Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Ukiwa na bima ya CHF hupati huduma kwenye hospital za rufaa za mikoa wala wilaya. Hizo ni siasa tu
 
Sisi wapenda Haki. Bure ni dhambi. Kitu chochote lazima ugharamike. Hiyo ni Moja.
Ndio maana Mungu Mkuu tunayemuabudu licha ya kuwa sio mhitaji lakini anatutaka tukienda kwake tusiende Mikono mitupu.
Kwa Sisi Watibeli, huo ni Wehu

Ubaya wa viongozi wetu unatokana na kushindwa kuwajenga watu wawe na minute ya kujitegemea(falsafa ya Nyerere)

Ingawaje Sera ya Elimu inataka watu wakimaliza shule waweze kuwa na uwezo wa kujitegemea. Ukishakuwa na uwezo wa kujitegemea huwezipendelea mambo ya burebure
Nikuache tu, tutabishana mpaka asubuhi, bure ni dhambi kivipi, bure ipi, serikali kutoa elimu bure si dhambi na hiyo haiitwi bure, gesi ni ya tanzania, kodi kila mmoja anachangia kwanini iwe dhambi, jukumu la serikali ni lipi, iwe dhambi kwa afya na elimu bure ila isiwe dhambi wao ambao wanatembelea gari ya milioni 400 ambapo mtanzania anakunywa maji bwawa moja na ng'ombe!??
Kwako bure ni nini!?
Serikali tumewapa mamlaka ya kusimamia/kutusimamia sisi katika mambo kadha wa kadha, serikali iboreshe standard ya maisha ya mtanzania, barabara nzuri zijengwe, umeme usambae tanzania kote na upatikane kwa bei nzuri(tuna vyanzo vizuri, uzalishwe kwa wingi, mwingine uuzwe kile kinachopatikana kimneemeshe kila mtanzania) afya ni jambo la msingi mnoo.

Niko tofauti na mtazamo wako, haiwezekani kiongozi ambae anatumia kodi ya mtanzania, gari la bure, umeme bure, maji bure, matibabu bure, anasomeshewa watoto bure, analipwa mshahara, posho lukuki kisha atoe kauli za kishenzi na kipuuzi kama hizo.
Kuna watu wana hali tete, kama hivyo nao waishi kwa mishahara yao. Kuna namna mambo mnayanangalia kwa namna tofauti.
 
Kwema Wakuu!

Chalamila hapa nitamtaja kama Mhusika bila kuhusisha cheo chake. Ni aina ha watu ambao hawana breki za kuongea na watu wa aina hii mara nyingi huongeaga UKWELI mchungu ambao wakati mwingine huweza kuwaacha watu mdomo wazi.

Chalamila kadiri unavyompa nafasi na Muda WA kuongea ndivyo anavyoweza Kuropoka mambo ambayo ni magumu. Kwa Sisi tunaojua watu aina yake hatuwapagi nafasi Sana ya kuongea au kuwauliza maswali Tata ambayo yatamfanya ajichie.

Chalamila ni kama Kina Tundu Lisu. Tofauti Yao ni Moja. Mmoja anajua kujenga hoja wakati mwingine hawezi kujenga hoja ila wote wanaweza kuwa wanasema ukweli uleule wa Jambo lilelile.

Wasema ukweli mara nyingi hawanaga Staha. Hiyo huwafanya kuitwa roporopo.

Tukirudi kwenye hoja ya Chalamila kuhusu Wajawazito. Yupo sahihi Kabisa

Serikali sio kama imeweza Kabisa lakini angalau inajaribu kujitahidi Kusaidia watu hasa watu wa chini ingawaje zipo changamoto za kiutendaji na kifedha.

Kuna Bima ya CHF kama sijakosea ambayo kwa mwaka ni elfu 40,
Mambo inayotibu Bima hii ni Magonjwa ya kawaida yote.
Ujauzito
Ultrasound
X-ray
Kujifungua na Upasuaji mdogo
N.k.

Hivi mtu unajua Kabisa unaenda kuzaa mtoto au umembebesha Mimba Binti au Mkeo. Kwa nini usiweke angalau kwa siku elfu Moja Miatano kwa siku kisha mwisho wa mwezi wa Kwanza wa Ile Mimba ukate Bima ya elfu 40 kwaajili ya kumsaidia Mkeo au huyo uliyempa Mimba

Au kama umetelekezwa, sio sababu ya kukosa Bima ya elfu 40 kwa Sababusiku hizi Fursa za uzalishaji na kujipatia kipato ni Haki Sawa baina ya Mwanaume na mwanamke. Nikimaanisha huna haja ya kumtegemea Mumeo au mwanaume wakati Fursa zimetolewa Sawa.

Kata Bima ya elfu 40 kwaajili yako kama mwanamke mjamzito.

Na sio kulialia kumtafutia mtu Lawama kwa Jambo linalokuhusu mwenyewe ambalo umerahisishiwa.

Mambo ya huruma huruma, burebure ndio yanaharibu jamii.

