Chalamila: Nasisitiza nikifa nizikwe kama waislamu siyo kiislamu. Tunafanya misiba ya kifahari baada ya miezi 2 watoto wanafukuzwa ada

Chalamila: Nasisitiza nikifa nizikwe kama waislamu siyo kiislamu. Tunafanya misiba ya kifahari baada ya miezi 2 watoto wanafukuzwa ada

Kwa mara ya kwanza jamaa namsikia anaongea point.
 
Naamini kuna vitu vingi ambavyo uisilamu unakataza lakini baadhi ya waumini wake wanavitaka. Alikufa jirani yetu muisilamu hapa, akatolewa hospitali na kuzikwa juu kwa juu, sisi tukaletewa tu taarifa kuwa jamaa ameshakufa na ameshazikwa huko huko siku hiyo hiyo. Watu wengi wakiwemo waisilamu walisikitika kwa kukosa fursa ya 'kumuaga' marehemu.
Hakuna hata umuhimu sana wa kumuaga marehemu.
 
Wakuu,

"Nikifa nizikwe kama Waislamu siyo nizikwe Kiislam, miaka ya leo tumekuwa na misiba yenye mbwembwe nyingi sana bajeti ya mamilioni zinakwenda kuupa ufahari msiba lakini baada ya wiki mbili au miezi mitatu kama ni baba na mama waliowaacha watoto msiba unakuwa ni mzuri na wakifahari halafu baada ya miezi miwili mitatu watoto walioachwa wakiwa yatima wanaanza kufukuzwa ada.

Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es asalaam kwenye hafla ya kutoa misaada kituo cha watoto yatima UMRA Kinondoni.
Fallacy
 
Hakuna hata umuhimu sana wa kumuaga marehemu.
Kama hakuna umuhimu, anachoomba ni kitu gani? Na wale waisilamu wanawake wanaoenda kanisani na makaburini katika mazishi ya jirani zao wakristu, kwa nini wanafanya hivyo?
 
Wakuu,

"Nikifa nizikwe kama Waislamu siyo nizikwe Kiislam, miaka ya leo tumekuwa na misiba yenye mbwembwe nyingi sana bajeti ya mamilioni zinakwenda kuupa ufahari msiba lakini baada ya wiki mbili au miezi mitatu kama ni baba na mama waliowaacha watoto msiba unakuwa ni mzuri na wakifahari halafu baada ya miezi miwili mitatu watoto walioachwa wakiwa yatima wanaanza kufukuzwa ada.

Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es asalaam kwenye hafla ya kutoa misaada kituo cha watoto yatima UMRA Kinondoni.
Fact
 
Kasema anakufa lini?

Maana ajira zimekua ngumu, ni sogea nipande.
 
Huyu anafanya uchawa kwa Samia hana lolote ,

Uzikwe na sanda,uzikwe kwenye sanduku, uzikwe uchi kama hukujiandaa na Mungu wako haisaidii kitu

Huyu anasema hivo ili Samia asimtumbue
Umeona mbali sana
 
Huyu anafanya uchawa kwa Samia hana lolote ,

Uzikwe na sanda,uzikwe kwenye sanduku, uzikwe uchi kama hukujiandaa na Mungu wako haisaidii kitu

Huyu anasema hivo ili Samia asimtumbue
We nawe umekurupuka hujamuelewa ,msikilize tena
 
Huyu kuna kitu ameshtuka.
Kauli yake ya kwanza alisema anataka akifa azikwe kiisilamu. Kama kawaida Roman Catholic wakainote down hiyo kauli maana huwa hawapendi kujihusisha kwenye mazishi ya mtu ambaye imani yake katika Kanisa imeondoka waziwazi (kwa kutamka, kuishi wawili bila ndoa, kujiua, kufia maeneo yanayoashiria uwepo wa matendo mabaya).

Sasa hivi amekuja na kauli mpya kwamba azikwe kama waisilamu na sio kiisilamu.

Ngoja msubiri picha siku atakapokufa kweli, bila kitubio Roman Catholic huwa hawaangalii sura ya mtu. Aulizwe Ngombale Mwiru, Ruge Mutahaba na Bilionea wa Arusha
Kitubio chenyewe eti cha kwenda kutubu kwa padre ambaye naye anakula wake za waumini wake kimya kimya, ushenzi mtupu mnawafurahisha wanadamu tu hapo.
 
Kitubio chenyewe eti cha kwenda kutubu kwa padre ambaye naye anakula wake za waumini wake kimya kimya, ushenzi mtupu mnawafurahisha wanadamu tu hapo.
Imeandikwa, lazima utamke kujuta dhambi zako. Hata wanaotoa ushuhuda, hao pia hutoa dhambi zako hadharani mbele ya washirikina, wazinzi na wezi wenzao
 
Point ya msingi hujalazimishwa kitu mkuu mtu anaweza akasikiliza na kuendelea na maisha yake, sasa makasiriko ya nini?
Yaani utumie rasilimali za serikali kutoa wosia wako? Tatizo hamjitambui
 
Karibuni kwenye uislamu hii ni dini simple sana, watu mnacimplicate maisha bure tu.
Uislamu sio tu kazika hata harusi zetu ni simple tu.
Ni msikitini pekee unaweza kukuta raisi wa nchi anasali safu moja na walala hoi hakuna special reserved seats kwa mheshimiwa yeyote msikitini.
Mkuu nani kakudanganya harusi ni simple? Au ni uhaba wa pesa tu.
 
Back
Top Bottom