CHAN Finals: Live from Ivory Coast

wana JF, kama kumbu kumbu zangu zipo saya. Nadhani huu utakua ndiyo first major Win in continental tournaments... Mwaka 80 kule Nigeria tuliambulia sare na vipigo tu. its history.........
 
saafi sana,Tumshukuru Mungu. Ila Refa amekuaje kazidisha muda hivyo? Alikua anafidia time au ni vipi sasa
 

Mechi ingekuwa Bongo ingebidi tummezeshe filimbi referee kwa kutaka kuwabeba jamaa na kuongeza dakika chungu nzima ambazo hazikustahili. Pamoja na kushinda inabidi tupeleke malalamiko kuhusiana na yule referee.
 

Wazambia tutawaweza maana nao wana mili midogo midogo kama yetu,sema wanacheza kwa akili,tukijitahidi tunawabanjuwa.
 

Wachezaji wanaanza kujiuza hawa, nasi huenda tukaanza kusikia wachezaji wetu katika ligi kama za Ulaya. Soka ni uchumi, hivyo vijana wanatakiwa kupigana kufa na kupona kutafuta ushindi utakaolipa Taifa letu sifa, kuwaongezea kipato hapo watalaposajiliwa na timu kubwa na vile vile nasi wananchi tufaidike kwa nchi yetu kutangazwa nje na pia kuongeza mapato. Kila la HERI.
 
Mlio nyumbani huko vipi?
Maana najua sasa hivi grocery zinakuwa mchana...
 
Wazambia tutawaweza maana nao wana mili midogo midogo kama yetu,sema wanacheza kwa akili,tukijitahidi tunawabanjuwa.

hao wazambia wanatuhofia sisi, hata tulipokua kule uganda kwa ajili ya kombe la chalenji. kocha wao alikua akiiongelea Tanzania kama timu yenye kucheza kwa nidhamu na akili sana. Hivyo nao wapo cautious kidogo............ Hawa tutawaweza tu, wana beki mbovu ila foward zao zipo very sharp.
 
Refa king'ang'anizi yani unaona kabisa anavyoibeba timu mwishoni!
Taifa starz safi sana leo,wajitahidi zaidi maana shughuli bado inaendelea!
Maximo sijui atakuwa amefurahi vipi, inabidi wakishinda pia tumseme siyo wakifungwa tu!
Bravooo!..
 
Aisee mechi ijayo ni ngumu zaidi,inabidi tujipange na tucheze Jihad kweli kweli
 

Mkuu BAK umeniacha hoi, japo kwa wengine hii nyimbo tutakuwa/watakuwa wameisikia kama zilipendwa, basi kama una link yake tupe maana ya kale dhahabu.
 
ushindi wa Starz ni fungulia mbwa kwa watoto wa geti kali.......... kama nawaona vile jinsi ukimwi unavyosambaa huko jijini Dalisalama na vitongoji vyake.
 
Kwamba thread kule jukwaa la Michezo inayohusiana na mchezo wa Taifa Stars and Ivory Coast haijaonekana au haina umuhimu hadi ianzishwe nyingine katika jukwaa la siasa?
 
kesho utaona vijitu na mashati yao ya KIJANI eti kimbelembele vikidai "ooh sisi ndio mafanikio".......praak..wananikera wale jamaaa wa lumumba....
 
Mimi binafsi siyafagilii kabisa haya mashindano, sioni maana yake ni nini, nahisi hii idea ilitolewa na nchi ambazo hazina wachezaji wanaocheza Ulaya ili tu nao wapate sababu ya kukenua. Ushindi wowote utakaopatikana- tujue kwamba itakapokuja time ya mashindano 'serious' bado tutaendelea kuburuzwa kwa kuwa wenzetu hawatumii 'vifaru' vyao hapa. Mimi nataka tukicheza na Ivory Coast iwe ni first eleven yao regardless wachezaji wao wanacheza ulaya au uchina, kama ni Cameroon iwe hivyo hivyo- Eto' awepo,ikiwa hivi ndo tutapata true reflection ya kiwango chetu cha soka. Tuelewe kwamba hapa timu yetu inayoshiriki ni 'the best 11 tanzanian footballers' ndo wanashuka dimbani wakati wenzetu wanatutoa kamasi na wachezaji ambao hata hawajulikani and we are still struggling- lakini kama kawaida yetu- tunashangilia!!!
 
Mlio nyumbani huko vipi?
Maana najua sasa hivi grocery zinakuwa mchana..
.

Hapa namkumbuka EL, hii ingekuwa moja ya utekelezaji wa sera za chama. Nafikiria nyumbani hivi sasa leo watu watavunjiwa milango na vibaka kwa kisingizio cha kusheherekea ushindi watu wawe makini.
 
Kwamba thread kule jukwaa la Michezo inayohusiana na mchezo wa Taifa Stars and Ivory Coast haijaonekana au haina umuhimu hadi ianzishwe nyingine katika jukwaa la siasa?

kimekuuma na hiki pia.. duh!!

Taifa Stars oyeeeee.. hii nayo ni siasa kama huamini subiri kesho uone!
 
Wewe mwanakijiji vipi?,,,,hata kama tumeshinda ndio uanzishe thread nyingine si kuna ile kule kwenye michezo......bandwidth
 
Wewe mwanakijiji vipi?,,,,hata kama tumeshinda ndio uanzishe thread nyingine si kuna ile kule kwenye michezo......bandwidth

Na wewe pia kimekuuma! well

Politics na Siasa ni mapacha!!! wasiofanana! Tanzania oyeeeeeee!!! I mean unaweza kuendelea na kule kushangilia..
 
Kwamba thread kule jukwaa la Michezo inayohusiana na mchezo wa Taifa Stars and Ivory Coast haijaonekana au haina umuhimu hadi ianzishwe nyingine katika jukwaa la siasa?
anajaza bandwidth.....Mods please futa hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…