CHAN Finals: Live from Ivory Coast

CHAN Finals: Live from Ivory Coast

TFF wadaiwa imesahau baraka za wazee kwa Taifa Stars
Steven William, Muheza

UONGOZI wa Chama cha Soka Tanzania,(TFF) umetakiwa kuwashirikisha wazee katika masuala yao ya kuiandaa timu ya Taifa Stars pale inapokwenda kushiriki michuano mikubwa ya kimataifa ili wapate baraka za wazee hao.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Mbwana Msumari wakati akizungumza na Mwandishi wetu juzi ofisini kwake Barabara 16 jijini Tanga.

Alisema kuwa lazima Watanzania wakubali mila na desturi zao za Kiafrika zipo na ndiyo maana wazee wanataka wapewe nafasi ya kutoa maoni na dua zao katika timu hiyo ili ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Msumari alisema kuwa hata timu kubwa hapa nchini Simba na Yanga zinakamati ya wazee kwanini timu ya Taifa stars haitaki wazee.

Alisema kuwa wazee wa kijiji cha Kwamsisi wilayani Handeni mkoani Tanga wamesema kuwa wapo tayari kwa hilo lakini uongozi wa TFF umekaa kimya bila timu kupata baraka za wazee.

Msumari alisema kuwa hivi karibuni TFF iliunda kamati mbalimbali lakini cha kushangaza kamati ya wazee ambayo ni nyeti waliisahau.

Alisema kuwa kama Taifa Stars ingeagwa na wazee kwenda Ivory Coast katika michuano ya CHAN ingefanya vizuri zaidi

Source: Gazeti la Mwananchi
 
Mods plz funga thread hii

Usituzibe midomo mkuu, thread hii iachwe open kama nyingine, kwa nini ifungwe wakati watu bado hawaja vent emotions zao?. halafu mashindano bado yanaendelea kwani yameisha?, mi mshabiki wa Zambia je wewe?
 
si vibaya tukipitisha macho na huku pia
RESULTS
Arsenal 0-0 Fulham
Chelsea 2-1 Wigan
Everton 2-0 West Brom
Middlesbrough 2-0 Liverpool
 
TFF wadaiwa imesahau baraka za wazee kwa Taifa Stars
Steven William, Muheza

UONGOZI wa Chama cha Soka Tanzania,(TFF) umetakiwa kuwashirikisha wazee katika masuala yao ya kuiandaa timu ya Taifa Stars pale inapokwenda kushiriki michuano mikubwa ya kimataifa ili wapate baraka za wazee hao.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Mbwana Msumari wakati akizungumza na Mwandishi wetu juzi ofisini kwake Barabara 16 jijini Tanga.

Alisema kuwa lazima Watanzania wakubali mila na desturi zao za Kiafrika zipo na ndiyo maana wazee wanataka wapewe nafasi ya kutoa maoni na dua zao katika timu hiyo ili ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Msumari alisema kuwa hata timu kubwa hapa nchini Simba na Yanga zinakamati ya wazee kwanini timu ya Taifa stars haitaki wazee.

Alisema kuwa wazee wa kijiji cha Kwamsisi wilayani Handeni mkoani Tanga wamesema kuwa wapo tayari kwa hilo lakini uongozi wa TFF umekaa kimya bila timu kupata baraka za wazee.

Msumari alisema kuwa hivi karibuni TFF iliunda kamati mbalimbali lakini cha kushangaza kamati ya wazee ambayo ni nyeti waliisahau.

Alisema kuwa kama Taifa Stars ingeagwa na wazee kwenda Ivory Coast katika michuano ya CHAN ingefanya vizuri zaidi

Source: Gazeti la Mwananchi

Hawa wazee wa Tanga wanatauta ulaji tu. Kwa nini wasianzie kwa Coastal Union na African Sport
 
Hawa wazee wa Tanga wanatauta ulaji tu. Kwa nini wasianzie kwa Coastal Union na African Sport

Inawezekana Hasira zao ndio zimepelekea matokeo haya ya leo hadi tukatolewa..😀😀😀
 
Hawa wazee wa Tanga wanatauta ulaji tu. Kwa nini wasianzie kwa Coastal Union na African Sport
Kweli wangeanzia huko kabla ya kugeuza klabu hizo kuwa nyumba za kuuzia juisi.....baraka zipi hizo...kwani hawaoni kuwa vijana walikuwa na bendera ya taifa kwenye jezi? Wangekaa na kutoa baraka zao huko waliko zingewafikia tu vijana....Na watupishe hapa!!
 
