CHAN Finals: Live from Ivory Coast

CHAN Finals: Live from Ivory Coast

Ina maana Nsajigwa na Canavarro?
wamejitahidi tatizo na ugeni wa mechi za kimataifa.....

....hivi rire rishem korofi Nyani Ngabu halinaga hobby na soka naona......siasa hajui....olimbaga kinehe
 
wamejitahidi tatizo na ugeni wa mechi za kimataifa.....

....hivi rire rishem korofi Nyani Ngabu halinaga hobby na soka naona......siasa hajui....olimbaga kinehe

NN yuko busy kwenye jukwaa la mambo ya kikubwa .....!!
 
Maelezo kamili ya game la Tanzania na Senegal kwa waliolimiss

BAO lililofungwa kwa kichwa na Traore katika dakika ya 35 katika mchezo ulioisha muda mfupi uliopita, limeiwezesha Senegal kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Tanzania katika mchezo wa michuano ya CHAN.

TRAORE alifunga bao hilo akiunganisha krosi safi kutoka upande wa kulia wa Uwanja baada ya mabeki wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Swed wakiwa wameduwaa.

Licha ya kufunga bao hilo katika mchezo huo wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), Stars ilionekana kuwamudu Senegal hasa katika dakika za mwanzo na mwisho za pambano hilokali na la kusisimua.

Mshambuliaji wa Stars, Jerry Tegete alikosa bao la wazi katika dakika ya nane ya mchezo huo baada ya kupiga shuti kali kuelekea langoni kwa Senegal, lakini mpira huo uliwababatiza mabeki.

Dakika nne baadaye, Mrisho Ngassa alipiga krosi safi kuelekea langoni kwa Senegal lakini haikuweza kuunganishwa na washambuliaji wenzake kutokana na kutokuwapo katika eneo la hatari kwa mchezaji yeyote wa Stars.

Bao hilo la Senegal lilidumu hadi mapumziko licha ya Kocha wa Stars, Marcio Maximo kuwatoa Bonny na Haruna Moshi ‘Boban’ katika kipindi cha kwanza na nafasi zao kuchukuliwa na Nurdin Bakari na Mussa Hassan ‘Mgosi’.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini hakuna timu iliyoweza kupata bao japokuwa kila wakati safu za ushambuliaji za timu hizo ziliweza kufika katika lango la wapinzani wao.

Stars itashuka tena uwanjani keshokutwa kucheza na wenyeji Ivory Coast ambao katika mchezo wa ufunguzi walifungwa mabao 3-0 na Zambia.

Stars iliwakilishwa na; Shaaban Dihile, Shadrack Nsajigwa, Juma Jabu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Swed, Geofrrey Bonny, Haruna Moshi ‘Boban’, Henry Joseph, Nizar Khalfan , Mrisho Ngassa na Jerry Tegete


Source: nifahamishe.com
 
The Teranga Lions of Senegal claimed their first win of the tournament with a lone goal victory over Tanzania’s Taifa Stars in their Group A clash on Sunday at the Felix Houphouet Boigny Stadium in Abidjan.

Midfielder Traore Mamadou’s 29th minute strike ensured victory for the Senegalese who were given a good run by the Tanzanians.

The match charcterised by midfield saw dominate proceedings from the early stages that resulted in the opener.

Midfielder Ndiour Babacar after making his way into the Tanzania half, fetched Traore, who made no mistake by shooting past goalkeeper Mohamed Shaban.


The Tanzanians resumed the second half strongly but their attempts at drawing parity yielded no results.


The result puts Senegal on same points as Zambia, with the latter having superior goal difference with Tanzania and Cote d’Ivoire following in that order pointless.

Senegal next play Zambia whilst Cote d’Ivoire face Tanzania.

Quotes

Joseph Koto (Coach, Senegal)
“The first match is always important in every competition and the best result is to win.

Winning the first match always puts you good position to qualify.

“I am happy with the result but not impressed with my team’s performance. They did not play to my instructions and I hope they will be better against Zambia on Wednesday.”

