Chalinze, Pwani: Rais Samia azindua mradi wa maji na kuzungumza na Wananchi

Baraka Mina

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2020
Posts
586
Reaction score
590
Kutoka Mlandizi, Chalinze - Mboga mkoani Pwani ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anazindua mradi wa maji na kuzungumza na wananchi leo tarehe 22 Machi 2022.



======

Rais Samia Suluhu Hassan amesema upatikanaji wa maji katika eneo la Chalinze haukuwa rahisi kwa sababu kulikuwa na mvutano mkali baina ya viongozi ambao uliolenga kujenga.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 22, 2022 mara baada ya kuzindua mradi wa maji Mlandizi Chalinze – Mboga ulioanza Julai 2019 na kukamilika Novemba 2021.

“Nakumbuka wakati wa kampeni tulipokuwa tunapita kuomba ridhaa ya wananchi kuongoza Serikali kupitia CCM, nilijionea mwenyewe changamoto za maji nchi nzima ikiwemo mkoani Pwani, hasa hapa Chalinze baada ya kampeni nilikuja kwa tukio jingine.

“Ndiyo hiyo siku nilimuona mwanangu Ridhiwan akifoka moto mdomoni unatoka akimfokea Injinia Luhemeja kwamba usipoleta maji hapa nakushtaki kwa wananchi lakini leo nimeshuhudia kila mmoja kamuomba radhi mwenzake kwa matamshi makali lakini maji yamepatikana Chalinze leo tunavyofurahia safari ilikuwa ndefu na ngumu,” amesema Rais Samia.

Amesema Serikali imeipa upekee mkubwa mkoa wa Pwani na maeneo mengine kwa kuwa ina dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani.

Rais Samia amewaagiza Dawasa kuhakikisha wanakamilisha mradi huo na miradi mingine ukiwemo wa awamu ya tatu unaotekelezwa kwa Sh100 milioni ambao umefikia asilimia 90.

“Nimeambiwa kwamba mradi huu unatoa lita milioni 9.3 kwa siku na utawafikia wakazi 120,912 kwa siku, kukamilika kwake kutaongeza hali ya upatikanaji wa maji katika mkoa kufikia asilimia 79 na Ilani ya CCM ni asilimia 85, Pwani ni mkoa wa viwanda tunakwenda kuzidi asilimia 85 na kwa takwimu zilizotolewa tukifikia mwaka 2025 tutafikia asilimia 100 kupata maji safi na salama,” amesema Rais Samia.
 
KATIBA MPYA ni MHIMU sana, mliopo karibu na Rais chonde chonde mpeni hiyo taarifa.

Tanzania inahitaji katiba mpya
 
Muungwana ni vitendo, kila atendaye mema anastahiri malipo mema pia.

Mama yetu/Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amejitahidi na anaendelea kujitahidi kuyafanya Yale ambayo watanzania tulitamani kuona yakifanyika.

Leo Mh Rais atakuwepo Pale Chalinze mkoa wa Pwani kuendelea na majukumu yake kama rais wa jamhuri ya muungano was Tanzania.

RAIS atakuwa chalimze leo tarehe 22/03/2022 kuzindua rasmi majengo ya halmashauri ya Chalinze, mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya TSHS 13 Bilioni na mengineyo mengi.

Kazi kwenu wakazi wa Chalinze na vitongoji vyake, jitokezeni kwa wingi kumpokea mheshimiwa rais na ugeni wake atakaoambatana nao.

Wakusanyikapo tai hapo ndipo penye mzoga.

Je ziara ya mheshimiwa rais Samia Chalinze, wana Chalinze mnategemea mema gani tofauti na Yale yaliyobainishwa?

Karibu Chalinze mheshimiwa Rais, karibu Chalinze mama yetu Samia Suluhu Hassan.
Baada ya muhamad kukaririshwa Qur'an pangoni na kupewa utumr na mke wake.

Kuishi mjini kunahitaji nguvu kidogo halafu akili mingi.

Hapa hatupo kwenye ushindani wa kidini ila nimeleta hii mada ili tuijadili kuhusu swali langu la msingi nililouliza mdau na wewe ungetoa Maoni yako kuliko kuhusu vitu ambavyo havipo mbona mada imejieleza vizuri inakuaje wewe unashindwa kuielewa?
 
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Mlandizi, Chalinze - Mboga mkoani Pwani ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anazindua mradi wa maji na kuzungumza na wananchi leo tarehe 22 Machi 2022.


Hii ni mbinu ya kwenye kwa JK
 
Back
Top Bottom