Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

MASKINI WEWE NENDA KAFANYE KAZI,ACHA KULIALIA HOVYO.KAMA HUNA HELA FUNGA KIZAZI!!!

SERIKALI INAMAMBO MENGI YA KUFANYA.
Huu ushauri mpelekee aliyekuzaa ili asiendelee kuzaa watoto wenye wajinga kama wewe!
 
Kwema Wakuu!

Chalamila hapa nitamtaja kama Mhusika bila kuhusisha cheo chake. Ni aina ha watu ambao hawana breki za kuongea na watu wa aina hii mara nyingi huongeaga UKWELI mchungu ambao wakati mwingine huweza kuwaacha watu mdomo wazi.

Chalamila kadiri unavyompa nafasi na Muda WA kuongea ndivyo anavyoweza Kuropoka mambo ambayo ni magumu. Kwa Sisi tunaojua watu aina yake hatuwapagi nafasi Sana ya kuongea au kuwauliza maswali Tata ambayo yatamfanya ajichie.

Chalamila ni kama Kina Tundu Lisu. Tofauti Yao ni Moja. Mmoja anajua kujenga hoja wakati mwingine hawezi kujenga hoja ila wote wanaweza kuwa wanasema ukweli uleule wa Jambo lilelile.

Wasema ukweli mara nyingi hawanaga Staha. Hiyo huwafanya kuitwa roporopo.

Tukirudi kwenye hoja ya Chalamila kuhusu Wajawazito. Yupo sahihi Kabisa

Serikali sio kama imeweza Kabisa lakini angalau inajaribu kujitahidi Kusaidia watu hasa watu wa chini ingawaje zipo changamoto za kiutendaji na kifedha.

Kuna Bima ya CHF kama sijakosea ambayo kwa mwaka ni elfu 40,
Mambo inayotibu Bima hii ni Magonjwa ya kawaida yote.
Ujauzito
Ultrasound
X-ray
Kujifungua na Upasuaji mdogo
N.k.

Hivi mtu unajua Kabisa unaenda kuzaa mtoto au umembebesha Mimba Binti au Mkeo. Kwa nini usiweke angalau kwa siku elfu Moja Miatano kwa siku kisha mwisho wa mwezi wa Kwanza wa Ile Mimba ukate Bima ya elfu 40 kwaajili ya kumsaidia Mkeo au huyo uliyempa Mimba

Au kama umetelekezwa, sio sababu ya kukosa Bima ya elfu 40 kwa Sababusiku hizi Fursa za uzalishaji na kujipatia kipato ni Haki Sawa baina ya Mwanaume na mwanamke. Nikimaanisha huna haja ya kumtegemea Mumeo au mwanaume wakati Fursa zimetolewa Sawa.

Kata Bima ya elfu 40 kwaajili yako kama mwanamke mjamzito.

Na sio kulialia kumtafutia mtu Lawama kwa Jambo linalokuhusu mwenyewe ambalo umerahisishiwa.

Mambo ya huruma huruma, burebure ndio yanaharibu jamii.

Tunajua nchi yetu ni Maskini na jamii zetu nyingi ni Maskini ndio maana serikali kwa sehemu nayo imerahisisha kwa upande wao. Sasa mwaka mzima ushindwe Kutafuta elfu 40 ulipie Bima ati utake serikali ikuhudumie. Huo kama sio Ukengemaji ni nini?

Chukua Bima ya 40 Kisha andaa pesa ya kujifungulia ya dharura na ya uzazi
Hayo ndio majukumu yenyewe. Pumbavu.

Tupo kwa ajili ya wengi wenye kuhitaji msaada wanaoustahili

Tupo hapa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
rubbish
 
Unaweza ukawa na bima lakini ukaendelea kuzungushwa pia
 
Acha kuadvertise radio na vipindi vya watu. Toa hoja yako ueleweke.
Nimemshangaa sana huyo bwege, yaani badala ya kutupa taarifa ya anachotaka kusema hata Kwa kutumia mfano Mmoja kuhusiana na hicho kipindi, yeye anatupa Tena assignment ya sisi kwenda kuitafuta hicho kipindi Chake kisha turudi hapa JF ndio tuelewe hoja yake.
 
Hao watu hawana hata ndugu, marafiki au wameshindwa kwenda hata ustawi wa jamii na mashirika mengine?
Akili huna kabisa, inaonekana una exposure ndogo sana ya maisha na hujaijua jamii nzima ya kitanzania in and out ikoje, na ndio maana unatoa majibu Rahisi rahisi bila kushirikisha ubongo hata kidogo.
 
