Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Kwema Wakuu!

Chalamila hapa nitamtaja kama Mhusika bila kuhusisha cheo chake. Ni aina ha watu ambao hawana breki za kuongea na watu wa aina hii mara nyingi huongeaga UKWELI mchungu ambao wakati mwingine huweza kuwaacha watu mdomo wazi.

Chalamila kadiri unavyompa nafasi na Muda WA kuongea ndivyo anavyoweza Kuropoka mambo ambayo ni magumu. Kwa Sisi tunaojua watu aina yake hatuwapagi nafasi Sana ya kuongea au kuwauliza maswali Tata ambayo yatamfanya ajichie.

Chalamila ni kama Kina Tundu Lisu. Tofauti Yao ni Moja. Mmoja anajua kujenga hoja wakati mwingine hawezi kujenga hoja ila wote wanaweza kuwa wanasema ukweli uleule wa Jambo lilelile.

Wasema ukweli mara nyingi hawanaga Staha. Hiyo huwafanya kuitwa roporopo.

Tukirudi kwenye hoja ya Chalamila kuhusu Wajawazito. Yupo sahihi Kabisa

Serikali sio kama imeweza Kabisa lakini angalau inajaribu kujitahidi Kusaidia watu hasa watu wa chini ingawaje zipo changamoto za kiutendaji na kifedha.

Kuna Bima ya CHF kama sijakosea ambayo kwa mwaka ni elfu 40,
Mambo inayotibu Bima hii ni Magonjwa ya kawaida yote.
Ujauzito
Ultrasound
X-ray
Kujifungua na Upasuaji mdogo
N.k.

Hivi mtu unajua Kabisa unaenda kuzaa mtoto au umembebesha Mimba Binti au Mkeo. Kwa nini usiweke angalau kwa siku elfu Moja Miatano kwa siku kisha mwisho wa mwezi wa Kwanza wa Ile Mimba ukate Bima ya elfu 40 kwaajili ya kumsaidia Mkeo au huyo uliyempa Mimba

Au kama umetelekezwa, sio sababu ya kukosa Bima ya elfu 40 kwa Sababusiku hizi Fursa za uzalishaji na kujipatia kipato ni Haki Sawa baina ya Mwanaume na mwanamke. Nikimaanisha huna haja ya kumtegemea Mumeo au mwanaume wakati Fursa zimetolewa Sawa.

Kata Bima ya elfu 40 kwaajili yako kama mwanamke mjamzito.

Na sio kulialia kumtafutia mtu Lawama kwa Jambo linalokuhusu mwenyewe ambalo umerahisishiwa.

Mambo ya huruma huruma, burebure ndio yanaharibu jamii.

Tunajua nchi yetu ni Maskini na jamii zetu nyingi ni Maskini ndio maana serikali kwa sehemu nayo imerahisisha kwa upande wao. Sasa mwaka mzima ushindwe Kutafuta elfu 40 ulipie Bima ati utake serikali ikuhudumie. Huo kama sio Ukengemaji ni nini?

Chukua Bima ya 40 Kisha andaa pesa ya kujifungulia ya dharura na ya uzazi
Hayo ndio majukumu yenyewe. Pumbavu.

Tupo kwa ajili ya wengi wenye kuhitaji msaada wanaoustahili

Tupo hapa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Naungana na Chalamila, ila kama hupiga cha Arusha apunguze.

Kwa hili ameongea ukweli , walio karibu naye mwambieni ipo lita kumi za wain toka Italy akitaka nimtumie
 
Nikuache tu, tutabishana mpaka asubuhi, bure ni dhambi kivipi, bure ipi, serikali kutoa elimu bure si dhambi na hiyo haiitwi bure, gesi ni ya tanzania, kodi kila mmoja anachangia kwanini iwe dhambi, jukumu la serikali ni lipi, iwe dhambi kwa afya na elimu bure ila isiwe dhambi wao ambao wanatembelea gari ya milioni 400 ambapo mtanzania anakunywa maji bwawa moja na ng'ombe!??
Kwako bure ni nini!?
Serikali tumewapa mamlaka ya kusimamia/kutusimamia sisi katika mambo kadha wa kadha, serikali iboreshe standard ya maisha ya mtanzania, barabara nzuri zijengwe, umeme usambae tanzania kote na upatikane kwa bei nzuri(tuna vyanzo vizuri, uzalishwe kwa wingi, mwingine uuzwe kile kinachopatikana kimneemeshe kila mtanzania) afya ni jambo la msingi mnoo.

