Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...!

Status
Not open for further replies.
Sipati picha itakuwaje na tufanye nini iwapo CCM na IKULU itathibitika kuwa ndo wapangaji wa mauaji na utesaji wa watu ambao wanawaona kama kikwazo kwao kama vile Dr. Steven Ulimboka, Absalom Kibanda na David Mwangosi!!.

Mimi nadhani CCM na mawakala wake kama kina Tendwa na wenzake akili zao za kuua nguvu ya kisiasa ya CDM na wale wote wanaowaunga mkono ziko ukingoni.........na mtu anapofikia kikomo cha kufikiri katika kukabiliana na matatizo yake binafsi, ni wazi huweza kuchukua maamuzi ya ovyo na hata pengine kutwaa maisha yake (kujiua) mwenyewe!!!

Hii ni ndo kusema kuwa hawa watu yaani CCM na SERIKALI chini ya yao wako katika ukomo wao wa kufikiri na kutenda!!. Kwao CDM ni adui wa maslahi wa matumbo na ulaji wao....hawaichukulii CDM kama changamoto kwao ili watende vyema zaidi....SO, NO ONE CAN BE SUPRISED IF THEY DECIDE TO DO ANYTHING STUPID AGAINST THEIR OPPONENTS!!.

The big question is.......WATAWEZA?....na wakiweza;......ILI IWEJE?

TUNASUBIRI!!
 
Watanzania tuna mambo!.

Kwa nini watu wanatumia nguvu sana kujadili kitu ambacho kiko wazi kisheria?. Sheria za nchi zimempa madaraka msajiri wa vyama vya siasa kukifuta chama kulingana na vigezo vilivyoainishwa katika sheria.

Ni sawa na kuanza kutumia nguvu kusema judge hawezi kuhukumu adhabu ya kifo wakati sheria inamuruhusu kufanya hivyo kulingana na vigezo kama vilivyoainishwa katika sheria.

Tunaweza tukasema sheria hii kwa sasa iko kinadharia kwa sababu haijawahi kutumika nchini kwa chama chochote chenye hadhi kama ya CHADEMA katika mazingira ya CHADEMA na kwenye swala linaloihusu CHADEMA.

Mkuu Pasco ,

Jaribu kuwa unaweka mabandiko yako katika lugha ya kawaida ili watu wengi waweze kuelewa. Unapotumia PARABLES kama maandiko kwenye vitabu vya maandiko ya mungu, unawafanya watu wengi hapa janvini kama nilivyobaini kutokuelewa ujumbe wako na matokeo yake, hata michango yao inakuwa nje ya mada uliyoileta.
 
Last edited by a moderator:
sitofurahia CHADEMA ifutwe bali ijirekebishe na ikubali kukosolewa kila mara inapokosea (TUKO PAMOJA) :yell:
 
Ni rahisi kuifuta UDP au TLP kwakuwa ukimwondoa CHEYO AU MREMA chama hakipo, LAKINI CHADEMA sivyo ilivyo!.
HIVI KUMUONDOA CHEYO NA MREMA kuna tofauti gani na kuwaondoa SLAA na MBOWE? Si hao ndiyo CDM yenyewe? Ukiwaondoa kuana CHADEMA Tena? Lema, Sugu, Nasari, ABWAO NA wengine si kazi yao ni kulamba miguu wa hao mabosi wao tu na wakiondoka huwezi kuwasikia tena.
 
CHADEMA wanafikiri bunge linaweza kuingilia maamuzi ya msajili wa vyama kama walivyofanya kwenye kesi ya UGAIDI dhidi ya LWAKATARE hadi kupelekea kufutiwa mashtaka wakati ni dhahiri lile ni tukio la ugaidi
 
naona hiyo bonafide genuine inakuwasha bila kuitumia hujisikii mkuno

mbafff
 

Mnachoongea wala hakipo. Kesi ngapi mawakili wa serikali wanashindwa na wakishindwa basi serikali nayo inafutwa!!! Kujua sheria tu hakutoshi. Mafarisayo na Waandishi waliojua taratibu au sheria za Kiyahudi walimpelekwa mwanamke kwa evidence zote lakini Kijana Yesu aliwaambia neno moja tu - "Anayejiona hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe huyu mwanamke." Thubutu, kama alibaki mtu pale. Wote waliokuja pale ndo walikuwa wazinzi namba moja. Yawezekana hata lile jamaa lililozini na yule mwanamke nalo lilikuwepo, eti kwa kuwa ni janaume (may be chama utawala) halikushtakiwa. Lwakatare anataabika tu, lakini mwenye kufanya hayo yupo naye amechukua mawe kutaka kumtupia mtoto wa watu. Haki haipotei ila inacheleweshwa.

