Chama cha Mapinduzi champongeza Rais Samia kwa kuimarisha Demokrasia

Dogo mtahangaika Sana! ccm haina mvuto hata mfanye kitu gani hakuna kitu mtabadili labda mkubali katiba mpya
Chadema inamvuto wapi?

Mbona mlisema chanjo ni agenda yenu mbona mlikwama mpaka Rais Samia alipokuja kuweka mambo sawa,
 
Mi sio chadema lakini niweke kumbukumbu sawa. Msimamo wa chadema ulikuwa ni kukubali uwepo wa covidi na kuchukua tahadhali, ikalazimu Wabunge wa cdm kuondoka bungeni kwenda lock down, maccm mkiongozw na yule zwazwa dugai mkawaponda sana.

kumbuka upuuzi wa Mwendakuzimu aliwabeza cdm, who, jumuiya ya kimataifa, pamoja kanisa katoliki, lakini covidi ikamwondoa duniani
 
Hakika!

Rais wetu mpendwa Samia ameonyesha ushupavu wa hali ya juu.

ushupavu wake na Uimara wake alio uonyesha ndani ya muda mfupi umetufanya watanzania wote tujiamini zaidi.

tunamuomba aendelee hivyo hivyo.

tunamuombea Mungu azidi kumlinda.
Miezi sita ya Rais Samia,

Nchi imetulia tuli,
Wawekezaji kama wote
Wahisani kama wote
Wananchi Shangwe kila kona

#KAZIIENDELEE
 
Mi sio chadema lakini niweke kumbukumbu sawa. Msimamo wa chadema ulikuwa ni kukubali uwepo wa covidi na kuchukua tahadhali, ikalazimu Wabunge wa cdm kuondoka bungeni kwenda lock down, maccm mkiongozw na yule zwazwa dugai mkawaponda sana.

kumbuka upuuzi wa Mwendakuzimu aliwabeza cdm, who, jumuiya ya kimataifa, pamoja kanisa katoliki, lakini covidi ikamwondoa duniani
Chanjo haikuwa sera ya Chadema awali?
 
Dogo mtahangaika Sana! ccm haina mvuto hata mfanye kitu gani hakuna kitu mtabadili labda mkubali katiba mpya
Rais Samia ameongeza wanafunzi 29,000 kwenye mikopo ya elimu ya juu HESLB kwa miezi sita tu,

miaka mitano mfululizo iliyopita tulifanikiwa wanafunzi wapya 32,000

Unaisemaje kasi ya Rais Samia?
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza na kumshukuru amiri Jeshi mkuu na Rais wa JMT Mama Samia Suluhu Hassan kwa Uzalendo wake kwa Taifa, Ushupavu na Ujasiri katika kulinda na kusimamia "Tunu za Taifa" letu kwa nguvu zake zote kwa akili zake zote na kwa moyo wake wote huku msingi mkuu wa yote haya ukiwa ni kuwaletea wananchi hawa masikini maendeleo endelevu.

Chama cha Mapinduzi pia kimempongeza na kumsifu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwathamani watumishi wa umma nchini ikiwa ni baada ya zaidi ya watumishi 180,000 kupandishwa vyeo (kuongezwa mishahara) na Wale wote wanaodaiwa mikopo ya bodi (HESLB) ambao kila mwezi walikatwa 15% ya Mshahara wao Mhe Samia Suluhu Hassan kawaondolea hiyo Value Retention Fee (VRF) ambayo ilikuwa ni 6% nakuwafanya wakatwe 9% tu kwa mwezi hivi leo.

Chama cha mapinduzi kimempongeza pia Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupunguza kodi ya Mishahara kwa watumishi wote wa Umma na binafsi yaani (PAYE) kutoka 9% ya awali hadi 8% hii yote ni nia ya Serikali ya CCM katika kuwaletea wananchi wake maendeleo endelevu.

Chama kimempongeza zaidi Rais Samia Suluhu Hassan katika kusimamia Utawala wa Sheria na Utawala bora, Haki za kibinadamu, Ukuzaji mkubwa wa demokrasia ya vyama vingi nchini, kujenga inchi isiyoyegemea itikadi ya dini|kabila|kanda yeyote na kuufurusha kila aina ya Ufisadi na Rushwa nchi.

Haya yamesemwa na Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi CCM Taifa Mhe Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akiongea na Wanahabari Ofisi ndogo ya Lumumba Jijini Dar es Salaam.

👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

Kutoka Mwaka 2015/16 hadi 2020/21 pesa iliyoongezwa bodi ya mikopo ilikuwa Tshs 101BL na wanafunzi wapya walikuwa elfu 32 ,

Awamu ya sita kwa miezi sita pesa iliyoongezwa kwenye bodi hiyohiyo ni Tsh 120b na wanafunzi wapya ni elfu 29

Budget ya HESLB kwa mwaka 2015/16 ilikuwa 348.7B kwa wanafunzi 98,300

Budget ya HESLB mwaka 2020/21 ilifikia 450B kwa wanafunzi 130,883

_________________________

Awamu ya sita kwa miezi sita imeongeza budget kutoka 450B za awali hadi 570B za sasa na idadi ya wanufaika imeongezeka na kufikia 160,000.

#Hoja hapa ni muda wa matokeo

#HAKUNA KAMA SAMIA
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza na kumshukuru amiri Jeshi mkuu na Rais wa JMT Mama Samia Suluhu Hassan kwa Uzalendo wake kwa Taifa, Ushupavu na Ujasiri katika kulinda na kusimamia "Tunu za Taifa" letu kwa nguvu zake zote kwa akili zake zote na kwa moyo wake wote huku msingi mkuu wa yote haya ukiwa ni kuwaletea wananchi hawa masikini maendeleo endelevu.

Chama cha Mapinduzi pia kimempongeza na kumsifu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwathamani watumishi wa umma nchini ikiwa ni baada ya zaidi ya watumishi 180,000 kupandishwa vyeo (kuongezwa mishahara) na Wale wote wanaodaiwa mikopo ya bodi (HESLB) ambao kila mwezi walikatwa 15% ya Mshahara wao Mhe Samia Suluhu Hassan kawaondolea hiyo Value Retention Fee (VRF) ambayo ilikuwa ni 6% nakuwafanya wakatwe 9% tu kwa mwezi hivi leo.

Chama cha mapinduzi kimempongeza pia Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupunguza kodi ya Mishahara kwa watumishi wote wa Umma na binafsi yaani (PAYE) kutoka 9% ya awali hadi 8% hii yote ni nia ya Serikali ya CCM katika kuwaletea wananchi wake maendeleo endelevu.

Chama kimempongeza zaidi Rais Samia Suluhu Hassan katika kusimamia Utawala wa Sheria na Utawala bora, Haki za kibinadamu, Ukuzaji mkubwa wa demokrasia ya vyama vingi nchini, kujenga inchi isiyoyegemea itikadi ya dini|kabila|kanda yeyote na kuufurusha kila aina ya Ufisadi na Rushwa nchi.

Haya yamesemwa na Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi CCM Taifa Mhe Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akiongea na Wanahabari Ofisi ndogo ya Lumumba Jijini Dar es Salaam.

Kuwa chawa wa CCM ni fedheha sana.
 
Back
Top Bottom