Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania chamtaka Rostam Aziz kuthibitisha tuhuma alizotoa dhidi ya Majaji na Mahakama ya Kisutu

Yani huyu muhindi anapambana na mahakama!?? Je mahakama ikiamua kumfikisha mahakamani kwa uchafuzi wa jina si amekwisha asubuhi na mapema
Inaweza pigwa tena simu kuwa aachwe[emoji23].
But huyu jamaaa ana reputation ya utafunaji fedha yes, lakini sijui kama ana histiria ya ujinga wa kuongea hivi hadharani.

Kwanini kaongea kipindi hiki, na sio kipindi cha JPM? Anayajua mangapi, matajiri wanajua mambo mengi sanaaa..
 

Wanajibaraguza tu,ukweli unafahamika mahakama na bunge na rubber stamp kwa mwenyekiti wa chama cha majambazi.

Hii nchi kile kinachoitwa mihimili kujitegemea ni maigizo matupu,kwahili naichukia sana hii nchi.
 
Rostam yupo sawa kabisa
 
Athibitishe sasa
Athibitishe wapi? Mahakamani? Achemi mikwara nyie!
Sawa
Athibitishe
Athibitishe kwa nani? Athibitishe wapi? Eti aitishe vyombo vya habari! Nani asiyejua vyombo vya habari navyo vinapokea maagizo? Nchi hii kwa unafiki hamjambo. Je asipothibitisha mtamfanya nini? Mtampeleka Mahakamani, thubutu!

Siku hiyo bila shaka mtamjua Rostamu ni nani! Muulizeni Nape Nnauye aliyeitaka chama tawala, CCM, kujivua magamba. Magamba matatu hadi leo yako pale pale! Mojawapo alikuwa Rostamu na hivi sasa anasaini mikataba huku Rais, anayewateua majaji na mahakimu akishuhudia!! Shauri yenu!
 

1. Asipotaja kama wanavyotaka watamfanyaje?
2. Asipoomba radhi baada ya kutomtaja watamfanya nini?
Hao majaji na chama chao kwa hili tamko lao inaonyesha wanamuogopa, kumfanya chochote hawawezi kisheria la sivyo wangeanisha na hatua ambazo wanaweza kumchukulia kwa kunukuu vifungu vya sheria!
Tamko lao ni useless, Rostam ikibidi arudi tena kwenye media aseme hili tamko ni "professional rubbish" na siyo kuomba radhi!
 
Wanajitutumua hao. Namuunga mkono Rostam .... Huo ndiyo ukweli wenyewe. Hata Jaji Mkuu uteuzi wake ulifanywa na JPM kwa mtindo uleule....!!
Aliteuliwa naibu jaji mkuu,akasotoe hiko cheo karibu mwaka mzima ndo akawa jaji mkuu
 
Mkuu kamwekaje Mwanasheria Mkuu!?
 
Ile kauli aliitoa toka moyoni kabisa na hata akikanusha watu wamesha mwelewa na pia yeye atabaki na huo ukweli wake moyoni mwake.

Hizo zitabaki kuwa taratibu tu za kuomba radhi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…