Nitashangaa sana kama kweli mzee Tendwa na age yake hiyo alitoa maneno hayo ambayo kimsingi ni ku-pre-empty kesi iliyoko mahakamani. Kama kweli alisema, basi hatuna kitu kabisa. Ni kujilisha upepo tu.

Naipenda Tanzania.
 

Na ndiyo maana Wajumbe wa Katiba ngazi ya Kata ni CCM pa see kisa ni kulinda maslahi ya CCM.
 
Chadema ni sawa na vyama vingine tu vilivyoko hapa nchini,kama kina makosa kinafutwa tu!hakipo juu ya sheria na kama kuna mtu yeyote anajidanganya kwamba cdm kiko juu ya sheria wasubiri waje waone na hakitafutwa kwa sbb hizo alizotoa Pasco isipokuwa kinakuja kufutwa kwa sbb tofauti.
 
Kwavile mkanda ni bonafide genuine na kwavile CHADEMA wamekataa kujitenga na mambo binafsi ya Lwakatare, basi Tendwa asilaumiwe huko mbeleni...

Thubutu yake hana uwezo wa kufanya siku akifanya hivyo najisaidia haja kubwa katikati ya ukumbi wa bunge nasema haya nikijua hawezi ata kujaribu kukifuta kwani yeye mnamuona mjinga kiasi icho.
 
Haitakaa itokee hata kama itathibitishwa kwamba ni kweli, kwani wenzetu hawa are not only organized, but are increasingly becoming institutionalized;we have to come into terms with a fact kwamba chadema is both a political movement and a political party; the last thing ccm inataka ni kumaliza chadema as a political party by an artificial death na kukifungulia mlango to specialize as a political movement;

Ni vigumu kuelewa kwanini ccm tunashindwa kuelewa kwamba hata chadema leo hii waseme wanaamua kukifuta chama chao wa ridhaa yao, haina maana kwamba ccm ndio tutasalimika; adui yetu ccm sio chadema bali viongozi wetu wengi walioamua kwa makusudi kabisa kuachana na misingi ya chama kwa mujibu wa katiba, mwongozo na baadhi ya masuala mazuri ndani ya azimio la arusha;

Ni muhimu tuelewe kwamba katika dunia ya leo inayoendeshwa kwa nguvu za utandawazi, watanzania wengi wanazidi kuelewa the prominent role of liberal democracy katika kuboresha maisha yao, na kwa sasa wengi wao wanazidi kujenga imani na chadema - kwamba ndicho chama kinachoweza kuwa mbadala wa ccm, for how long? It remains to be anybody's guess;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Pasco pamoja na maelezo yako mazuri ambayo yanaweza kumshtua mwanangu wa chekechea ambaye anaijua salamu ya salamu ya chadema nikiri kuwa umeshindwa kulitendea haki jukwaa letu pendwa la JF! Yaani katika udaku wote wa kujitishia nyau wewe na Mzee hukuweza kuumuliza kwa nini anakiuka tamaduni za utawala bora?!

Unge muuliza kwa nini umri wa kustafu umesha mfika na bado ana ng'ang'ania kuwa mbeba mbeleko wa ccm?
 
Last edited by a moderator:

Umesema vema. Mungu hana chama kabisa. Mungu ni wa watu wote. Jambo moja kubwa ni kwamba Mungu anachukia sana uovu na hasa uovu wa kuwaumiza watu na kuwafanya mateka kwa ajili ya maslahi ya watu au kikundi bila kujali ni kikundi cha chama au vipi. Mungu hana chama, lakini hutumia taratibu zetu katika kufanya kazi. Anaweza pia kutumia utaratibu wa vyama kwani ndo mfumo tuliokubaliana nao ili kupata viongozi. Si njia sahihi kuonyesha kuwa Mungu yupo katika chama fulani, you cannot contain God. Ifahamike kuwa Mungu anachukia sana ufisadi. Neno "Ufisadi" ni la Kibiblia na linaelezwa tangu agano la Kale. Israel waliadhibiwa sana kwa sababu ya matendo maovu na kubwa likiwa ni "Ufisadi" - yaani "Uchafu" - Corrupt. Serikali yoyote fisadi haimpendezi Mungu kabisa na hasa Ufisadi unapokuwa sehemu ya mfumo ambao unalindwa na kutetewa kisiasa na kiutawala. Chama fisadi hakimpendezi Mungu - kwa mujibu wa vitabu vitakatifu na kwa maadili yetu.

