Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
![]()
KLHN News Alert:
Hatimaye refarii aliweza kukipata kipenga chake na kupuliza kwa uvivu kuashiria mpambano wa timu ya Taifa ya Tanzania na ile ya Ivory Coast ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani kufikia tamati.
kwa ushindi huo wa Taifa Stars inaonekan kibarua cha kocha wa timu ya Taifa ya Ivory Coast kinaelekea kuota nyasi baada ya timu kamambe ya Taifa Stars ya Tanzania kuibanjua timu yake bao moja bila katika michuano ya kwanza ya timu za Taifa za wachezaji wa ndani (CHAN) inayofanyika huko Ivory Coast. Bao hilo la Tanzania lilifungwa kwa gonga moja ya kichwa ya mshambuliaji machachari Mrisho Ngassa. Timu ya Tanzania ikicheza kwa kujiamini chini ya kocha wake Mbrazili Maximo iliweza vyema kulinda bao hilo liliopatikana dakika ya 38 ya mchezo huo. Kwa ushindi huo timu hiyo ya Tanzania imejiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea na mashindano hayo.
Mechi hiyo ambayo dakika za mwisho zilitafsiriwa na mashabiki wa Tanzania kama jitihada za refarii kuibeba Ivory Coast ilikuwa ni ya kusisimua na yenye mvuto wa aina pekee ambapo timu hiyo changa ya Tanzania imezidi kujijengea jina katika eneo la Afrika ya Magharibi.
Vijana angalau sasa watakuwa na Morali ya kimchezo, nadhani Zambia wahesabu siku za kuondoka. Sijui mechi za siku hiyo zitachezwaje, zinatakiwa zichezwe muda sawa ili kuondoa kukatisha tamaa wachezaji, manake mpaka sasa Zambia na Senegal wameshinda mechi moja na kudroo moja, wakati waTZ tumefungwa moja na kushinda moja. Hivyo nafasi yetu bado ngumu, manake Ivory Coast wao ni wa mwisho, naona mchezo waona Senegal wanaweza wawe wamekata tamaa.
Ila kwakuwa wana upinzani na Senegal, uko uwezekano Senagal wakawafunga ili kuwatoa kabisa. Nasi tukishinda kwa Zambia hapo tutasonga, ila tukitoa droo ama kufungwa tumekwisha.
Bao hilo la Tanzania lilifungwa kwa gonga moja ya kichwa ya mshambuliaji machachari Mrisho Ngassa. Timu ya Tanzania ikicheza kwa kujiamini chini ya kocha wake Mbrazili Maximo iliweza vyema kulinda bao hilo liliopatikana dakika ya 38 ya mchezo huo. Kwa ushindi huo timu hiyo ya Tanzania imejiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea na mashindano hayo.
timu hiyo changa ya Tanzania imezidi kujijengea jina katika eneo la Afrika ya Magharibi.
Wazambia tutawaweza maana nao wana mili midogo midogo kama yetu,sema wanacheza kwa akili,tukijitahidi tunawabanjuwa.
Nawatakia heri, viongozi wa TFF na wachezaji wote wa timu ya Taifa mwaka 2009 uwe wa mafanikio.
Nawatakia heri, viongozi wa FAT na wachezaji wote wa timu ya Taifa mwaka 72 uwe wa mafanikio. Kibaden oyeee oyeee kwa uchezaji bora kitwana oyeoyee. Wachezaji wote wa enzi hizo walitajwa katika wimbo huu. Nadhani baadhi yenu mtaukumbuka huu wimbo ulikuwa maarufu sana mwaka 72. Kuna haja ya kutunga mwingine kwa wachezaji wa sasa
Mlio nyumbani huko vipi?
Maana najua sasa hivi grocery zinakuwa mchana...
Kwamba thread kule jukwaa la Michezo inayohusiana na mchezo wa Taifa Stars and Ivory Coast haijaonekana au haina umuhimu hadi ianzishwe nyingine katika jukwaa la siasa?
Wewe mwanakijiji vipi?,,,,hata kama tumeshinda ndio uanzishe thread nyingine si kuna ile kule kwenye michezo......bandwidth
anajaza bandwidth.....Mods please futa hiiKwamba thread kule jukwaa la Michezo inayohusiana na mchezo wa Taifa Stars and Ivory Coast haijaonekana au haina umuhimu hadi ianzishwe nyingine katika jukwaa la siasa?