Huyu RC aliwahi kusema kama huna uwezo wa kuvuka kigamboni piga mbizi
Ona Sasa halafu mpaka leo Bado ni RC?
Lakini sishangai sana maana Kuna Mmoja aliwahi kutuambia kama hatuwezi kulipa tozo tuhamie Burundi na mpaka leo hii bado ni waziri.

Hii nchi kuwatukana na kuwakosea heshima wanainchi sio kosa, kosa ni kumkosea heshima au kumtukana raisi tu.
 
Huduma kwa mama mjamzito ni bure, Serikali kama haiwezi iseme. Hadi huduma za mama na mtoto zinawashinda, aibu iliyoje.
Binafsi Mimi Sina tatizo na wagonjwa/wahudimiwa kuchangia kidogo gharama za matibabu, lakini je wanatakiwa wachangie Kwa wakati sahihi ambapo ni baada ya wao kupata huduma.

Kwanini wameweka utaratibu mbovu ni lazima utoe pesa kwanza ndio upate huduma? Kwanini wasimpe kwanza matibabu mgonjwa kisha ndio masuala ya malipo yafuatie baadae?
 
Acheni kujipa umuhimu fanyeni kazi hakuna mwananchi wa kawaida wala asiye wa kawaida.

Nyie maskini mnajiendekeza sana.Na mnadanganywa sana na wanasiasa.

📌📌📌Hii dunia hakuna cha bure,amka toka usingizini!!!
Mkuu naona unafanya attacks zisizo na msingi. Nani amekwambia me sifangi kazi au nashindwa hudumia familia yangu. Hapa siongelei umimi. Ninaongelea nafasi ya pili na ya tatu ambayo wewe na mimi tunajua, wapo watu wana changamoto kiuchumi.

Tunaposema Tanzania si maskini ni kweli Tanzania si maskini. Ila wananchi wake wengi ni maskini na sababu za umaskini zinachangiwa na factors mbalimbali. Sidhani kama kuna Mtanzania ambaye hafanyi kazi, ila anafanya kazi kulingana na nature ya mazingira aliyopo. Kipato ndo linayofautiana. kuja wanaopaya kikubwa na wanaopata kidogo, kutosha au kutotosha mlo wa siku. Sasa tusiwasemee au ndo tuwazodoe kisa sisi tunaoata kikubwa?

Tunaposema usimamizi wa rasilimali, nakupa mfano. Nchi za Kiarabu zenye mafuta je wao wanafanya kazi kutuzidi? Wao wamejua nanma bora ya kuhakikisha rasilimali mafuta inawanufaisha vizuri. Sisi gesi imetunufaisha kwa kiasi gani kiuchumi ukiachiloa mbali matumizi ya ndani ambayo bado jamii kubwa badoninashindwa hata nunua Mzungi wa gesi?

Nimehoji, mbona hela za kufanyia vitu visivyo vya msaada kwa MTZ zinapatikana mfano, matamasha, fulani, khanga na vitenge n.k then hela ya kununua vufaa muhimu vya hospital vinakosekana?

Nikuulize, ushawahi tibiwa au kuwa na jamaa yako ametibiwa hospital za serikari? Niambie hali ya usafi wodini, changamoto. Nenda vyooni, changamoto. Na hii ni kwa sababu hakuna vitendea kazi. Nenda shule za serikari nianbie kama wana vifaa vya kutosha vya kufundishia au watoto kunifunzia?

So unataka kuniambia kwamba wananchi sababu ni wazembe na maskini ndo maana hizi huduma zinakuwa hafifu?

We can still make this country a better place to live kama tutaondoa ubisnafsi na kuhakikisha tunakuwa na mikakati bora ya kulinda uchumi wetu hasa kwa kuhakikisha rasilimali zetu za asili zinasimamiwa vyema.
 
Akili huna kabisa, inaonekana una exposure ndogo sana ya maisha na hujaijua jamii nzima ya kitanzania in and out ikoje, na ndio maana unatoa majibu Rahisi rahisi bila kushirikisha ubongo hata kidogo.
Mkuu huku mtaani kwetu kuna vyama vidogo vidogo vya wamama ambao wanasaidiana endapo mwenzao kapatwa na tatizo sasa kama hakuwepo kwenye kikundi hata kimoja hilo ni tatizo lake. Halafu mtu kama ni masikini unaruhusuje kubeba mimba.
 
