Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwanini afunge?, kwakuwa tumefungwa, manake bado mashindano yanaendelea,tutaitumia kutuma matokeo ya timu zilizofika nusu fainali.Mods plz funga thread hii
Mods plz funga thread hii
TFF wadaiwa imesahau baraka za wazee kwa Taifa Stars
Steven William, Muheza
UONGOZI wa Chama cha Soka Tanzania,(TFF) umetakiwa kuwashirikisha wazee katika masuala yao ya kuiandaa timu ya Taifa Stars pale inapokwenda kushiriki michuano mikubwa ya kimataifa ili wapate baraka za wazee hao.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Mbwana Msumari wakati akizungumza na Mwandishi wetu juzi ofisini kwake Barabara 16 jijini Tanga.
Alisema kuwa lazima Watanzania wakubali mila na desturi zao za Kiafrika zipo na ndiyo maana wazee wanataka wapewe nafasi ya kutoa maoni na dua zao katika timu hiyo ili ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Msumari alisema kuwa hata timu kubwa hapa nchini Simba na Yanga zinakamati ya wazee kwanini timu ya Taifa stars haitaki wazee.
Alisema kuwa wazee wa kijiji cha Kwamsisi wilayani Handeni mkoani Tanga wamesema kuwa wapo tayari kwa hilo lakini uongozi wa TFF umekaa kimya bila timu kupata baraka za wazee.
Msumari alisema kuwa hivi karibuni TFF iliunda kamati mbalimbali lakini cha kushangaza kamati ya wazee ambayo ni nyeti waliisahau.
Alisema kuwa kama Taifa Stars ingeagwa na wazee kwenda Ivory Coast katika michuano ya CHAN ingefanya vizuri zaidi
Source: Gazeti la Mwananchi
Hawa wazee wa Tanga wanatauta ulaji tu. Kwa nini wasianzie kwa Coastal Union na African Sport
Kweli wangeanzia huko kabla ya kugeuza klabu hizo kuwa nyumba za kuuzia juisi.....baraka zipi hizo...kwani hawaoni kuwa vijana walikuwa na bendera ya taifa kwenye jezi? Wangekaa na kutoa baraka zao huko waliko zingewafikia tu vijana....Na watupishe hapa!!Hawa wazee wa Tanga wanatauta ulaji tu. Kwa nini wasianzie kwa Coastal Union na African Sport
arrrrrg mods fungi na huyu Mfumwa......kwanini afunge?, kwakuwa tumefungwa, manake bado mashindano yanaendelea,tutaitumia kutuma matokeo ya timu zilizofika nusu fainali.
huyu nae katokea wapi?si vibaya tukipitisha macho na huku pia
RESULTS
Arsenal 0-0 Fulham
Chelsea 2-1 Wigan
Everton 2-0 West Brom
Middlesbrough 2-0 Liverpool
arrrrrg mods fungi na huyu Mfumwa......
huyu nae katokea wapi?
mkuu huko siku nyingi sipo........chama langu lilikuwa Napoli enzi za Careca....Katokea mtandaoni kaja kuthubiria habari njema za EPL kwi kwi kwi...Liverpool mdebwedoooo kama Washika bunduki tu
Kweli wangeanzia huko kabla ya kugeuza klabu hizo kuwa nyumba za kuuzia juisi.....baraka zipi hizo...kwani hawaoni kuwa vijana walikuwa na bendera ya taifa kwenye jezi? Wangekaa na kutoa baraka zao huko waliko zingewafikia tu vijana....Na watupishe hapa!!
Hawa wazee wa Tanga wanatauta ulaji tu. Kwa nini wasianzie kwa Coastal Union na African Sport
Naam timu hizo zingekuwa na mafanikio labda tungewaamini. Kwa maoni yangu kwanza kabisa TFF iwe na sera kwamba timu zote za zinazoshiriki ligi kuu ziwe na timu za watoto na timu ambayo itashindwa kutimiza hili ipewe adhabu kali hata kuzuiliwa kushiriki kwenye ligi.
Pili, nadhani kazi iliyofanywa na Maximo inatosha kabisa. Kiwango chake inaelekea kimefikia kikomo hana uwezo wa kuinyanyua juu zaidi Timu yetu zaidi ya hapo alipoifikisha, kwa hiyo inabidi kutafuta kocha mwingine mwenye uwezo zaidi ili ainue zaidi kiwango cha uchezaji cha timu yetu ya Taifa.
Tatu, migogoro ndani ya vilabu vyetu hasa Simba na Yanga inarudisha sana maendeleo ya soka Tanzania. TFF iweke mikakati ya kupambana na migogoro ndani ya vilabu hasa vilabu hivi viwili vikongwe. Sijui kiifanywe nini ili kuimaliza kabisa migogoro hii. Labda kuwe na adhabu kwamba klabu ambayo inakuwa na migogoro kila kukicha labda ipigwe faini kwa kuwa migogoro hiyo haizoreteshi klabu pekee bali hata soka la Tanzania. Haya ni maoni tu. Hongera timu ya Taifa mmejitahidi kadri ya uwezo wenu.[/B]