Marcio Maximo (Coach, Tanzania)

“I have always said this competition will be a good test for my team. This is an opportunity to play against some of the best teams in Africa.

“We have lost but we hope to improve in our next match against Cote d’Ivoire.”


Source: cafonline.comhttp://www.cafonline.com/competitio...-senegal-pip-tanzania-to-claim-first-win.html
 
Du, mwanzo mbaya japo hatujafungwa mengi. Tafadhali mlioona hiyo match tusimulie ilikuaje.
 
Kwa kuangalia mechi ya jana sioni namna ambavyo Staz inaweza kututoa kimasomaso au kutupa raha kama asemavyo JK. Udhaifu mkubwa ambao nauona na ambao huwa unawakumba wachezaji wetu na benchi la ufundi, hali ya kuridhika na mchezo wa historia. Hebu ona tulivyokuwa tukijiandaa na mechi ya jana:

Wengi walikuwa na mawazo haya, katika mechi mbili za mwisho tulizocheza na Senegali, mechi ya kwanza walitufunga kwao bao nne, mechi ya pili Mwanza almanusura tuwafunge kabla ya kutuchoropoka zikiwa zimesalia dakika tisa waliposawazisha bao letu. Lakini timu tuliyotoa sare nayo siyo hii bali ni ile iliyosheheni wachezaji wanaosakata kabumbu la kulipwa katika timu za ulaya. Kwa mantiki hiyo kwa vile hawa ni wachezaji wa ligi ya ndani, hapana shakaka watakuwa wetu tu na tutawapiga bao. Sijui kama na wachezaji na Benchi lao la Ufundi walikuwa wanafikira kama hizi. Lakini Mgeni aliyekuwa TBC 1 aliongea fikra hizi laiv. Kama kulikuwa na fikra hizi miongoni mwa wachezaji, ni wazi ushindi ni ndoto.

Lakini kingine ni pale Maximo alivyoshindwa kuwaelekeza wachezaji wetu kutumia zaidi mchezo wa chini baada ya kuwa wachezaji wetu kuzidiwa urefu n a Wasenegali. Kwa vimo vya wachezaji tulionao, total football ndiyo suluhu yetu
 
It was the same old "TAIFA STARS"!

Defensive we were horrible, Midfield was completely asleep, forward line was kept alive by Mrisho Ngassa (who is an attacking midfielder!).

What I saw tells me that, we will NOT WIN any match. I've lost all the hopes!
 
Hapa sasa, uwezekano wa kuacha kutegesha kichwa ili jamaa wajifunze kunyoa ni mdogo. Lakini wanasema mpira unadunda, lolote lawezekana. Kama tukishinda mechi inayofuata na wenyeji, then Zambia na Senegal watoke sare kidogo tutajiwekea matumaini ya kusonga mbele.
 
All in all they need to win Wednesday match with Ivorians, no matter what.
 
Stars walionesha uhai kwenye dak 30 za mwisho na bado forwad zilikuwa butu sana yaani shots on goal zilikuwa kama mbili tu...Kuna kazi kubwa sana kwa stars kusonga mbele..tunaweza kuwafunga wenyeji ila zambia na senegal wanasonga mbele kwenye kundi letu..kabumbu safi walioonesha zambia inatosha kunithibitishia kuwa watakuwa vinara wa kwenye kundi...Ngoja tuone za leo zitakavyokuwa then tutaweza kujudge wot next...
 
Mimi nikimlaumu mwalimu mara nyingi, wengi huniona labda simpendi, lakini kuthibitisha udhaifu wake jana kaonesha. hakupaswa kumuanzisha dogo tegete, tegete kwangu mimi ni supersub, anatakiwa kukaa nje akiusoma mchezo na kuingia kwenye kipindi cha pili. pia tabia ya defending muda mrefu sio nzuri, uanze defensive game baada ya kupata bao.
Lakini bado nina matumaini na vijana.
 