Mtibeli sio kila jambo ni la kuangalia Kwa jicho la ki-capitalist.

Kuna mambo mengine yanapaswa kuangaliwa Kwa angle ya uhalisia WA ya kimaisha ya walio wengi.

Wengi wanaoenda kutibiwa kwenye hospitals zetu hizi za government ni watu wenye vipato duni/maskini na sometimes unakuta mtu anaenda pale Hana akina yoyote mfukoni kwake.

Kwa hiyo kumwambia eti hili apate matibabu ni lazima atoe pesa kwanza ya vifaa huko ni sawa na kumwambia kama huna Hela ya kutulipa basi wewe kufa tu hakuna namna. Ni kauli Moja hivi ya kikatili sana.

Hata kama ni lazima tuchangie huduma Sasa ni kwanini mtu asipate matibabu kwanza halafu baadae ndio mje mumbane kwenye malipo? Tena mgonjwa mwenyewe ni mjazito ambaye wote tunajua ni jinsi Gani watu Hawa matibabu Yao yanapaswa kufanyika Kwa haraka.

Na pia hivi kweli hospital Gani inakosa mpaka gloves nazo pia mpaka mgonjwa alipie?
 
Ukikata hiyo ya 40, ndani ya wiki mbili inafanya Kazi.

Hivyo kama Mwanamke atagundua ni mjamzito ule mwezi wa Kwanza anaweza kukata kisha first trimester anaanza Kliniki Akiwa na Bima. Anakula Raha za Mimba bila stress za kuwaza itakuwaje
Bima ya elfu 40 ina cover kujifungua?
Tuwekee hapa sera za hiyo Bima mbona unaruka ruka tu huweki ushahidi?
 
hiyo bima inakidhana na sera ya afya(wizara)

kutibiwa bure kwa mama mjamzito ,watoto na wazee!!! au unazungumzia Voda bima ambayo Juzi nimesitisha wizi wao wa makato bila idhini yangu ya 7700 kila mwezi
 
Lakini ikija harusi anatafuta elfu hamsini ya mchango .. hiyo arubaini kwa ajili ya mkewe sio kipaumbele kwake
Hao unaowasema wanatoa mchango wa elfu 50, sio hao walioshindwa kulipa bima, tukubali hii nchi ina umaskini wa kutupa, tembeeni muone acheni kuangalia mambo kwenye maeneo yenu mnayoishi,
Nasisitiza tena ITEMBEENI NCHI YENU MJIONEE UMASKINI ULIOPO.
 
Bima ya elfu 40 ina cover kujifungua?
Tuwekee hapa sera za hiyo Bima mbona unaruka ruka tu huweki ushahidi?

Bima ya CHF inatumika zahanati, vituo vyote vya afya
Ingia Google CHF

Unataka ushahidi upi nimekuambia Jambo ambalo Mimi nalitumia.

Mimi wakati nakata CHF ni baada ya kukosa pesa ya ku-renew NHIF hivyo nilifungua CHF kidharura. Na nilitibiwa.
Ninayo hiyo kwa matumizi na wakati wa dharura kama ilivyonitokea awali
 
Kwema Wakuu!

Chalamila hapa nitamtaja kama Mhusika bila kuhusisha cheo chake. Ni aina ha watu ambao hawana breki za kuongea na watu wa aina hii mara nyingi huongeaga UKWELI mchungu ambao wakati mwingine huweza kuwaacha watu mdomo wazi.

Chalamila kadiri unavyompa nafasi na Muda WA kuongea ndivyo anavyoweza Kuropoka mambo ambayo ni magumu. Kwa Sisi tunaojua watu aina yake hatuwapagi nafasi Sana ya kuongea au kuwauliza maswali Tata ambayo yatamfanya ajichie.

Chalamila ni kama Kina Tundu Lisu. Tofauti Yao ni Moja. Mmoja anajua kujenga hoja wakati mwingine hawezi kujenga hoja ila wote wanaweza kuwa wanasema ukweli uleule wa Jambo lilelile.

Wasema ukweli mara nyingi hawanaga Staha. Hiyo huwafanya kuitwa roporopo.

