Jana ilikuwa mara yangu ya kwanza kuangalia Taifa stars live. Wanamatatizo makubwa ya kiufundi. Na itachukuwa muda na juhudi kuyarekebisha.
Kwanza Taifa stars wana viungo ambao hawajiamini wanapokuwa na mpira. Soccer inaendeshwa na wachezaji viungo wanaojiamini na wenye uwezo wa kumiliki mpira na kufanya maamuzi sahihi. Hili bado kwetu ni tatizo. Mechi ya jana stars walishindwa kabisa kumiliki mpira na kumalizia pasi mara kwa mara.
Defenders wetu pia walikuwa waoga na hivyo kusababisha kona kadhaa ambazo zilikuwa zinatia hofu kutokana na ufupi wa wachechazi wetu. Kutokana na woga huu, defenders wakawa wanalazimisha kubutua mipira ambayo 90% iliishia miguuni mwa wapizani.
Bado hakuna maelewano miongoni mwa wachezaji. Ilikuwa vigumu sana kuona plans za wachezaji wetu katika ushambuliaji, umaliziaji na uokoaji. Kulitokea wakati kipindi cha pili mchezaji wetu alishindwa ku-control cross akiwa pekeyake kwasababu hakutegemea. Kulitokea wakati kipindi cha kwanza mchezaji wetu alitoa cross bila kumlenga mchezaji anayetakiwa amalizie cross yake.
Bado wachezaji wetu wanashindwa kusoma na kurekebisha kasi ya mchezo. Mfano wachezaji wetu walishindwa kutumia advantage ya mbio waliokuwa nazo. Wapizani wetu mwanzoni waliofu mbio zetu hivyo wakaweka ndefenders juu ya mstari wa maguu 18...cha ajabu walivyofanya hivyo sisi tukabaki nyuma tukicheza mpira wa taratibu, na wakaona hakukuwa na haja ya kuweka walinzi wao kwenye 18, na walipowaleta mbele tukawa matatani. Kwa kutotumia mbio zetu kipindi cha kwanza tukaonekana kama tulikuwa tunalazimisha draw au tunacheza kwa kujihami. Tulipokuwa tunatumia mbio na kuongeza kasi tulipata nafasi kadhaa.
Bado tunatatizo kubwa la kupiga free kicks na kona. Tulipata free kicks ambazo hazikuleta japo chembe hatari golini mwa wapinzani. Tunajuwa kwamba wachezaji wetu ni wafupi kulinganisha na wapinzani lakini bado free kicks zetu zilikuwa za juu. Sikuona sababu ya kutopiga short kicks (kugeuza free kicks kuwa short pass).
Goli tulilofungwa lilikuwa lakizembe mno, na linatokana na makosa niliyoyataja hapo juu. It is very simple, kama timu inawachezaji wafupi inatakiwa isiruhusu wachezaji wa timu pizani wapige cross. Hii ina maana kwamba mpira ukivuka mstari unaogawa uwanja kuelekea golini kwetu, viuongo na walinzi lazima wacheze man-to-man (police marking) ili kuzuia cross ambazo wanajuwa zitawashinda. Yule mchezaji wa Senegal aliyetoa cross alikuwa na muda wote wakuchagua apeleke wapi cross yake, na alipanga mapema hata kabla hajapata mpira, na Senegal walijuwa kwamba mipira ya juu itawapa ushindi.
Kipa wetu ingawa anastahili pongezi kwa kucheza vizuri sana kuliko wachezaji wote, bado alikuwa na uwezo wa kuzuia goli tulilofungwa kama ange ji-position vizuri. Simple: kipa anatakiwa kufanya maamuzi sahihi ya wapi asimame. Kukiwa na cross na kipa akajuwa kwamba hawezi kuikata (ku-intercept) kipa anatakiwa asimame katikati ya gori kwenye mstari au mita moja kutoka mstarini ili kuongeza ugumu kwa mfungaji kwani mfungaji atalazimika kuongoza mpira kwenye nyavu ndogo na kwa kasi, hii inaongeza chances za kukosa. Sasa kipa wetu huku akijuwa kwamba hasingeweza kuikata cross akaondoka kwenye mstari na kuwa nusu kipa nusu mlizi, laiti kama angekuwa kwenye mstari katikati ya goli angedaka bila ya papara. Kipa hafunzwi kudaka tu bali anafunzwa kufanya maamuzi ya positioning.
Hopeful tutasonga mbele pamoja na matatizo yetu.