CHAN Finals: Live from Ivory Coast

CHAN Finals: Live from Ivory Coast

Nadhani Tatizo la Taifa stars lilikuwa kuanza ku defance tokea mwanzo. In my opinion ilikuwa tucheze free flowing football na kumuacha Ngasa mbele peke yake asingeweza kufanya kitu even though amejitahidi kadri ya uwezo wake.

Kama uliangailia mpira,utaona kuwa baada ya Maximo kurealise akanza kufanya substitution ili kubadili formation. Kama ulikuwa unamsikiliza mtangazaji alishangazwa sana na sub za mapema lakini Maximo alikuwa hana jinsi baada ya kuona kuwa kucheza kwa kudefense tusingeweza kupata bao.

Bado nina imani kama tutacheza kwa kushambulia tokea dk.ya kwanza na defence ikawa makini zaidi titafika nusu fainali.

Kila la heri Taifa Stars!!!
 
Mechi ya ZIMBAMBWE vs GHANA ni HF na matokeo ni 2-1 Zim wanaongoza
huku bao la kusawazisha za GHA likiwekwa kimiani na mtoto wa ABEID PELE, Ibrahim Ayew. Mimi nona Stars bado tuna nasafi maana wenzetu ZIM na ZAM amabao hawana majina wanafanya vizuri na mashindano haya ni ya wachezaji wa ndani kwa nini tusiperform??
 
Jana ilikuwa mara yangu ya kwanza kuangalia Taifa stars live. Wanamatatizo makubwa ya kiufundi. Na itachukuwa muda na juhudi kuyarekebisha.

Kwanza Taifa stars wana viungo ambao hawajiamini wanapokuwa na mpira. Soccer inaendeshwa na wachezaji viungo wanaojiamini na wenye uwezo wa kumiliki mpira na kufanya maamuzi sahihi. Hili bado kwetu ni tatizo. Mechi ya jana stars walishindwa kabisa kumiliki mpira na kumalizia pasi mara kwa mara.

Defenders wetu pia walikuwa waoga na hivyo kusababisha kona kadhaa ambazo zilikuwa zinatia hofu kutokana na ufupi wa wachechazi wetu. Kutokana na woga huu, defenders wakawa wanalazimisha kubutua mipira ambayo 90% iliishia miguuni mwa wapizani.

Bado hakuna maelewano miongoni mwa wachezaji. Ilikuwa vigumu sana kuona plans za wachezaji wetu katika ushambuliaji, umaliziaji na uokoaji. Kulitokea wakati kipindi cha pili mchezaji wetu alishindwa ku-control cross akiwa pekeyake kwasababu hakutegemea. Kulitokea wakati kipindi cha kwanza mchezaji wetu alitoa cross bila kumlenga mchezaji anayetakiwa amalizie cross yake.

Bado wachezaji wetu wanashindwa kusoma na kurekebisha kasi ya mchezo. Mfano wachezaji wetu walishindwa kutumia advantage ya mbio waliokuwa nazo. Wapizani wetu mwanzoni waliofu mbio zetu hivyo wakaweka ndefenders juu ya mstari wa maguu 18...cha ajabu walivyofanya hivyo sisi tukabaki nyuma tukicheza mpira wa taratibu, na wakaona hakukuwa na haja ya kuweka walinzi wao kwenye 18, na walipowaleta mbele tukawa matatani. Kwa kutotumia mbio zetu kipindi cha kwanza tukaonekana kama tulikuwa tunalazimisha draw au tunacheza kwa kujihami. Tulipokuwa tunatumia mbio na kuongeza kasi tulipata nafasi kadhaa.

Bado tunatatizo kubwa la kupiga free kicks na kona. Tulipata free kicks ambazo hazikuleta japo chembe hatari golini mwa wapinzani. Tunajuwa kwamba wachezaji wetu ni wafupi kulinganisha na wapinzani lakini bado free kicks zetu zilikuwa za juu. Sikuona sababu ya kutopiga short kicks (kugeuza free kicks kuwa short pass).

Goli tulilofungwa lilikuwa lakizembe mno, na linatokana na makosa niliyoyataja hapo juu. It is very simple, kama timu inawachezaji wafupi inatakiwa isiruhusu wachezaji wa timu pizani wapige cross. Hii ina maana kwamba mpira ukivuka mstari unaogawa uwanja kuelekea golini kwetu, viuongo na walinzi lazima wacheze man-to-man (police marking) ili kuzuia cross ambazo wanajuwa zitawashinda. Yule mchezaji wa Senegal aliyetoa cross alikuwa na muda wote wakuchagua apeleke wapi cross yake, na alipanga mapema hata kabla hajapata mpira, na Senegal walijuwa kwamba mipira ya juu itawapa ushindi.