Tunajua nchi yetu ni Maskini na jamii zetu nyingi ni Maskini ndio maana serikali kwa sehemu nayo imerahisisha kwa upande wao. Sasa mwaka mzima ushindwe Kutafuta elfu 40 ulipie Bima ati utake serikali ikuhudumie. Huo kama sio Ukengemaji ni nini?

Chukua Bima ya 40 Kisha andaa pesa ya kujifungulia ya dharura na ya uzazi
Hayo ndio majukumu yenyewe. Pumbavu.

Tupo kwa ajili ya wengi wenye kuhitaji msaada wanaoustahili

Tupo hapa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Gloves 50000tsh ni gloves za mwanakondoo hizo
 
Serikali inakosea kutoa Elimu bure wakati ingepaswa itoe Elimu kwa gharama nafuu kwa kila Mtanzania

Hata elfu 10 Tu kwa Mwaka.
Kuendekeza Bure ni kulemaza hata wale waliokuwa na uwezo wa kupambana
 
Serikali ikupe BIMA hujatumia zaidi ya mwaka upewe na kula supu ya uzazi.

Kama daftari linamshinda mtu mwenye hali ya chini watoto wanasubili siku likipatikana ataandika mambo ya nyuma, mia tano mzazi anakosa kumpa mtoto pesa ya kula shule.

Hiyo elfu 40000 kwa mwaka inakuaje. Kaka Mtibeli unaujua UMASKINI ewwwwww.
 
Hela za sangoma hawakosi lakini
 
Serikali inakosea kutoa Elimu bure wakati ingepaswa itoe Elimu kwa gharama nafuu kwa kila Mtanzania

Hata elfu 10 Tu kwa Mwaka.
Kuendekeza Bure ni kulemaza hata wale waliokuwa na uwezo wa kupambana
Kwanza waboreshe standard ya maisha ya mbongo.

Kuna serikali duniani huko zinatoa elimu bure na sio bure tu ni bora pia ila mataifa yao ni wapambanaji na wana mabilionea wa kidunia.
Ajiulize kuna miaka elimu ilikuwa ya kulipia, je kipi kiliongezeka kwa mtanzania, kwamba ndio walikuwa na uchungu sana kiasi wakapambana wakawa na hela sana?

Achana na elimu bure, kuna mataifa mpaka afya ni bure lakini bado raia wake ni wapambanaji na wana maisha mazuri, wametuacha mbali mnoo, tusiwe na excuse zisizo na kichwa wala miguu.
Haya wafanye elimu ada ni laki kabisa unadhani ndio mtanzania atapigana zaidi na kuwa milionea.

La hasha kuna vitu havipo sawa nchini, na vinaanzia na serikali,
Hao Denmark, Australia, norway, Sweeden sio wenzetu, tunawafikia kwa kipi?
 
Serikali ikupe BIMA hujatumia zaidi ya mwaka upewe na kula supu ya uzazi.

Kama daftari linamshinda mtu mwenye hali ya chini watoto wanasubili siku likipatikana ataandika mambo ya nyuma, mia tano mzazi anakosa kumpa mtoto pesa ya kula shule.

Hiyo elfu 40000 kwa mwaka inakuaje. Kaka Mtibeli unaujua UMASKINI ewwwwww.
Kama ni masikini aliruhusuje kubeba mimba?
 
Huduma za uzazi hazipatikani mpaka uchangie kwa mwaka mmoja kama si miwili, kua na akili.
Hawa watoto wanaongea usengrema tu hawajui maisha.
Hawajui gwaride la maisha. Ukisikia nyuma geuka ...tajiri anakuwa masikini na masikini anakuwa tajiri. Wa kwanza anakuwa wa mwisho na wa mwisho anakuwa wa kwanza.

Ni masaa kadhaa tu unaweza kutoka kuwa na nyumba, magari na akiba bank kisha ukajikuta masikini huna 1000 tu ya kununua maji ya kunywa au chai. Tena una madeni juu.
Wanaongea kauli za mtu mwenye shibe ambae hajawahi kulala na njaa maamaeh Zhao.
Wana kauli za kishujaa sana hawa 'makocho'.

Wanaongea vitu bila kufuatilia undani wake. Hizo bima za hovyo tu, hupati huduma nyingi au nyingine hupati huduma nje ya eneo flani.
Wanawasikiliza wanasiasa walioshiba au wanao jipendekeza kwa mkuu wao.

Huyo Chalamila mwenyewe hazijui adha za hizo bima za 40K.
Leo nimechafukwa sana na hawa watoto.
 
Kuna watu wanaongoza kuroga kama matajiri

Matajiri wapo nyuma ya Maskini kwenye ulozi.

Maskini wanaloga hata wasiohusika.
Matajiri wao wanaenda kuloga kwa mambo Yao ili wafanikiwe Kupata pesa.

Maskini anaweza kwenda kumloga Mtibeli ati kisa kapost hapa😃
 
Back
Top Bottom