Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Oystebay, leo Septemba 4, 2023.
CHALAMILA: SIJAONA RAIS UKIELEKEZA UKATOLIKI AU ULUTHERANI WA MTU KUFANYA MAMBO UNAYOYATAKA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema “Sijawahi kuona Rais ukielekeza Ukatoliki wetu au Ulutherani wa mtu mwingine kufanya mambo ambayo unayataka, ungesimama na kuanza kutuelekeza tungekuwa tumepoteza mwelekeo.
Kama kuna mtu yeyote atasimama kukuelekeza wewe na Serikali yako kufanya vitu ambavyo wanataka iwe hivyo, naomba usimame na unyooshe kamba kwa kuwa utapimwa kwa matokeo.
Simama katika mstari, hatuko tayari kuona Rais ukitukanwa na kurushiwa mawe, Polisi wameimba wakikuvaa tutawavaa, na mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar naahidi wakikuvaa nitawavaa.
Rais Samia anazungumzaRais Samia amepongeza jeshi la polisi kwa kupunguza uhalifu nchini, amewaomba kuimarisha dhana ya ulinzi shirikishi, wananchi wawe huru kufanya shughuli zao bila hofu ya kuvamiwa na majambazi.
Kumbe huyu naye ni chawa!