Niko tofauti na mtazamo wako, haiwezekani kiongozi ambae anatumia kodi ya mtanzania, gari la bure, umeme bure, maji bure, matibabu bure, anasomeshewa watoto bure, analipwa mshahara, posho lukuki kisha atoe kauli za kishenzi na kipuuzi kama hizo.
Kuna watu wana hali tete, kama hivyo nao waishi kwa mishahara yao. Kuna namna mambo mnayanangalia kwa namna tofauti.
Serikali ina cha kuwajibika
Lakini ukiambiwa Bure sio ujue eti ni Bure kama Bure
Tukisema elimu Bure ina maana mwalimu, madarasa, vitabu n. K
Sio tena elimu Bure usizingatie vitu vidogo kama sare, mlo, vitabu, masomo ya ziada, nauli n. K
Ukisikia huduma ya uzazi ni Bure serikali inunue nepi, taulo, beseni, ndio, nyembe, gloves, mwanvuli, uji wa mama, n. K
 
Matajiri wapo nyuma ya Maskini kwenye ulozi.

Maskini wanaloga hata wasiohusika.
Matajiri wao wanaenda kuloga kwa mambo Yao ili wafanikiwe Kupata pesa.

Maskini anaweza kwenda kumloga Mtibeli ati kisa kapost hapa😃
Tuachane na hayo inakuaje gloves ziwe 50k?
 
Kwenye Bure kuna gharama ndio kama hizo za Chalamila
Ni gharama ndogo sana hazihusiani na bima, vitu kama beseni sijui alafu kuhakikisha vitu vya msingi vya kumpokea mtoto mf. nguo kama sehemu ya kuwakumbusha. Kama kutakuwa na complication atabebwa na ambulance kwenda hospital ya rufaa na atatibiwa bure kwa kuwa ameanzia chini ambapo ni bure.

Ila wale wanaokwenda directly hospitali ya rufaa wanahudumiwa ila zinawatoka hela au bima ya Afya hapa ndo inahusika zaidi
 
Sio gloves tu
Hapo Kuna nyembe
Beseni, ndogo, taulo, kanga vipande 3 na vitenge vipande 3, uji na mlo wa kwanza maalumu wa mzazi, n. K
Kwa hiyo beseni na uji na kanga unapewa na doctor hapo hosi kwenye hiyo 50k?
 
Kwani wewe umekua kwa daipers?
Sawa tuweke pampers pembeni kumbuka kuna sabuni na mafuta ya mtoto bila kusahau clinic ya mtoto na lishe bora hivi vyote vinahitaji hela bila kusahau mavazi ya mtoto.
 
Sawa tuweke pampers pembeni kumbuka kuna sabuni na mafuta ya mtoto bila kusahau clinic ya mtoto na lishe bora hivi vyote vinahitaji hela bila kusahau mavazi ya mtoto.
Wewe kwa kua ulikua kwa sabuni na uji wenye sukari unadhani watoto wote wanakua vivo hivyo?
 
Hii serikali nayo ndio imewazoesha mambo ya burebure ili Kupata sifa za kijinga.

Weka gharama reasonable lakini bure ni uamuzi usio Sahihi.

Kama hiyo elfu 40 iko reasonable
Haya, elimu nayo waweke Ada kila mtoto atoe Ada elfu 20 iende serikali kuu.
Waalimu Wapate mishahara, marupurupu na serikali isipate Mzigo kuchukua pesa kwenye sekta zingine

Kila sekta ijihakikishie inajitegemea kwa angalau asilimia 50
Tunakimbilia kuiga iga vitu ili kupata sifa kisiasa wakati uwezo huo hatuna ,haya ni matokeo ya kuwa na viongozi wenye akili ndogo kabisa
 
Kwema Wakuu!

