Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania chamtaka Rostam Aziz kuthibitisha tuhuma alizotoa dhidi ya Majaji na Mahakama ya Kisutu

Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania chamtaka Rostam Aziz kuthibitisha tuhuma alizotoa dhidi ya Majaji na Mahakama ya Kisutu

Ila ndio ukweli na hii sio kwa mahakimu tu hata majaji wako hivyo!
Kuna mifano hai mingi sana na huenda jukwaa hili likatumika kuwaumbua mcchana kweupe!
 
Kiongozi wa taifa letu na machawa wake
FB_IMG_16862516449430799.jpg
 
Kwa mantiki hii sasa wenye hoja kuwa mkataba wa DP world mahakama zetu ziwe ndio watatuzi wa kesi btn Gov and Dp na sio South Afrika
 
Mnamo tarehe 26 Juni, 2023 manyabiashara Bw. Rostam Azizi wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu masuala ya uwekezaji alinukuliwa akiituhumu aliyoiita Mahakama ya Kisutu kwa kutokuwa huru katika uendeshaji wa shughuli zake.

Kutokana na taarifa hiyo tunapenda kuhabarisha umma yafuatayo:

Hakuna Jaji anayehudumu katika Mahakama hiyo kama ilivyoripotiwa na mzungumzaji wa taarifa hiyo.

Mahakama ya Tanzania ni chombo pekee cha utoaji haki nchini kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na huendesha shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu au chombo chochote.

Uongozi wa Mahakama na au Chama Cha Majaji na Mahakimu haujawahi kupokea tuhuma au lalamiko lolote kutoka kwa mtu yeyote ikionyesha Maafisa wa Mahakama kupigiwa simu na kuelekezwa namna ya kutoa maamuzi katika mahakama hiyo.

Kutokana na maelezo hayo Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania tunatoa kauli zifuatazo:
  1. Tumesikitishwa sana na kauli za Bw Rostam Aziz ambaye hatukutegemea aongee mambo mazito kama hayo bila kuwa na uhakika wala uthibitisho.
  2. Matamshi ya Bw Rostam Aziz yanaweza kuhatarisha uhusiano na ushirikiano katika mihimili mitatu ya dola ndani ya nchi yetu.
  3. Tunaomba wananchi wenye nia njema na Mahakama na mihimili mingine waendelee kuwa na Imani na mfumo wa utoaji haki nchini.
Kwa taarifa hii, Chama Cha Majaji na Mahakimu Tanzania kinamtaka Bw. Rostam Azizi athibitishe kauli yake akibainisha jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Kiongozi wa Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo.

Akishindwa kutoa uthibitisho tunamtaka atumie Jukwaa lile lile kuomba radhi kwa uzito ule ule.

Imetolewa na:
UONGOZI WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU TANZANIA (JMAT)
4 JULAI 2023


Pia soma: Rostam Aziz: Hakuna mwekezaji atakubali kuwekeza halafu umwambie aende Mahakama ya Kisutu ambapo Majaji wanaweza kupigiwa simu na watu wa Serikali
Sasa wanashtuka kuambiwa ukweli?
 
Haya
 

Attachments

  • 8E4489CA-2873-4251-AAE3-3A494B5B7999.jpeg
    8E4489CA-2873-4251-AAE3-3A494B5B7999.jpeg
    137 KB · Views: 2
Rostam aliishuku mahakama hiyo Juni 26, mwaka huu alipozungumzia sakata la bandari akisema, “Hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.”

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Rostam alizungumzia faida za uwekezaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari, akirejea mkataba wa ushirikiano uliosainiwa na Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.

Hata hivyo, sakata hilo limeibua hisia tofauti za wananchi, wengine wakikosoa kutokana na kile wanachoeleza kuwa, baadhi ya vifungu vya mkataba huo vina kasoro na hatari kwa masilahi ya nchi.

Kutokana na kauli yake, iliyotafsiriwa kuwa ni kuidharau Mahakama, JMAT imechapisha taarifa kwa umma leo, Julai 4, 2023 ikimtaka mfanyabiashara huyo athibitishe kauli yake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, chama hicho hakikuwahi kupokea tuhuma au lalamiko lolote kutoka kwa mtu yeyote ikionyesha maofisa wa mahakama kupigiwa simu na kuelekezwa namna ya kutoa uamuzi.

“Kutokana na maelezo hayo, tumesikitishwa na kauli ya Rostam Aziz ambaye hatukutarajia aongee mambo mazito kama hayo bila kuwa na uhakika wala uthibitisho,” imeeleza taarifa hiyo.

JMAT kupitia taarifa hiyo, imesema kauli za mfanyabiashara huyo zinahatarisha uhusiano na ushirikiano kati ya mihimili mitatu ya dola ndani ya nchi.

“Tunaomba wananchi wenye nia njema na Mahakama na mihimili mingine waendelee kuwa na imani na mfumo wa utoaji haki nchini," imeeleza.
 
Back
Top Bottom