Kipa wetu ingawa anastahili pongezi kwa kucheza vizuri sana kuliko wachezaji wote, bado alikuwa na uwezo wa kuzuia goli tulilofungwa kama ange ji-position vizuri. Simple: kipa anatakiwa kufanya maamuzi sahihi ya wapi asimame. Kukiwa na cross na kipa akajuwa kwamba hawezi kuikata (ku-intercept) kipa anatakiwa asimame katikati ya gori kwenye mstari au mita moja kutoka mstarini ili kuongeza ugumu kwa mfungaji kwani mfungaji atalazimika kuongoza mpira kwenye nyavu ndogo na kwa kasi, hii inaongeza chances za kukosa. Sasa kipa wetu huku akijuwa kwamba hasingeweza kuikata cross akaondoka kwenye mstari na kuwa nusu kipa nusu mlizi, laiti kama angekuwa kwenye mstari katikati ya goli angedaka bila ya papara. Kipa hafunzwi kudaka tu bali anafunzwa kufanya maamuzi ya positioning.

Hopeful tutasonga mbele pamoja na matatizo yetu.
 
Kipa wetu ingawa anastahili pongezi kwa kucheza vizuri sana kuliko wachezaji wote, bado alikuwa na uwezo wa kuzuia goli tulilofungwa kama ange ji-position vizuri. Simple: kipa anatakiwa kufanya maamuzi sahihi ya wapi asimame. Kukiwa na cross na kipa akajuwa kwamba hawezi kuikata (ku-intercept) kipa anatakiwa asimame katikati ya gori kwenye mstari au mita moja kutoka mstarini ili kuongeza ugumu kwa mfungaji kwani mfungaji atalazimika kuongoza mpira kwenye nyavu ndogo na kwa kasi, hii inaongeza chances za kukosa. Sasa kipa wetu huku akijuwa kwamba hasingeweza kuikata cross akaondoka kwenye mstari na kuwa nusu kipa nusu mlizi, laiti kama angekuwa kwenye mstari katikati ya goli angedaka bila ya papara. Kipa hafunzwi kudaka tu bali anafunzwa kufanya maamuzi ya positioning.
QUOTE]

MgonjwaUkimwi,

Upo? Mbona ndugu huwa unapotea hivyo???

Mchango wako mzuri!

Kipa jana alicheza safi..lile bao krosi ilipigwa kipa atajiandaa na mfungaji mrefu akadivert na kufunga kwa kichwa!

Kwa bao kama lile ni makipa wachache sana wangeuona ule mpira!
 


MgonjwaUkimwi,

Upo? Mbona ndugu huwa unapotea hivyo???

Mchango wako mzuri!

Kipa jana alicheza safi..lile bao krosi ilipigwa kipa atajiandaa na mfungaji mrefu akadivert na kufunga kwa kichwa!

Kwa bao kama lile ni makipa wachache sana wangeuona ule mpira!


Nipo Mzalendo, nipo kwa sana tu...ila kama unavyojuwa tena tumbo lazima liahangaikiwe.

Nakubaliana na wewe, kipa hakuona na ndio maana nilisema kama angebaki kwenye mstari angeona. Kumbuka kwamba yule kipa hasingeweza ku-intercept ile cross, alikuwa mbali. Kosa alilofanya ni kwenda mbele wakati walinzi wake wakijaribu kuufikia mpira sambamba na mfungaji.

Kipa ni kama dereva, dereva hasipoona barabara kwa umbali muafaka hatakiwi aende kwa speedi, wala ku-overtake. Kipa akiona hawezi kuufikia mpira na kwamba vision yake na mwendo au kasi ya mpira sio ya uhakika anatakiwa alinde goli.

Lakini kati ya yote kipa ni mchezaji bora wa mchezo wa jana, akifuatiwa na kapteni.
 
Jamani lakini tuache lawama, tunaweza kweli kulingana na senegal leo hii?? Mimi nadhani bado tunahitaji muda wa kujilinganisha na senegal.
 
Wacheni kujipa moyo ,longolongo za Maximo na wengine kuisifu Taifa Star ni kutuibia tu,Taifa hamna mpira kitu, halafu timu zenyewe walizopata ni za huko mgharibi aisee mbona tumeumia ,hao Wazambia tu watatutoa kamasi na mafua kwa kutuendesha puta , yaani najiona kama vile nami nimo uwanjani nimeshavaa koti 😀
 
mmmmmmmmmmmhhhh,mi chichemi,nkichema ntaambiwa sio mzalendo!
 
Tatizo wachezaji wanaonekana wamekosa confidence kabisa au labda hawakuvuta hizo bangi zao
 
Ukweli ni kwamba hatuma Washambuliaji ,ndio maana magoli yetu mengi yanafungwa na viungo halafu pia karibu wachezaji wetu wote ni wafupi na wana miili midogo
 
HALI inaweza ikawa shwari kwa Taifa Stars katika mchezo wake wa kesho dhidi ya Ivory Coast baada ya daktari wa timu hiyo, Juma Sufiani kubadili mpangilio wa chakula kwa wachezaji wa timu hiyo.