Tukirudi kwenye hoja ya Chalamila kuhusu Wajawazito. Yupo sahihi Kabisa

Serikali sio kama imeweza Kabisa lakini angalau inajaribu kujitahidi Kusaidia watu hasa watu wa chini ingawaje zipo changamoto za kiutendaji na kifedha.

Kuna Bima ya CHF kama sijakosea ambayo kwa mwaka ni elfu 40,
Mambo inayotibu Bima hii ni Magonjwa ya kawaida yote.
Ujauzito
Ultrasound
X-ray
Kujifungua na Upasuaji mdogo
N.k.

Hivi mtu unajua Kabisa unaenda kuzaa mtoto au umembebesha Mimba Binti au Mkeo. Kwa nini usiweke angalau kwa siku elfu Moja Miatano kwa siku kisha mwisho wa mwezi wa Kwanza wa Ile Mimba ukate Bima ya elfu 40 kwaajili ya kumsaidia Mkeo au huyo uliyempa Mimba

Au kama umetelekezwa, sio sababu ya kukosa Bima ya elfu 40 kwa Sababusiku hizi Fursa za uzalishaji na kujipatia kipato ni Haki Sawa baina ya Mwanaume na mwanamke. Nikimaanisha huna haja ya kumtegemea Mumeo au mwanaume wakati Fursa zimetolewa Sawa.

Kata Bima ya elfu 40 kwaajili yako kama mwanamke mjamzito.

Na sio kulialia kumtafutia mtu Lawama kwa Jambo linalokuhusu mwenyewe ambalo umerahisishiwa.

Mambo ya huruma huruma, burebure ndio yanaharibu jamii.

Tunajua nchi yetu ni Maskini na jamii zetu nyingi ni Maskini ndio maana serikali kwa sehemu nayo imerahisisha kwa upande wao. Sasa mwaka mzima ushindwe Kutafuta elfu 40 ulipie Bima ati utake serikali ikuhudumie. Huo kama sio Ukengemaji ni nini?

Chukua Bima ya 40 Kisha andaa pesa ya kujifungulia ya dharura na ya uzazi
Hayo ndio majukumu yenyewe. Pumbavu.

Tupo kwa ajili ya wengi wenye kuhitaji msaada wanaoustahili

Tupo hapa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Watu wanapenda mitelezo sana ,wanataka hadi serikali impe hela ya nauli ya kwenda hospital ,magufuli alivyosema elimu bure wazazi wakataka hadi Uniform na madaftari wanunuliwe na Magufuli.

Kwenda kujifungua kuna maandalizi ya khanga,pamba ,gloves etc hizo anakuja nazo kutoka nyumbani hazitolewi na serikali ,Chalamila yupo sahihi....Unapofisikia kujifungua bure ni services ya hospitali kama wataalamu,umeme,kitanda etc na si gloves/pamba/khanga nazo unataka serikali ikununulie,mwisho wa siku utaomba hadi serikali ikulipie gharama za usafiri wa kukurudisha nyumbani.
 
Hao unaowasema wanatoa mchango wa elfu 50, sio hao walioshindwa kulipa bima, tukubali hii nchi ina umaskini wa kutupa, tembeeni muone acheni kuangalia mambo kwenye maeneo yenu mnayoishi,
Nasisitiza tena ITEMBEENI NCHI YENU MJIONEE UMASKINI ULIOPO.

Niambie wapi nitembee.
Umaskini upo ndio lakini sio wakukosa elfu arobaini
Mbona pesa za waganga wa jadi zinapatikana na ni ghali zaidi
 
Watu wanapenda mitelezo sana ,wanataka hadi serikali impe hela ya nauli ya kwenda hospital ,magufuli alivyosema elimu bure wazazi wakataka hadi Uniform na madaftari wanunuliwe na Magufuli.

Kwenda kujifungua kuna maandalizi ya khanga,pamba ,gloves etc hizo anakuja nazo kutoka nyumbani hazitolewi na serikali ,Chalamila yupo sahihi....Unapofisikia kujifungua bure ni services ya hospitali kama wataalamu,umeme,kitanda etc na si gloves/pamba/khanga nazo unataka serikali ikununulie,mwisho wa siku utaomba hadi serikali ikulipie gharama za usafiri wa kukurudisha nyumbani.

Sema serikali yenyewe ndio imewaendekeza watu wake.

Ndio maana inawanyanyasa. Watu wanapenda burebure wataachwaje kunyayaswa
 
Back
Top Bottom