em tuweni realistic kama umeangalia mechi live kama nilivyoangalia nadhani hautajiskia vibaya kuona tanzania tumetolewa na zambia kama wewe ni mfuatiliaji wa mpira wa siku nyingi,zambia walituzidi,tumejitahidi lakini wamestahili kushinda.
kusema kweli kama tunataka kushinda mechi kubwa bado kazi ipo,ile timu bado iko kwenye mafunzo,sio timu ya kuitegemea kuleta ushindi saana pale ambapo ushindi unatakiwa.sipati picha kama wale mabeki wetu wakicheza na brazil kwa mfano wa-ubavu wa kumzuia baptista au adriano,kwa vile tanzania ni nchi basi lazima tuandae timu yenye uwezo wa kupambana na nchi zingine.kwa hakika ile soka tunayo cheza hata china wanatufunga live...sitaki ku-offend die hard fans lakini independently speaking i dont have any hard feelings with the results,otherwise ni njia nzuri katika process nzima ya kujenga timu kucheza mashindano kama hayo na kufikia hapo tulipofikia manake hilo(kuandaa na kujenga timu) ndo hicho ambaacho kinatakiwa tukipe kipaumbele kwanza.
maximo aendelee kukiandaa timu kwa kuwa na long time plan na hatimaye baadae labda
tutaweza kuwa na timu inayo weza kupambana katika level ya kimataifa.
 
kwanini afunge?, kwakuwa tumefungwa, manake bado mashindano yanaendelea,tutaitumia kutuma matokeo ya timu zilizofika nusu fainali.
arrrrrg mods fungi na huyu Mfumwa......
si vibaya tukipitisha macho na huku pia
RESULTS
Arsenal 0-0 Fulham
Chelsea 2-1 Wigan
Everton 2-0 West Brom
Middlesbrough 2-0 Liverpool
huyu nae katokea wapi?
 
arrrrrg mods fungi na huyu Mfumwa......

huyu nae katokea wapi?

Katokea mtandaoni kaja kuthubiria habari njema za EPL kwi kwi kwi...Liverpool mdebwedoooo kama Washika bunduki tu
 
Katokea mtandaoni kaja kuthubiria habari njema za EPL kwi kwi kwi...Liverpool mdebwedoooo kama Washika bunduki tu
mkuu huko siku nyingi sipo........chama langu lilikuwa Napoli enzi za Careca....
Watanzania tunahitaji tiba.....
[ame=http://www.youtube.com/watch?v=qhxWrM9l5lg]YouTube - Yesu Nakupenda[/ame]
 
Kweli wangeanzia huko kabla ya kugeuza klabu hizo kuwa nyumba za kuuzia juisi.....baraka zipi hizo...kwani hawaoni kuwa vijana walikuwa na bendera ya taifa kwenye jezi? Wangekaa na kutoa baraka zao huko waliko zingewafikia tu vijana....Na watupishe hapa!!

Si unajua mambo ya 'Kamati ya Ufundi' tena Lol!
 
Hawa wazee wa Tanga wanatauta ulaji tu. Kwa nini wasianzie kwa Coastal Union na African Sport

Naam timu hizo zingekuwa na mafanikio labda tungewaamini. Kwa maoni yangu kwanza kabisa TFF iwe na sera kwamba timu zote za zinazoshiriki ligi kuu ziwe na timu za watoto na timu ambayo itashindwa kutimiza hili ipewe adhabu kali hata kuzuiliwa kushiriki kwenye ligi.

Kama mtakumbuka yule kocha toka Romani Victor Stancilaus aliyefundisha Yanga mwanzoni miaka ya sabini alianzisha timu ya watoto ambayo matunda yake yalisaidia sana timu za Yanga, Pan na hata timu ya Taifa. Wachezaji waliotamba katika soka la Tanzania kama akina Juma Pondamali, Mohamed Mkweche, Gordian Mapango, Adolph Rishard, Yahya Tostao na wengi wengine walitokana na timu ya watoto wa Yanga. Hii itasaidia sana katika kuinua kiwango cha soka siyo tu vilabuni hata pia kwenye timu yetu ya Taifa

Pili, nadhani kazi iliyofanywa na Maximo inatosha kabisa. Kiwango chake inaelekea kimefikia kikomo hana uwezo wa kuinyanyua juu zaidi Timu yetu zaidi ya hapo alipoifikisha, kwa hiyo inabidi kutafuta kocha mwingine mwenye uwezo zaidi ili ainue zaidi kiwango cha uchezaji cha timu yetu ya Taifa.