Hali hiyo imekuja baada ya baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kusumbuliwa na tumbo la kuhara mara kwa mara kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni mapishgi mabovu ya chakula hicho cha wenyeji ambacho hakitofautiana na cha Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, Sufiani alisema hali ya viungo Geofrey Bonny na Nurdin Bakari kusumbuliwa na tumbo la kuhara ghafla huku wengine wakilalamika kutojisikia vizuri imemfanya atilie mkazo kwa kubadili mpangilio wa chakula.

Sufiani alisema kuwa alitakiwa kupeleka mpangilio wa chakula (menu) kwa wahusika lakini utekelezaji ukawa si wa kuridhisha na kwa sasa ameamua kusimamia kwa ukaribu zaidi mfumo mzima wa utayarishaji wa chakula hicho.


"Siwezi kutoka nje kabisa ya chakula walichokizoea kula nyumbani, hii itawafanya wawe katika hali ya kawaida,” alisema daktari huyo.

Katika mchezo wake wa kwanza katika kundi A la michuano ya CHAN, Stars ilifungwa bao 1-0 na Senegal na kuiweka katika wakati wa kuhakikisha inashinda mchezo wa kesho ili iweze kusonga mbele.

Stars kesho itaingia uwanjani kucheza na Ivory Coast katika muendelezo wa michuano hiyo.

Source: Nifahamishe.com
 
Ndio kusema wanatengeneza mazingira ama.............? Ila sisi bado tunaamini mtashinda na kusonga mbele.
 
Nina uchungu sana kwa timu yangu ya Taifa Stars kupoteza mechi yake na Senegal kwa kukubali kipigo cha bao 1-0. Ninashindwa kuamini kama mechi ya leo na Ivory Coast kama tutashinda au la. Niwaombeni Watanzania wengine tuiombee timu yetu ili ipate ushindi. Ni majaliwa ya mwenyezi Mungu leo Taifa Stars kushinda kwani mara nyingi timu inapocheza nyumbani ni ngumu sana kushinda. Je jamani tumekuwa tukishindwa mara kwa mara, je wadau wa michezo tufanye nini ili tufike hata nusu fainali?
 
Mkuu mhache nadhani hii ilifaa kuwa katika jukwaa la michezo na sii hili jukwaa la habari mchanganyiko. Mods mngeipeleka kwa jukwaa linalostahili.
 
Siku zote nikisema tatizo Mwalimu hawanielewi, Maximo alitakiwa kuondoka mara tu baada ya kumaliza mkataba wake wa Mwanzo wakamuongezea kwa kisingizio ati kapandisha chat ya mpira wa Tanzania, wakati hajapata hata kufikia record ya rank tuliyowahi kuifikia mwaka miaka ya nyuma ambapo tulishika nafasi ya 65.
Pia kama wachezaji wana matatizo, ni nani anayechagua wachezaji kama si yeye Maximo? tangu aje hajaweza kuchukua kombe lolote katika ukanda huu, hata huko ivory cost hatukwenda kwa ujuzi wa Maximo bali kwa Udhamini mnono wa Serikali na wadau.
 
Maximo hana jipya tena.tuinamshukuru kwa kutufikisha tulipofika.
ila jitihada za kumtafuta coach mwenye uwezo zaidi zifanyike.
Maximi mzito sana kufanaya sub.unakuta mchezaji kapwaya mapemamapema anamwacha tuu anazunguka uwanjani
 
Leo mbona tunafungashwa vilago.
Maximo tatizo lake mbishi sana ana nini na Kaseja???
Gori tulilo fungwa la kizembe.....bora leo tufungwe 3-0.
 
Leo mbona tunafungashwa vilago.
Maximo tatizo lake mbishi sana ana nini na Kaseja???
Gori tulilo fungwa la kizembe.....bora leo tufungwe 3-0.
 
Leo mbona tunafungashwa vilago.
Maximo tatizo lake mbishi sana ana nini na Kaseja???
Gori tulilo fungwa la kizembe.....bora leo tufungwe 3-0.

Mimi Kaseja nilikuwa namfagilia alipokuwa Simba, sasa naona kachuja hata kama kachaguliwa na TASWA mchezaji bora wa Januari...ha ha haaaaaaaaa.

Fidel80 umzalendo kweli, unataka tufungwe 3-0. Mhh!, futa usemi wako. Hivi mechi ni saa ngapi saa za nyumbani?. KILA LA HERI WACHEZAJI WA TIMU YETU YA TAIFA, tuko nyuma yenu.
 
Back
Top Bottom