAHAM....
Amesema hivi, watu wanafanya misiba ya kifahari na baada ya msiba familia iliyobaki hata kama ilikuwa na watoto wadogo wanatelekezwa. Badala ya kutumia mahela meeengi kwenye msiba afahadhali hizo fedha zipewe familia/watoto wake kama wapo (kama Waislam wanavyo wapa familia hela zilizo changwa kwenye msiba).
Lazima awaambie watuhadharani, Yeye ni kiongozi na ndio maana ya kiongozi, kilicho chema Kwa manufaa ya Raia lazima uwaambie.Kwani Ukristu unazuia mtu kuzikwa saa hiyo hiyo aliyokufa, au ni maamuzi tu ya wanafamilia?
Yeye hana haja ya kuwaambia watu wengine hadharani, awaambie tu wanafamilia wake au aandike wosia, naamini watauheshimu. Hata serikali huwa inasikia kwanza ratiba ya familia. Awaambie tu wanafamilia kuwa hata akifa kifo chenye utata asicheleweshwe, azikwe saa hiyo hiyo, naamini watamtii, hawatasubiri uchunguzi wa polisi
Angekuwa ana mamlaka ya kuwapangia watu, angekuwa sahihi maana yangekuwa ni maelekezo ya kiongozi kwa anaowaongoza.Lazima awaambie watuhadharani, Yeye ni kiongozi na ndio maana ya kiongozi, kilicho chema Kwa manufaa ya Raia lazima uwaambie.
We unafikiri yeyey anashida yoyote? Ameyaona haya Kwa watu anaowaongoza na ni matatizo yanayoikumba jamii, kwa hiyo kaamua kufikisha ujumbe Kwa style hiyo, na kasema wazi kabisa..
Lakini izo mbwembwe zipo Mjini tu, Sisi huku vijijini majeneza yenyewe tumeanza kuyajua hivi karibuni.... Mh. Kumbe hakutakiwa kusema kama waisilamu, alitakiwa aseme kama vijijini.
Kwenye kuzika mmenyooka mkuu, ila inapokuja suala la kitimoto, ushungi, jihad na story nyingine za Mudy hapo mnazua tafrani kubwa sana.Kumbe Uislamu mnaokubali japo mnaishi kiunafiki
Karibuni kwenye uislamu hii ni dini simple sana, watu mnacimplicate maisha bure tu.
Uislamu sio tu kazika hata harusi zetu ni simple tu.
Ni msikitini pekee unaweza kukuta raisi wa nchi anasali safu moja na walala hoi hakuna special reserved seats kwa mheshimiwa yeyote msikitini.
Kufanya mazishi au harusi "simple and inexpensive" ni maamuzi ya wahusika, si kanisa wala msikiti. Kuna waislam wanalisha nyomi kwenye harusi na misiba mpaka wanafunga barabara.Kumbe Uislamu mnaokubali japo mnaishi kiunafiki
Hoja yake ipo kwenye gharama zisizo za lazima ili kuepuka watoto kufukuzwa shule kukosa ada na mifano ya namna hiyo.Huyu anafanya uchawa kwa Samia hana lolote ,
Uzikwe na sanda,uzikwe kwenye sanduku, uzikwe uchi kama hukujiandaa na Mungu wako haisaidii kitu
Huyu anasema hivo ili Samia asimtumbue
Muongo Mzee,chalamila humjui Mzee , kwamba kuzikwa kwenye jeneza kunazuia vipi watoto kufukuzwa shule?Hoja yake ipo kwenye gharama zisizo za lazima ili kuepuka watoto kufukuzwa shule kukosa ada na mifano ya namna hiyo.
Hapa Chalamila yuko sahihi 100%
Naomba kukuuliza, hayo uliyoyasema kuhusu kanisa katoliki, NI mafundisho ya moja kwa moja ya biblia? Au ni matashi ya kanisa?Huyu kuna kitu ameshtuka.
Kauli yake ya kwanza alisema anataka akifa azikwe kiisilamu. Kama kawaida Roman Catholic wakainote down hiyo kauli maana huwa hawapendi kujihusisha kwenye mazishi ya mtu ambaye imani yake katika Kanisa imeondoka waziwazi (kwa kutamka, kuishi wawili bila ndoa, kujiua, kufia maeneo yanayoashiria uwepo wa matendo mabaya).
Sasa hivi amekuja na kauli mpya kwamba azikwe kama waisilamu na sio kiisilamu.
Ngoja msubiri picha siku atakapokufa kweli, bila kitubio Roman Catholic huwa hawaangalii sura ya mtu. Aulizwe Ngombale Mwiru, Ruge Mutahaba na Bilionea wa Arusha
Akifa huyo, wewe una uwezo wa kwenda kuilazimisha familia yake imzike leo leo kama alivyosema? Kama hauna uwezo wa kuilazimisha familia yake, huo ujumbe wake una faida gani kwa wasio wanafamilua wake?