Chalamila hapa nitamtaja kama Mhusika bila kuhusisha cheo chake. Ni aina ha watu ambao hawana breki za kuongea na watu wa aina hii mara nyingi huongeaga UKWELI mchungu ambao wakati mwingine huweza kuwaacha watu mdomo wazi.

Chalamila kadiri unavyompa nafasi na Muda WA kuongea ndivyo anavyoweza Kuropoka mambo ambayo ni magumu. Kwa Sisi tunaojua watu aina yake hatuwapagi nafasi Sana ya kuongea au kuwauliza maswali Tata ambayo yatamfanya ajichie.

Chalamila ni kama Kina Tundu Lisu. Tofauti Yao ni Moja. Mmoja anajua kujenga hoja wakati mwingine hawezi kujenga hoja ila wote wanaweza kuwa wanasema ukweli uleule wa Jambo lilelile.

Wasema ukweli mara nyingi hawanaga Staha. Hiyo huwafanya kuitwa roporopo.

Tukirudi kwenye hoja ya Chalamila kuhusu Wajawazito. Yupo sahihi Kabisa

Serikali sio kama imeweza Kabisa lakini angalau inajaribu kujitahidi Kusaidia watu hasa watu wa chini ingawaje zipo changamoto za kiutendaji na kifedha.

Kuna Bima ya CHF kama sijakosea ambayo kwa mwaka ni elfu 40,
Mambo inayotibu Bima hii ni Magonjwa ya kawaida yote.
Ujauzito
Ultrasound
X-ray
Kujifungua na Upasuaji mdogo
N.k.

Hivi mtu unajua Kabisa unaenda kuzaa mtoto au umembebesha Mimba Binti au Mkeo. Kwa nini usiweke angalau kwa siku elfu Moja Miatano kwa siku kisha mwisho wa mwezi wa Kwanza wa Ile Mimba ukate Bima ya elfu 40 kwaajili ya kumsaidia Mkeo au huyo uliyempa Mimba

Au kama umetelekezwa, sio sababu ya kukosa Bima ya elfu 40 kwa Sababusiku hizi Fursa za uzalishaji na kujipatia kipato ni Haki Sawa baina ya Mwanaume na mwanamke. Nikimaanisha huna haja ya kumtegemea Mumeo au mwanaume wakati Fursa zimetolewa Sawa.

Kata Bima ya elfu 40 kwaajili yako kama mwanamke mjamzito.

Na sio kulialia kumtafutia mtu Lawama kwa Jambo linalokuhusu mwenyewe ambalo umerahisishiwa.

Mambo ya huruma huruma, burebure ndio yanaharibu jamii.

Tunajua nchi yetu ni Maskini na jamii zetu nyingi ni Maskini ndio maana serikali kwa sehemu nayo imerahisisha kwa upande wao. Sasa mwaka mzima ushindwe Kutafuta elfu 40 ulipie Bima ati utake serikali ikuhudumie. Huo kama sio Ukengemaji ni nini?

Chukua Bima ya 40 Kisha andaa pesa ya kujifungulia ya dharura na ya uzazi
Hayo ndio majukumu yenyewe. Pumbavu.

Tupo kwa ajili ya wengi wenye kuhitaji msaada wanaoustahili

Tupo hapa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Screenshot_20250126-223325.jpg
Screenshot_20250126-223355.jpg
 
Swali: kwanini walifikiria kuweka bure?
Unazijua sababu za kuweka bure?
Je, Leo zimeisha hizo sababu?

Sababu zilikuwa zisizo na AKILI
Wangesema tuu gharama nafuu Kabisa

Huwezi kutoa bure alafu wewe ni nchi Maskini.

Kitendo cha kusema ni bure kinawabwetesha hata wale wenye uwezo wa Kutafuta pesa na kujihudumia
 
Back
Top Bottom