Tatu, migogoro ndani ya vilabu vyetu hasa Simba na Yanga inarudisha sana maendeleo ya soka Tanzania. TFF iweke mikakati ya kupambana na migogoro ndani ya vilabu hasa vilabu hivi viwili vikongwe. Sijui kiifanywe nini ili kuimaliza kabisa migogoro hii. Labda kuwe na adhabu kwamba klabu ambayo inakuwa na migogoro kila kukicha labda ipigwe faini kwa kuwa migogoro hiyo haizoreteshi klabu pekee bali hata soka la Tanzania. Haya ni maoni tu. Hongera timu ya Taifa mmejitahidi kadri ya uwezo wenu.
 
Naam timu hizo zingekuwa na mafanikio labda tungewaamini. Kwa maoni yangu kwanza kabisa TFF iwe na sera kwamba timu zote za zinazoshiriki ligi kuu ziwe na timu za watoto na timu ambayo itashindwa kutimiza hili ipewe adhabu kali hata kuzuiliwa kushiriki kwenye ligi.

...kabla ya timu kubwa kuwa na timu za watoto, michezo ya UMISHUMTA, na UMISETA ipewe kipaumbele, kisha chipukizi/wanafunzi wenye vipaji huko 'walelewe kimafunzo zaidi' kwenye timu za daraja la kwanza ama la pili za mikoa yao...

Pili, nadhani kazi iliyofanywa na Maximo inatosha kabisa. Kiwango chake inaelekea kimefikia kikomo hana uwezo wa kuinyanyua juu zaidi Timu yetu zaidi ya hapo alipoifikisha, kwa hiyo inabidi kutafuta kocha mwingine mwenye uwezo zaidi ili ainue zaidi kiwango cha uchezaji cha timu yetu ya Taifa.

...kaka, hili tatizo linaanzia chini zaidi kuliko kiwango cha Maximo, tulikuwa na kina Mwinga Mwanjala, kina Nzael Kyomo, Zakayo Mwarekwa, kina Filbert Bayi, Nyambui na Shahanga huko kwenye Riadha,...hao wote walikuwa wanamichezo walotokea kwenye chimbuko la UMISETA, leo hii hebu taja mwanariadha hata mmoja ambaye hata akija Michael Johnson (400m world record holder) anaweza kutusaidia?

kwenye masumbwi tulikuwa na kina Emmanuel Mlundwa, Benjamin Mwangata, Isangura bros, Makoye na Willy, tulikuwa na kina Nassor Michael, Aloyce Ng'itu, familia ya kina Matumla... wengi wao walitokea Arnatouglo Hall, leo hii hatuna hata bondia mwenye kiwango hata cha kutuletea medali kwenye All african games... wapi michezo ya Majeshi?

Serikali ikitaka, tutaweza pata kina Edibily Lunyamila na Dua Saidi wengi tu huko UMISHUMTA na UMISETA... nia tu ikiwepo...

Tatu, migogoro ndani ya vilabu vyetu hasa Simba na Yanga inarudisha sana maendeleo ya soka Tanzania. TFF iweke mikakati ya kupambana na migogoro ndani ya vilabu hasa vilabu hivi viwili vikongwe. Sijui kiifanywe nini ili kuimaliza kabisa migogoro hii. Labda kuwe na adhabu kwamba klabu ambayo inakuwa na migogoro kila kukicha labda ipigwe faini kwa kuwa migogoro hiyo haizoreteshi klabu pekee bali hata soka la Tanzania. Haya ni maoni tu. Hongera timu ya Taifa mmejitahidi kadri ya uwezo wenu.
[/B]

...Simba na Yanga ya miaka hii, haina tofauti sana na ile Simba na Yanga miaka ya kina Jabir Shikamkono na kina Ali Kiluvia, yaani kuziba zibia viraka kwa kusajili wachezaji toka mikoani... kina Mavumbi Omar, kina Yussuph Ismail Bana etc... Kama unakumbuka PAMBA enzi zao kina Masatu, Ngassa, Marsha, Fumo Felician, John Makelele wooote hawa walitokea mikoani na vipaji vyao, kama ilivyokuwa kwa vilabu vingine kama TUKUYU Stars, Majimaji Songea, nk...

Ni wakati wa kina Tostao, Adolph Rishard, Peter Tino, Pondamali na wengineo tu ndipo Dar es salaam nao walijitapa 'watoto' wa mjini kuunda timu ya taifa. Kwa mtizamo huo, bado naamini sana mafanikio ya timu ya taifa hayatatokana na Simba na Yanga tu, bali Mikoa yote Tanzania nzima, ndio maana naona umuhimu sana wa TAIFA CUP.

Kumtimua Maximo ni kumuonea tu, serikali kama ilivyo kwa sekta nyingine, imeshindwa kuweka mikakati ya kuendeleza vipaji kwenye michezo!
 
Back
Top Bottom