Hakika umesema, sisi tunatakiwa tuwakimbize mpaka wachanganyikiwe, then ndio tuwapige mabao, tukitegemea kucheza kama wao hamna kitu.
 
Tatizo letu moja tuu.....kama mkubali ama msikubali..wachezaji wetu bila ndumu hawana moral kabisaa...hilo ndio limewafanya wazubae uwanjani maana hawajui lini waliweza kucheza bila ndumu.....wooote wameshazoea nguvu ya ndumu....kazi ipo sana ...wale senegal ni watoto wadogo ambao wote wametoka kwenye football academy mpira wa kufundishwa na kufanyia home work....kazi ipo...waso so physique kulinganisha na sisi...hatuwezi kumiliki mpira wala kukaa nao...
 
It was the same old "TAIFA STARS"!

Defensive we were horrible, Midfield was completely asleep, forward line was kept alive by Mrisho Ngassa (who is an attacking midfielder!).

What I saw tells me that, we will NOT WIN any match. I've lost all the hopes!


Not only that but if they play like they did against Zambia they could get thumped at least 5-0.
 
Ilinikatisha ssaana tamaa maana majigambo na masifa waliyokuwa wakijipa hasa kutoka kwa Mr Politiciaan(Maximo)nilijenga imani kubwa ya ushindi
 
Ni walewale wa Senegal tena? goal margin leo inatia moyo, ingawa kufungwa ni kufungwa tu. Mliotazama mechi tupeni taarifa za kiufundi.
so far huu hapa chini ndio msimamo baada ya mechi za kwanza.

1/8th final round
GROUP A
02-28-2009 Cote d'Ivoire 16:00 Senegal
02-28-2009 Zambia 16:00 Tanzania
02-25-2009 Tanzania 19:00 Cote d'Ivoire
02-25-2009 Zambia 16:00 Senegal
02-22-2009 Senegal 1 - 0 Tanzania
02-22-2009 Cote d'Ivoire 0 - 3 Zambia
Group A
Team MP W D L GF GA GD Pts
Zambia 1 1 0 0 3 0 3 3
Senegal 1 1 0 0 1 0 1 3
Tanzania 1 0 0 1 0 1 -1 0
Cote d'v 1 0 0 1 0 3 -3 0

GROUP B
03-01-2009 Ghana 16:00 RD Congo
03-01-2009 Zimbabwe 16:00 Libya
02-26-2009 Libya 18:00 Ghana
02-26-2009 Zimbabwe 15:00 RD Congo
02-23-2009 RD Congo 18:00 Libya
02-23-2009 Ghana 15:00 Zimbabwe

Ndio kwanza mwanzo wa safari. Imani yetu bado ipo sana tena ni asilimia 100.
 
Kiwango chetu kidogo sana. Maximo ameshindwa na aondoke...!!! We need serious mwalim awajenge vijana na sio maximo anaebahatisha hata kupanga list ya wachezaji.

Huyu Jamaa aliechangia kuhusu Ndumu...ilibidi nicheke tu...Maana wachezaji kama kina nyoso ambao wao kupata kadi sio tatizo.Na ndumu ndio huwafanya wachangamke..wanajizoesha vibaya mno.locally ktk soka wanakula sana ndumu na the so called ma-dr hakuna anaewacheck au kuwadhibiti....!!!

Sio siri Forward hatuna...na ndio maana Yanga wakaamua kuwachukua wakenya ktk forward.Japo nachukia kwanini hatuandai forward kali na akina Machupa na Lunyamila.

Pia ushirikina tuache...nasikia Mipira siku hizi tumekuwa tunaamini hatuwezi shinda hadi tuwe na waganga wa Jadi...na hilondilo linalopelekea ndugu zetu ALBINO kuteketea...Tuombe M/Mungu atuepushe na kila aina ya ushirikina.

Pia naona wachezaji wetu kama wanalishe DUNI...sijui wadau wenzangu mnaonaje?
 
Back
Top Bottom