Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Serikali isikwepe jukumu lake.

Jamani tembeeni muone, kuna watu wana maisha magumu ukimwambia aitoe 40 kwa pamoja ni bora umpige kisu, HANA, kuna watu wana maisha magumu huko.
Mfano mzuri kuna ile video yule mzee anatembea na samaki akapewa 20k mpaka akatoa machozi ya shukrani, vijijini huko kuna wakina mama wanalipa vipande ama mraba 20 kwa 20 ama 10 kwa 10, hizo ni mita kwa elfu saba. Anaweza kumaliza siku 2 mpaka 3, sasa jiulize kazi ya elfu 7 amalize kwa siku 3 ama 2, kwa siku kaingiza kiasi gani, anakula kiasi gani, bajeti ya hospital kiasi gani, shule mtoto kiasi gani, umeme ama solar, ama mafuta ya taa, ama miahumaa kiasi gani, na hizo kazi ni za msimu

Serikali itoe hudumu muhimu ikiwezekana bure, elimu bure, afya bure inawezekana kabisa.. Mkuu wa wilaya, sijui nani nani wanatembelea gari za milioni 400 huko, je pesa hizo hazitoshi kuhudumia afya na elimu wilaya husika!?

Na huduma hizo zisiwe bure tu ila ziwe ni bora kabisa.
Kuna umuhimu wa serikali kurudisha kampeni ya uzazi wa mpango(nyota ya kijani) na kusisitiza uzazi wa mpango kwa raia.
 
Hii serikali nayo ndio imewazoesha mambo ya burebure ili Kupata sifa za kijinga.

Weka gharama reasonable lakini bure ni uamuzi usio Sahihi.

Kama hiyo elfu 40 iko reasonable
Haya, elimu nayo waweke Ada kila mtoto atoe Ada elfu 20 iende serikali kuu.
Waalimu Wapate mishahara, marupurupu na serikali isipate Mzigo kuchukua pesa kwenye sekta zingine

Kila sekta ijihakikishie inajitegemea kwa angalau asilimia 50
Hakuna kitu kinaitafuna serikali kama Elimu ya bure hadi fm 6,wanaona aibu tu kuifuta ila inawakosti billions of money kila mwezi kutoa ruzuku,hii kitu walikurupuka.
 
Mkuu ukienda hospital watu wanalia Sana. Gharama za Upasuaji serikali kwenye Mimba na kujifungua sio chini ya 150k Mpaka unatoka sio ajabu ukatoa 200k

Watu wengi wanalia wakati wangekuwa na Bima ingekuwa elfu 40 tuu
Hio bima ingekuwa ni bima kweli usingeona watu wakihangaika na huduma za afya.

Leo hii nenda hospitali yeyote ile unayoijua, fika pale useme una bima uone namna utakavyokuwa treated kama mbuzi. Kwanza mtapangishwa foleni na wahudumu hawajali kuhusu nyie. Unaweza shinda siku nzima uko hospitali kwa ajili ya huduma basic tu. Licha ya yote huwezi kuta vyote viki covered na bima. Kwa sasa bima imekuwa tiketi ya kumuona daktari tu, mengine lazma ulipie tu.
 
Hivi mnataka vitu vya bure alafu mtegemee vifaa hospitalini, logically imekaa Sawa hiyo.

Watanzania wangapi wanalipa Kodi? Au Ndio ninyi mnasema tukinunua vitu ndio tunalipa Kodi?

Watu watoe Kodi wapewe huduma.

Mbona hela za pombe zinapatikana?
Hivi unadhani shida ni kukusanya kodi au shida ni matumizi ya hizo kodi? Hebu fikiria ukoo wenu 70% labda ni diaspora wana miliki uchumi mzuri halafu 30% wako local apeche alolo. Wale 70% wakisema wachange hela ili kuwakomboa hao 30% kisha waliopewa dhamana miongoni mwao wakawa hawasaidii hawa 30% kwa makusudi unadhani wa kulaumiwa ni nani?

