Acheni kujipa umuhimu fanyeni kazi hakuna mwananchi wa kawaida wala asiye wa kawaida.
Nyie maskini mnajiendekeza sana.Na mnadanganywa sana na wanasiasa.
📌📌📌Hii dunia hakuna cha bure,amka toka usingizini!!!
Mkuu naona unafanya attacks zisizo na msingi. Nani amekwambia me sifangi kazi au nashindwa hudumia familia yangu. Hapa siongelei umimi. Ninaongelea nafasi ya pili na ya tatu ambayo wewe na mimi tunajua, wapo watu wana changamoto kiuchumi.
Tunaposema Tanzania si maskini ni kweli Tanzania si maskini. Ila wananchi wake wengi ni maskini na sababu za umaskini zinachangiwa na factors mbalimbali. Sidhani kama kuna Mtanzania ambaye hafanyi kazi, ila anafanya kazi kulingana na nature ya mazingira aliyopo. Kipato ndo linayofautiana. kuja wanaopaya kikubwa na wanaopata kidogo, kutosha au kutotosha mlo wa siku. Sasa tusiwasemee au ndo tuwazodoe kisa sisi tunaoata kikubwa?
Tunaposema usimamizi wa rasilimali, nakupa mfano. Nchi za Kiarabu zenye mafuta je wao wanafanya kazi kutuzidi? Wao wamejua nanma bora ya kuhakikisha rasilimali mafuta inawanufaisha vizuri. Sisi gesi imetunufaisha kwa kiasi gani kiuchumi ukiachiloa mbali matumizi ya ndani ambayo bado jamii kubwa badoninashindwa hata nunua Mzungi wa gesi?
Nimehoji, mbona hela za kufanyia vitu visivyo vya msaada kwa MTZ zinapatikana mfano, matamasha, fulani, khanga na vitenge n.k then hela ya kununua vufaa muhimu vya hospital vinakosekana?
Nikuulize, ushawahi tibiwa au kuwa na jamaa yako ametibiwa hospital za serikari? Niambie hali ya usafi wodini, changamoto. Nenda vyooni, changamoto. Na hii ni kwa sababu hakuna vitendea kazi. Nenda shule za serikari nianbie kama wana vifaa vya kutosha vya kufundishia au watoto kunifunzia?
So unataka kuniambia kwamba wananchi sababu ni wazembe na maskini ndo maana hizi huduma zinakuwa hafifu?
We can still make this country a better place to live kama tutaondoa ubisnafsi na kuhakikisha tunakuwa na mikakati bora ya kulinda uchumi wetu hasa kwa kuhakikisha rasilimali zetu za asili zinasimamiwa vyema.