JohnShaaban
JF-Expert Member
- Aug 23, 2007
- 464
- 116
Mkuu Mbu, nimependa uchambuzi wako; kwa ufupi yote yanachangiwa na "lack of determination" ambayo chanzo chake ni ubinafsi miongoni mwetu na ujinga katika kutambua vigezo vya mafanikio....kaka, hili tatizo linaanzia chini zaidi kuliko kiwango cha Maximo, tulikuwa na kina Mwinga Mwanjala, kina Nzael Kyomo, Zakayo Mwarekwa, kina Filbert Bayi, Nyambui na Shahanga huko kwenye Riadha,...hao wote walikuwa wanamichezo walotokea kwenye chimbuko la UMISETA, leo hii hebu taja mwanariadha hata mmoja ambaye hata akija Michael Johnson (400m world record holder) anaweza kutusaidia?
kwenye masumbwi tulikuwa na kina Emmanuel Mlundwa, Benjamin Mwangata, Isangura bros, Makoye na Willy, tulikuwa na kina Nassor Michael, Aloyce Ng'itu, familia ya kina Matumla... wengi wao walitokea Arnatouglo Hall, leo hii hatuna hata bondia mwenye kiwango hata cha kutuletea medali kwenye All african games... wapi michezo ya Majeshi?
Mara nyingi Mtanzania hafikirii zaidi ya "mimi nitafaidikaje" linapokuja suala la kutekeleza kazi fulani, sikatai kwamba hili ndio lengo kubwa la kufanya kazi. Lakini kibaya zaidi, hata akigundua nafasi ya yeye kufaidika, ubora wa utendaji wake anausitisha pale anapogundua kwamba ameshafaidika (tena kwa kigezo cha kijinga kwamba wale "aliotaka wamuone" tayari taarifa wanayo). "Simple mind" ya wengi wetu ndio tatizo kubwa kwa maendeleo ya Tanzania; mfano, jaribu kufikiria mchango ambao ungetolewa na Athumani Iddi na Haruna Moshi katika mechi ya leo kama wangekuwepo katika timu! Nina hakika ukifatilia kutokuwepo kwao kwenye timu utakuta ni sababu ambayo haitofautiani na niliyoongea hapo juu. Sababu hiyo hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa wachezaji wetu wasiweze kupata timu katika nchi za Magharibi; hatujiwekei malengo na hata tunapofanya hivyo tunaishia kubweteka kwa vigezo vya kipumbavu sana!
Bado tunahitaji mageuzi makubwa sana kifikra toka kwa mwananchi wa kawaida mpaka watendaji.