Narudia kusema: Mungu hana Chama. Hata hivyo Mungu anatumia hata mifumo yetu kufanya kazi yake.

I love Tanzania
 
Ukizidiwa unatumia mbinu zozote kujilinda lakini hiyo hauzui haki kupatikana. Iko mifano mingi: 1. Mandela alihukumiwa kwenda jela maisha lakini siku ilipotimia akawa raisi wa Afrika ya kusini 2. Wakoloni wali mtisha baba wa taifa asiendeleze juhudi zake za kutafuta uhuru mwisho wa siku uhuru ulipatikana.

Kwahiyo kuifuta CHADEMA SIO KUZUIA UKOMBOZI WA PILI WA NCHI HII, NA KWA HAKIKA WENGI WATAISHIA JELA KWA UFISADI WALIO UFANYA KATIKA NCHI HII. JAMANI NANI ANAYEFURAHIA UFISADI, HATA HUYO TENDWA TUMULIZE HAONI KUWA CCM KWELI IMESHINDWA KUDHIBITI UFISADI, KATIBU WAO DIYO HUYO JANGILI, MAWAZIRI NDIYO HAO WANASAINI MIKATABA KWA MANUFAA YAO BINAFSI, VIONGOZI WANAFICHA HELA ZA NCHI USWISS, WANANCHI KILA KUKICHA MAISHA YANAZIDI KUWA MAGUMU, HUDUMA ZA JAMII HAKUNA HATA MOJA YENYE NAFUU SASA WAKIFUTA CHADEMA HIYO HALI ITABADILIKA?. TATIZO SIO CHADEMA TATIZO NI WIZI, UFISADI, KUPUUZA WANANCHI. ZeMarcopolo
 
Last edited by a moderator:
Na ule ushahidi uliomwagwa na Marando ukiwahusisha viongozi wa CCM kwenye mchezo huo mchafu ukithibitishwa pasipo shaka yoyote atakuwa tayari kuifuta CCM?
 

Hakuwaacha watangetange jangwani, get your facts right, alikuwa nao jangwani for all those years mpaka alipoowaona wapo mature enough to go to the next stage.

Hata wewe mtoto wako huwezi kumpeleka shule akiwa na miezi 9, utakaa nae na utamngojea huku ukimsaidia mpaka umri wa kwenda shule ukifika na akiwa mature enough intellectually ndio utampeleka shule.
 
Aisee,
Kama nimekuelewa Mkuu wangu Pasco ni kwamba, towards 2015 chama kimoja wapo kikubwa kabisa hapa Tanzania kitapotezwa kwenye ulingo wa siasa; yaani ama CHADEMA au CCM! Manake, hata kama CCM ndio watabainika na hivyo kuachwa mahakama iamue; basi maamuzi fair yatakuwa kwamba CCM hawataruhusiwa kushiriki uchaguzi mkuu 2015! Kama hivyo ndivyo; je ikithibitika kwamba tatizo ni CCM; Mahakama itawachukua miaka mingapi kutoa hukumu ya kesi ya msingi (ya Lwakatare)? Labda wataangalia matokeo ya uchaguzi 2015; CCM wakirudi madarakani, maamuzi ya kesi ya msingi yatakuwa suspended for more five years but ikiwa ni CHADEMA ndo wataingia madarakani; kesi ya msingi itaamuliwa somewhere between January to July 2016!

Hapa napata picha moja! Tukiona hukumu inachelewa kutolewa hadi kufikia October 2015, then possibly CCM found involved in one way or another lakini tukiona hukumu inatolewa mapema, manake yake Lwakatare na CHADEMA found guilty!
 
Last edited by a moderator:
Maneno machafu kama haya yanaandikwa na watu wenye mawazo mgando kama wewe

kuna msemo unasema never argue with a fool, people might not notice the difference... sasa wewe usiye na mawazo mgando vipi??? mbona unakua kama unawashwashwa pia??

wabhejasana mama!!
 
Ndugu yangu kwa sasa CCM kuifuta CHADEMA KWA kupitia vyombo vyake vya utawala pamoja na ofisi ya msajili wa vyama, wanajua ni kama mtu kuchukua petroli na kujimwagia kisha ujilipue moto, hiyo itakuwa ni hatari kwa serikali inayo tawala!!!

 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…