Same applies kwa serikali, its proven to lack integrity especially when it comes to revenues. Kila mwezi tunajinadi kukusanya trillion mbili ila mwisho wa kila mwaka unaskia imetoa 700 Billions kununua magari ya anasa. Land cruiser zimekuwa built to last at least 25 years ni gari ngumu na za gharama ila kila baada ya miaka mitatu zinanunuliwa upya. Achilia mbali hilo, kuna udokozi wa hatari kikundi kidogo kimegawana trillion huyu kachukua 500B yule 300B mwengine 100B wengine wamegawana 50B. Hizo ni kodi za wananchi na madeni ambayo watayalipa tu. Mbaya hao jamaa wakishatajwa kesi huwa zinaishia hewani. Nani atakuwa na moyo wa kulipa kodi katika mazingira hayo?
 
Hivi unadhani shida ni kukusanya kodi au shida ni matumizi ya hizo kodi? Hebu fikiria ukoo wenu 70% labda ni diaspora wana miliki uchumi mzuri halafu 30% wako local apeche alolo. Wale 70% wakisema wachange hela ili kuwakomboa hao 30% kisha waliopewa dhamana miongoni mwao wakawa hawasaidii hawa 30% kwa makusudi unadhani wa kulaumiwa ni nani?

Same applies kwa serikali, its proven to lack integrity especially when it comes to revenues. Kila mwezi tunajinadi kukusanya trillion mbili ila mwisho wa kila mwaka unaskia imetoa 700 Billions kununua magari ya anasa. Land cruiser zimekuwa built to last at least 25 years ni gari ngumu na za gharama ila kila baada ya miaka mitatu zinanunuliwa upya. Achilia mbali hilo, kuna udokozi wa hatari kikundi kidogo kimegawana trillion huyu kachukua 500B yule 300B mwengine 100B wengine wamegawana 50B. Hizo ni kodi za wananchi na madeni ambayo watayalipa tu. Mbaya hao jamaa wakishatajwa kesi huwa zinaishia hewani. Nani atakuwa na moyo wa kulipa kodi katika mazingira hayo?

Tukilipa Kodi wengi hapa tutakuwa na uchungu wa hii nchi.
Najua pesa ukitoa inavyouma.

Sema watoa Kodi ni Wachache hivyo serikali ni rahisi kuwadhibiti hata wakileta chokochoko.

Moja ya dalili ya sehemu kuna mafisadi ni wananchi wengi kutokulipa kodi
 
Tukilipa Kodi wengi hapa tutakuwa na uchungu wa hii nchi.
Najua pesa ukitoa inavyouma.

Sema watoa Kodi ni Wachache hivyo serikali ni rahisi kuwadhibiti hata wakileta chokochoko.

Moja ya dalili ya sehemu kuna mafisadi ni wananchi wengi kutokulipa kodi
Wengi tunalipa indirect tax. Wanaolipa direct tax ni wachache
 
MASKINI LEO WANABAGAZWA MBELE,NYUMA,JUU,KATIKATI.🤗🤣🤣🤣🤣🤣

MASKINI WANAJIENDEKEZA SANA HIVI KAMA UNAKOSA HATA ELFU HAMSINI UNAZAA ILI UGUNDUE NINI ZAIDI YA KUTAKA KUPATA LAANA BURE YA UZAO WAKO.

KAMA HATA ELFU HAMSINI HUNA BORA URUDI KIJIJINI UKALIME. MJINI HUKO DASLAM UNAISHIJE.NDIMAANA BIASHARA ZA UKAHABA,BAIKOKO WIZI NA UTAPELI ZIMETAMALAKI HUKO MIJINI.


CHALAMILA YUPO SAHIHI WATANZANIA WAJIFUNZE KUBEBA MAJUKUMU YAO.KAMA MTU HUWEZI MAJUKUMU SITISHA KWANZA.HAKUNA SIFA KATIKA KUTESEKA.
 
Robert Heriel Mtibeli
Huenda haujui Umasikini au umekuzwa katika mfumo wa mafanikio acha nikae kimya.
Kama wewe ni maskini hakuna haja ya kuzaliana tafuta kwanza unafuu wa maisha kwa kuweza kujihudumia wewe kwanza kisha ndo ufikiri kuleta kiumbe hapa duniani.

Hakuna justification kwa mtu asiye na uwezo wa kutunza mtoto,alete mtoto ambaye anauwezo wa kuzuia kwa kutumia CONDOM!!!
 
Kwema Wakuu!

Chalamila hapa nitamtaja kama Mhusika bila kuhusisha cheo chake. Ni aina ha watu ambao hawana breki za kuongea na watu wa aina hii mara nyingi huongeaga UKWELI mchungu ambao wakati mwingine huweza kuwaacha watu mdomo wazi.

Chalamila kadiri unavyompa nafasi na Muda WA kuongea ndivyo anavyoweza Kuropoka mambo ambayo ni magumu. Kwa Sisi tunaojua watu aina yake hatuwapagi nafasi Sana ya kuongea au kuwauliza maswali Tata ambayo yatamfanya ajichie.

Chalamila ni kama Kina Tundu Lisu. Tofauti Yao ni Moja. Mmoja anajua kujenga hoja wakati mwingine hawezi kujenga hoja ila wote wanaweza kuwa wanasema ukweli uleule wa Jambo lilelile.

Wasema ukweli mara nyingi hawanaga Staha. Hiyo huwafanya kuitwa roporopo.

Tukirudi kwenye hoja ya Chalamila kuhusu Wajawazito. Yupo sahihi Kabisa

Serikali sio kama imeweza Kabisa lakini angalau inajaribu kujitahidi Kusaidia watu hasa watu wa chini ingawaje zipo changamoto za kiutendaji na kifedha.

Kuna Bima ya CHF kama sijakosea ambayo kwa mwaka ni elfu 40,
Mambo inayotibu Bima hii ni Magonjwa ya kawaida yote.
Ujauzito
Ultrasound
X-ray
Kujifungua na Upasuaji mdogo
N.k.

Hivi mtu unajua Kabisa unaenda kuzaa mtoto au umembebesha Mimba Binti au Mkeo. Kwa nini usiweke angalau kwa siku elfu Moja Miatano kwa siku kisha mwisho wa mwezi wa Kwanza wa Ile Mimba ukate Bima ya elfu 40 kwaajili ya kumsaidia Mkeo au huyo uliyempa Mimba

Au kama umetelekezwa, sio sababu ya kukosa Bima ya elfu 40 kwa Sababusiku hizi Fursa za uzalishaji na kujipatia kipato ni Haki Sawa baina ya Mwanaume na mwanamke. Nikimaanisha huna haja ya kumtegemea Mumeo au mwanaume wakati Fursa zimetolewa Sawa.

Kata Bima ya elfu 40 kwaajili yako kama mwanamke mjamzito.

Na sio kulialia kumtafutia mtu Lawama kwa Jambo linalokuhusu mwenyewe ambalo umerahisishiwa.

Mambo ya huruma huruma, burebure ndio yanaharibu jamii.

Tunajua nchi yetu ni Maskini na jamii zetu nyingi ni Maskini ndio maana serikali kwa sehemu nayo imerahisisha kwa upande wao. Sasa mwaka mzima ushindwe Kutafuta elfu 40 ulipie Bima ati utake serikali ikuhudumie. Huo kama sio Ukengemaji ni nini?

Chukua Bima ya 40 Kisha andaa pesa ya kujifungulia ya dharura na ya uzazi
Hayo ndio majukumu yenyewe. Pumbavu.

Tupo kwa ajili ya wengi wenye kuhitaji msaada wanaoustahili

Tupo hapa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Naunga mkono hoja
 
Unataka kusema huwezi kupata 50,000/= Kwa miezi 8? Bwashe mimba siyo chafya
Hii nchi wajinga wanataka kujiona wana haki.Yaani mtu akabanjuke kwa mpango wake alafu anataka aje atusumbue kwenye majukumu ambayo ni matokeo ya starehe yake😁😁😁

Maskini waambiwe ukweli hakuna kitu wanachangia katika hii nchi zaidi ya kunyonya wengine.

Umaskini ndo unapelekea ukahaba,umachinga,udalali,mawinga,majambazi na vibaka,nk.Watu wangekuwa wanaoanga uzazi lawama zingekuwa chache na ajira zingetosha.
 
Back
Top Bottom